Afisa wa tume: Tume yetu ya uchaguzi haina tofauti na ya Kenya

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,502
2,046
Akiongea na kituo kimoja cha redio hapa nchini, mkurugenzi msaidizi wa elimu ya mpiga kura kuhusu tathimini yake ya uchaguzi uliomalizika hivi karibuni nchini Kenya, amesema hakuna tofauti kubwa ya namna tume ya uchaguzi ya Kenya inavyotekeleza hilo jukumu na tume yetu.

Inaonekana huyu afisa ana jinsi yake ya kutafsiri mfanano.
 
hakuna tofauti kubwa
Hakuna tofauti kubwa kimsingi kwa sababu hizi nchi mbili tofauti kila nchi inaangalia namna nzuri ya kufanya mambo yake hivyo si lazima tufanane kila kitu hata kama kuna maboresho yanatakiwa kufanyika kwa Tume yetu ya uchaguzi ni sawa lakini sio kutaka tufanane kila kitu. Hata hao kenya nao wana changamoto vilvile ndio maana Odinga alienda mahakamani kulalamika kuwa ameibiwa kura ingekua mfumo wao ni mzuri kiasi hicho usingesikia malalamiko yoyote.

Rejea hata uchaguzi wa Marekani ambao ndio wanajiita mapapa wa demokrasia Trump nae alilalamika sana kuwa ameibiwa kura kwa hiyo tusitake copy and paste toka kenya hata Ruto wakati anatoa hotuba yake juzi alisema atazidi kuimarisha Tume yao maana yake ni kuwa anaona kuwa ina mapungufu. Hali ya amani na utulivu tulio nao sasa haivi ni matokeo ya kazi iliyofanywa na hii hii Tume kwa hiyo tusiwe wanyonge kiasi hicho ila tushauri namna bora ya kuboresha utendaji wa Tume yetu.
 
Nadhani haina tofauti na wewe unavyotafsiri hiyo kauli yake. Katiba ya Kenya imetoa mamlaka kwa Tume ya Kenya kwa namna ilivyoonelea inafaa sambamba na Katiba ya Tanzania ilivyokasimisha mamlaka kwa Tume ya Tanzania.
Execution ya majukumu inaweza kuwa sawa kulingana na maelekezo ya sheria mama.
Wafuasi wa Raila kule Kenya hawaitaki hata kuisikia hii Tume unayoiona wewe supa...
 
Tume zote linatekelezwa majukumu yake kwa mujibu wa katiba na sheria zake isipokuwa tunatifautiana kwenye maneno machache ambayo nayo yanatekelewa kwa mujibu wa katiba na sheria zilizotungwa kwa maslahi ya nchi husika
 
Watanzania tuache kujiaibisha kwa kulinganisha giza na NURU.Tume ya tanzania na wakurugenzi wote ni makada wa chama kimoja.labda mtwambie Yule mwenyekiti wa iebc alichaguliwa na Kenyatta ndo mtakuwa na hoja.vinginevyo ni kama unalinganisha mtoto wa darasa la saba na chuokikuu.
 
Fuatilia vizuri halafu uje na maelekezo ya kujitosheleza kuwa Chebukati aliteuliwa na nani?
 
Akiongea na kituo kimoja cha redio hapa nchini, mkurugenzi msaidizi wa elimu ya mpiga kura kuhusu tathimini yake ya uchaguzi uliomalizika hivi karibuni nchini Kenya, amesema hakuna tofauti kubwa ya namna tume ya uchaguzi ya Kenya inavyotekeleza hilo jukumu na tume yetu.

Inaonekana huyu afisa ana jinsi yake ya kutafsiri mfanano.
huyo anawaza kwa kutumia makalio badala ya kichwa
 
Hakuna tofauti kubwa kimsingi kwa sababu hizi nchi mbili tofauti kila nchi inaangalia namna nzuri ya kufanya mambo yake hivyo si lazima tufanane kila kitu hata kama kuna maboresho yanatakiwa kufanyika kwa Tume yetu ya uchaguzi ni sawa lakini sio kutaka tufanane kila kitu. Hata hao kenya nao wana changamoto vilvile ndio maana Odinga alienda mahakamani kulalamika kuwa ameibiwa kura ingekua mfumo wao ni mzuri kiasi hicho usingesikia malalamiko yoyote.

Rejea hata uchaguzi wa Marekani ambao ndio wanajiita mapapa wa demokrasia Trump nae alilalamika sana kuwa ameibiwa kura kwa hiyo tusitake copy and paste toka kenya hata Ruto wakati anatoa hotuba yake juzi alisema atazidi kuimarisha Tume yao maana yake ni kuwa anaona kuwa ina mapungufu. Hali ya amani na utulivu tulio nao sasa haivi ni matokeo ya kazi iliyofanywa na hii hii Tume kwa hiyo tusiwe wanyonge kiasi hicho ila tushauri namna bora ya kuboresha utendaji wa Tume yetu.
Acha unafiki, kuwa mkweli uwe huru. Wewe ni mtumwa wa mfumo unaolindwa na tume hii ya mwenyekiti wa ccm.
 
