Africa hapakosi vituko: Rais wa Algeria mwenye miaka 81 ametangaza kugombea tena licha kuwa hata hawezi kutembea anatembelea kiti cha magurudumu

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,841
17,440
Rais wa Algeria (81) asema atagombea muhula wa tano wa urais
Feb 11, 2019 07:51 UTC
Rais Abdulaziz Bouteflika wa Algeria ametangaza kuwa atagombea muhula wa tano wa kiti cha rais, katika uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika mwezi Aprili mwaka huu.
Bouteflika ambaye hajakuwa akionekana hadharani kwa muda mrefu sasa kutokana na sababu za kiafya alitoa tangazo hilo jana Jumapili.
Rais huyo wa Algeria mwenye umri wa miaka 81 na ambaye anatumia kiti cha magurudumu kwa kuwa hawezi tena kusimama wala kutembea mwenyewe, hajaonekana hadharani tangu apigwe na kiharusi mwaka 2013.
Bouteflika ametangaza kuwa, karibuni hivi ataitisha 'Kongamano Jumuishi la Kitaifa' litakalozungumzia masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika, kuelekea uchaguzi mkuu wa Aprili 18.
Mapema mwezi huu, muungano unaotawala nchini Algeria ulimtangaza rasmi Abdulaziz Bouteflika kuwa mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya muungano huo katika uchaguzi ujao wa rais.
Hata hivyo vyama vya upinzani nchini Algeria vimemtaka kiongozi huyo mkongwe kutoshiriki kwenye uchaguzi huo wa rais, vikisisitiza kuwa hana uwezo wa kuliongoza tena taifa kutokana na umri mkubwa alionao na maradhi yanayomsibu.

Swali:Kwanini bado waalgeria wanampenda huyu mzee?kwani kafanya nini cha maana?binafsi sio mjuzi wa siasa za algeria
4bpo823740d7d813p37_800C450.jpg
4bse9c0f3f2ab51czxm_800C450.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamjua Winston lameck Spencer Churchill.
Alikuwa mbishi anagombea hadi uzeeni.
81 alikuwa bado PM. Kama Mzee havunji katiba agombee tu hakuna uafrika hapo.
 
Malkia wa Uingereza angekuwa mweusi watu wangesema sana ila kwa kuwa mzungu wanasema ni familia ya kifalme...
 
hapo mabashite wa Algeria wamemlazimisha agombee ili wajihakikishie ulaji ikumbukwe kuwa dingi ni mtia sahihi tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom