Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 18,173
- 27,223
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Jijini Mwanza imemkamata Afisa wa TRA, Bi. Mary Moyo akipokea rushwa kutoka kwa Mfanyabiashara.
Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo, DAUD NDYAMUKAMA amesema mtuhumiwa Moyo aliomba rushwa ya tsh Milion 8 (8,000,000) kutoka kwa Mfanyabiashara huyo hili apunguzie malipo ya kodi.
Mtuhumiwa amefikishwa Mahakamani kwa ajili ya kusomemwa kesi yake.
--------
Afisa wa TRA Bi. Mary hatimaye amekamatwa, waliosema za mwizi ni arobaini hawakukosea kabisa.
Niwe muwazi moja ya kitu ambacho niliwahi kukata nacho tamaa ni TRA mkoa wa mwanza, nimeenda mara nyingi kwenye shughuli zangu nikitokea dar ili kuweza kuweka mambo sawa lakini nilikutana na kila aina ya usumbufu na dharau.
Mtu anataka umpatie pesa ila dharau anayokuonyesha sio ya kawaida, mimi bado siamini kama serikali inawatuma kufanya hivyo ila tu ni tabia zao ambazo wameamua kwa makusudi wawe nazo.
Pole sana Bi. mary, hii ni fundisho kwako na kwa wenzako hapo mwanza, za mwizi ni arobaini.
Nawapongeza sana Takukuru kwa hiki mlichofanya mwanza kwa kumuwekea mtego mtu huyu na pia nampongeza sana mfanyabiashara huyo kwa kwenda kutoa taarifa takukuru ili kukomesha hii tabia.
Kuna wakati niliwahi kuwaambia kuwa nitawashitaki takukuru na nilitaka kwenda kuwaambia takukuru ili tuwaekee mtego, lakini huruma iliniingia sana.
TRA jirekebisheni sio kila mtu ana huruma kama sisi wengine.