  • Ni sawa na kusema hakuna tofauti Kati ya katiba ya Kenya na katiba ya Tanzania.
  • Na mpaka kwenda on-air maafisa kadhaa wenzake wamemwandaa.
  • Kutetea 'ugali' si mchezo, watu mpaka 'wanaungua'.
 
Fuatilia vizuri halafu uje na maelekezo ya kujitosheleza kuwa Chebukati aliteuliwa na nani?
Chebukati alipatikana kupitia mchakato wa kikatiba- was not handpicked by Kenyatta. Usifikiri Kenya ni kama Tanzania ambapo mwenye kiti wa ccm anateua mwenyekiti wa neck, igp, majajii etc. Kenya wana judicial service commission, police service commission etc ambapo watu wanaotaka nafasi kama hizo wanaomba (application), wanapitia mchujo mkali (rigorous vetting), hatimae wanapatikana watu waadilifu na wasioegemea upande wote wanawekwa ofisini. Rais anapelekewa jina Moja au mawili kwaajili ya 'uteuzi rasmi'. Maofisa Hawa Wana kuwa huru kweli, sio kama hapa watu wanapewa vyeo Kwa kuangalia uswahiba na ukada.
 
Acha unafiki, kuwa mkweli uwe huru. Wewe ni mtumwa wa mfumo unaolindwa na tume hii ya mwenyekiti wa ccm.
Hapa ndipo mnapoharibu sasa kwa hiyo mtu akiwapinga mnasema analindwa na mfumo? acheni uzwazwa andikeni mambo ya msingi kama mtaendela kuandika vihoja tutavikataa hatupaswi kuunga mkono kila kitu hata kama si sawa
Rais anapelekewa jina Moja au mawili kwaajili ya 'uteuzi rasmi
Sasa hapa unakwepa nini? Kwa hiyo anaeteua Mwenyekiti wa Tume ni nani? unataka tena tuanze kubishana? au bado hujajua kuwa umejijibu?
 
Hapa ndipo mnapoharibu sasa kwa hiyo mtu akiwapinga mnasema analindwa na mfumo? acheni uzwazwa andikeni mambo ya msingi kama mtaendela kuandika vihoja tutavikataa hatupaswi kuunga mkono kila kitu hata kama si sawa

Sasa hapa unakwepa nini? Kwa hiyo anaeteua Mwenyekiti wa Tume ni nani? unataka tena tuanze kubishana? au bado hujajua kuwa umejijibu?
Soma taratibu mwanzo mpaka mwisho utaelewa.
 
Hapa ndipo mnapoharibu sasa kwa hiyo mtu akiwapinga mnasema analindwa na mfumo? acheni uzwazwa andikeni mambo ya msingi kama mtaendela kuandika vihoja tutavikataa hatupaswi kuunga mkono kila kitu hata kama si sawa

Sasa hapa unakwepa nini? Kwa hiyo anaeteua Mwenyekiti wa Tume ni nani? unataka tena tuanze kubishana? au bado hujajua kuwa umejijibu?

Kwani kwetu anateua kutoka kwenye majina mangapi anayoletewa kutoka wapi? Labda ungeanzia hapo kumwona mbayuwayu mkwepaji?
 
Hakuna tofauti kubwa kimsingi kwa sababu hizi nchi mbili tofauti kila nchi inaangalia namna nzuri ya kufanya mambo yake hivyo si lazima tufanane kila kitu hata kama kuna maboresho yanatakiwa kufanyika kwa Tume yetu ya uchaguzi ni sawa lakini sio kutaka tufanane kila kitu. Hata hao kenya nao wana changamoto vilvile ndio maana Odinga alienda mahakamani kulalamika kuwa ameibiwa kura ingekua mfumo wao ni mzuri kiasi hicho usingesikia malalamiko yoyote.

Rejea hata uchaguzi wa Marekani ambao ndio wanajiita mapapa wa demokrasia Trump nae alilalamika sana kuwa ameibiwa kura kwa hiyo tusitake copy and paste toka kenya hata Ruto wakati anatoa hotuba yake juzi alisema atazidi kuimarisha Tume yao maana yake ni kuwa anaona kuwa ina mapungufu. Hali ya amani na utulivu tulio nao sasa haivi ni matokeo ya kazi iliyofanywa na hii hii Tume kwa hiyo tusiwe wanyonge kiasi hicho ila tushauri namna bora ya kuboresha utendaji wa Tume yetu.
Unachomaanisha hapa ni kipi.maana unazunguka zunguka tu ili kutaka kutetea mambo mabaya.
 
Back
Top Bottom