Afisa wa TRA mbaroni kwa kuomba rushwa ili asaidie ukwepaji wa kodi

Kataka $17,000 kapewa $1000 kakamatwa duuu sielewi ni hali mbaya au michezo, duuu.
 
Ofisa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Elias Yunus (38), anashikiliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Ilala kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Sh milioni 50 na kupokea Dola za Marekani 1,000 kwa ahadi ya kumsaidia mfanyabiashara aliyetaka kukwepa kodi na kujaza taarifa za uongo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 2, Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Enock Ngailo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuomba ushwa kwa mfanyabiashara Raia wa Uturuki (jina limehifadhiwa), ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya HEM Heavy Equipments Company Ltd.

Ngailo amesema ofisa huyo alitengeneza mazingira ya rushwa baada ya mfanyabiashara huyo kutoa taarifa za uongo katika usajili wa mtambo aliouingiza kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukwepa kodi.

“Kinyume na kifungu cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007, mtuhumiwa aliomba rushwa ya Sh milioni 50 na tayari amepokea Dola za Marekani 1,000 ili aweze kumsaidia mfanyabiashara huyo.

“Uchunguzi wa Takukuru umebaini mtuhumiwa aliomba rushwa hiyo na baada ya majadiliano alipunguza kiasi hicho na kufikia Sh milioni 35 kwa masharti ya kupewa fedha hizo zikiwa katika Dola za Marekani (Dola 17,000).
afanyiwe yanayostahili
 
Awamu ya 4 hapakuwa na Project na Rushwa iliwepo? hoja yako ni Mfu
Mekoo watu wataiba Sana tena kuliko awamu yeyote, sababu endelea Tu kuweka fedha Kwa elephant projects kuliko kuwekeza kwa watu
 
Yaani sasa hivi huku maofisini tunaogopana. Kila mtu ni mlinzi wa mwenzake. Kuna Rafiki yangu mpaka leo yupo Rumande tokea mwaka jana kisa sasa wale wa chini yake walifanya kosa flani yaani namuonea huruma sana naamini yupo innocent ila kosa lake alipitisha document kumbe kule field hii kazi haikufanyika yeye akapitisha kama imefanyika. Too sad.
Bado yule jamaa hajatoka? Du nilimuona siku moja amekonda sana. Duh halafu mke wake huku mitaani ni matanuzi kwenda mbele na gari ya jamaa.
 
Sote sisi ni wala rushwa au watoaji rushwa. Tofauti iliopo ni kwamba yeye amekamatwa na sisi tupo huru.
Simcheki mshkaji hata mm niliwahi kula rushwa.... sikudakwa enzi hizo..
ninachoshangaa huyu jamaa ameshindwaje kusoma alama za nyakati.... !!
majira ya sasa sio ya kipupwe ni kiangazi usiku mchana January to December...
Watumishi wa umma badilikeni shauri zenu!!?
 
TRA wamepandishiwa mishahara juzi karibu mara 2, bado wanaiba?

Anyway, mfuno wetu wa kodi unahitaji marekebisho makubwa maana bado unatoa mianya ya majadiliano ambapo hapo watu hujipigia hela.
 
kuna matiaraei ambao wanatembea nakigari chao cha stjei...tena wapo group

walichukua cash kisa risiti iliyoleta mzigo haiendani na bei halisi ya mzigo...

nikajitetea mzigo nimeagizia,na mawasiliano ya Supplier yapo kwa risiti... tena kwa hela cash na slip za bank ninazo! Hawakunielewa,wakaenda kuufungia.

Ray na genge lako,siku zinahesabika.!!

Utawasikia;"hizi hela ni ndogo tutagawanaje.!?" ukizidi kubembeleza;ndio wanakumaliza kabisa "huyu tumpeleke kwa Hasani akalipe milioni 5.!?"

"Shuka kwenye gari.!!''
 
Ofisa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Elias Yunus (38), anashikiliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Ilala kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Sh milioni 50 na kupokea Dola za Marekani 1,000 kwa ahadi ya kumsaidia mfanyabiashara aliyetaka kukwepa kodi na kujaza taarifa za uongo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 2, Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Enock Ngailo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuomba ushwa kwa mfanyabiashara Raia wa Uturuki (jina limehifadhiwa), ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya HEM Heavy Equipments Company Ltd.

Ngailo amesema ofisa huyo alitengeneza mazingira ya rushwa baada ya mfanyabiashara huyo kutoa taarifa za uongo katika usajili wa mtambo aliouingiza kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukwepa kodi.

“Kinyume na kifungu cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007, mtuhumiwa aliomba rushwa ya Sh milioni 50 na tayari amepokea Dola za Marekani 1,000 ili aweze kumsaidia mfanyabiashara huyo.

