Afisa wanyama pori Kortini kwa Nyara za Serikali

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili washtakiwa watatu akiwemo afisa wanyama pori (KDU) ,Jonson Kadengele(34)Mkazi wa Njiro imeanza kusikilizwa katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha, ambapo shahidi wa kwanza ameieleza mahakama jinsi mshtakiwa alivyomkuta na Makucha sita , Jino moja ya Simba, mkia wa nyumbu kwenye pochi katika kiti Cha dereva ndani ya gari lake.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo namba 80/2019 ni pamoja na mshtakiwa namba moja Simon Kisima(48) ,Mkazi wa Kimandolu na mshtakiwa namba mbili ,Bernard Julius(24)Mkazi wa Ngusero wote Wakazi wa jiji la Arusha.

Akiongozwa na mwendesha mashtaka wa Serikali, Janet Sekule mbele ya hakimu ,Teophilo Nguvava wa mahakama hiyo shahidi huyo ,F6025 Koplo Frank baba ubaya(45) kutoka ofisi ya mkuu wa upelelezi (RCO) Arusha aliieza alivyomkamata mshtakiwa , Simoni Kisima akiwa na Nyara za serikali

Amedai kuwa siku ya tukio Agost 24 ,2019 majira ya jioni katika eneo la Sombetini Kwa diwani jijini Arusha,akiwa doria ya kawaida na wenzake alipata taarifa kuwa kwenye gari namba T 656 ABL aina ya Land cruiser Kuna nyara za Serikali.

Ameeleza kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo aliwasiliana na kiongozi wake wa kazi ,Inspekta Deo ambaye alimwamuru kukamata gari Hilo na kulifanyia upekuzi.

Alidai kuwa mara baada ya kulikamata gari hilo na kufanya upekuzi alikuta nyara za Serikali ambazo ni kucha sita na Jino moja za Simba na Mkia mmoja wa Nyumbu .

Aliieleza mahakama hiyo kwamba gari hilo ni Mali ya mshtakiwa namba moja , Simon Kisima ambaye alikuwa dereva wa gari hilo na mshtakiwa namba mbili Bernard Julius ambaye alikuwa ndani ya gari hilo, alifanikiwa kutoroka eneo la tukio.

Shahidi alidai kuwa baada ya kufanikiwa kumshikilia Mmiliki wa gari hilo mshtakiwa namba moja(Kisima)alidai atatoa ushirikiano wa kuweza kupatikana Kwa mshtakiwa namba mbili(Julias) ambaye alidai ndio mhusika wa nyara hizo.

Akihojiwa na wakili wa utetezi ,Kapimpiti Mgalula anayemwakilisha mshtakiwa wa tatu Jonson Kadengele anayetajwa kama mshtakiwa katika kielelezo cha mashtaka.

Wakili:je unafahamu kuwa idara yenu imekuwa ikilalamikiwa kwa kubambika kesi Watuhumiwa???

Shahidi;Nasikia.

Wakili:Kwa mujibu wa kielelezo Cha mashtaka kimeandikwa Jonson Kadengele ni Kama nani??

Shahidi: Shuhuda

Wakili :Kwenye taarifa yako wapi Jonson Kadengele alikupa taarifa ya ushuhuda wa tukio

Shahidi ;hakuna.

Wakili :je ni wapi katika kielelezo sehemu ya Watuhumiwa Jonson Kadengele aliandikwa alikuwepo eneo la tukio

Shahidi : hakuwepo.
 
Back
Top Bottom