africa:kufa hufi ila chamoto unakiona

babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
13,087
15,981
1195535853_mtu.jpg
pole sana babu yangu.:(
 
Duh! Jamani! Babu kama huyu alitakiwa awe amepumzika baada ya kufanya kazi za mitulinga kwa miaka mingi. Ilitakiwa awe nyumbani na wajukuu wanamtania na kufaidi hekima zake. Sasa kwa umri huu kweli anabeba mzigo mzito kichwani. Hakika shida haina adabu. Sijui nani alaumiwe hapo! Naamini mfumo mzima wa jamii yetu!
 
dah kweli africa mbaya lakini ndo kwetu,yahitaji tujinyanyuee wenyewe
ndio hivyo mkuu,kwa wenzetu kibabu kama hiki kinahudumiwa kila kitu mpaka kupelekwa ****** na serikali,lakini sisi huko watu ni kupiga dili tu,kodi tunazolipa sijui zinaenda wapi,ndo zilitakiwa zihudumie wazee hawa wakifika umri huu
 
sidhani kama alifika salama na huo mzigo,nahisi alianguka maskini loh.
 
Hii Ndio Africa yetu na Tanzania pia

congo-firewood.jpg
Hawa hawana jinsi ila kuna nyingine tunajitakia kuna mama mmoja ana kisima anauza maji kwa majirani zake kwa adha ya kubeba ndoo kichwani majirani wamejinunulia mipira ili iwe rahisi kwao kupata maji yule mama hataki anataka kuona ndoo bombani, eti watamuibia shame!
 
huyu mama huu mzigo wote na mtoto juu, kweli afrika kuna tabaka kubwa sana kati ya maskini na mwenye nazo

Ping,
Unashangaa huyo mtoto na huo mzigo kichwani? si ajabu hapo ana mwingine tumboni, Mungu atunusuru WAAFRIKA.
 
Kawaida tu. Kwani maisha ya kijijini mageni kwenu, nenda kijijini ukazoeee
 
Hawa hawana jinsi ila kuna nyingine tunajitakia kuna mama mmoja ana kisima anauza maji kwa majirani zake kwa adha ya kubeba ndoo kichwani majirani wamejinunulia mipira ili iwe rahisi kwao kupata maji yule mama hataki anataka kuona ndoo bombani, eti watamuibia shame!
Kwa wale ambao maisha haya ni mageni kwenu, huyo mama kabeba kuni za miti fulani miepesi sana...usione ukubwa cha muhimu uzito.
 
kwakweli kina mama hasa wa africa shida ni kubwa mno na inasikitisha kweli:(
 
huyu mama huu mzigo wote na mtoto juu, kweli afrika kuna tabaka kubwa sana kati ya maskini na mwenye nazo
...Lakini si ndio hawa hawa unapofika uchaguzi wakapewa kanga, vilemba na pilau wanasema hakuna kama Nambari wani????
 
Back
Top Bottom