“Uchunguzi wa Takukuru umebaini mtuhumiwa aliomba rushwa hiyo na baada ya majadiliano alipunguza kiasi hicho na kufikia Sh milioni 35 kwa masharti ya kupewa fedha hizo zikiwa katika Dola za Marekani (Dola 17,000).

Tutawafunga sana hawa jamaa. Naona hawakomi. Temeke na Ilala ni matatizo matupu. Sasa ni mwendo wa kulipuana
 
Katika kipindi hiki kama wewe ni mla rushwa hutakiwi kua mtu mwenye tamaa i.e kama anaetoa rushwa hajaridhika usilazimishe ukilazimisha lazima mambo kama haya hutokea
Ahahahah mzeee kweli we unakula rushwa kwa kwenda na wakati, yaani mtu akupe rushwa huku akifurahi akiamini umemsaidia siyo unamkamua anatoa huku analaani....
 
kuna matiaraei ambao wanatembea nakigari chao cha stjei...tena wapo group

walichukua cash kisa risiti iliyoleta mzigo haiendani na bei halisi ya mzigo...

nikajitetea mzigo nimeagizia,na mawasiliano ya Supplier yapo kwa risiti... tena kwa hela cash na slip za bank ninazo! Hawakunielewa,wakaenda kuufungia.

Ray na genge lako,siku zinahesabika.!!

Utawasikia;"hizi hela ni ndogo tutagawanaje.!?" ukizidi kubembeleza;ndio wanakumaliza kabisa "huyu tumpeleke kwa Hasani akalipe milioni 5.!?"

"Shuka kwenye gari.!!''
Hao ni rahisi kuwadaka kama panzi mparage. Unawaingiza kingi jumla jumla.
 
OFISA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elias Yunus(38), anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Tsh. Milioni 50.

Elias inadaiwa aliomba rushwa hiyo kutoka kwa mfanyabishara raia wa Uturuki ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Hem Heavy Equipments baada ya kumtuhumu kwamba ametoa taarifa za uongo.

Inadaiwa raia huyo alitoa taarifa za uongo kwa ofisa katika usajili wa mtambo aliouingiza kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukwepa kodi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala, Enock Ngailo, alisema uchunguzi wa TAKUKURU ulibaini kwamba Ofisa huyo aliomba rushwa ya kiasi hicho na baada ya majadiliano alipunguza hadi kufikia Tsh. Milioni 35.

Ngailo alisema masharti ya fedha hizo zilitakiwa kupewa zikiwa katika dola za Marekani 17,000.

"Mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kupokea kiasi cha dola za Marekani 1,000 kama sehemu ya rushwa pia alikutwa akiwa na nyaraka mbalimbali za TRA alizokuwa anampelekea mfanyabishara huyo," alisema.

Alisema uchunguzi dhidi ya tuhuma umekamilika na atafikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma zinazomkabili.

Ngailo alitoa wito kwa watumishi wa umma pamoja na wafanyakazi kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwani madhara yake ni hasara kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

"TAKUKURU inatoa wito kwa wananchi wote kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa wakati huu ambao tunakwenda kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu," alisema.

TRA hawa jamaa hawasikii na wala hawajali kabisa. Ni wabinafsi mno. Wamezoea kula vya bure bure kisa wanasimamia kukusanya kodi. Kuomba mamilioni ni kitu cha kawaida mno sasa.
Takukuru waangalieni kwa jicho la karibu. Sio Ilala tu. Nendeni Temeke na kwingineko. Imetosha sasa. waanze kupata wanachotaka ili wajifunze
 
Unahifadhi jina,kisha unataja cheo chake na kampuni anayofanyia kazi.
Sasa kuna haja gani ya kuficha jina.
 
TRA wanasumbua wateja kwa rushwa wakae mkao wa kula. watalipuliwa sana. Naona wanafikiri ni utani.
Rushwa Africa ni janga coz wengi wetu ni wakosaji tukisema haki wengi wataingia jela mtu anajifanya anataka kuwa straight wakati ana makosa kibao ukimkomalia hoo serikali inanyanyasa yakubrash kiatu ana lalamika .
 
Ahahahah mzeee kweli we unakula rushwa kwa kwenda na wakati, yaani mtu akupe rushwa huku akifurahi akiamini umemsaidia siyo unamkamua anatoa huku analaani....
Hio ndo principle mkuu...ukijua hio principle uwe mla rushwa au muuza bidhaa kwa bei ghali mtu ataamini umemsaidia kumbe ndo vile vile una balance maisha...
 
Back
Top Bottom