Afisa wa TRA mbaroni kwa kuomba rushwa ili asaidie ukwepaji wa kodi

Wafanyakazi wa TRA wanajisahau sana, mara kwa mara wao tu ndo wana kesi za rushwa na bado hawakomi.!
 
Elias rafiki yangu ila ndio hivyo ajali kazini.

Nisiongee sana wakaja kutumia maandishi Yangu kama sehemu ya ushahidi.

Ila namkubali sana huyu mshikaji nitaenda kumtembelea gereza lolote atakalowekwa.
Ivumayo haidumu,ukileta za nzi ndiyo hivyo,ukipiga za mbele wenzako wanapiga za nyuma,kajaa bila kupenda
 
OFISA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Elias Yunus(38), anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Tsh. Milioni 50.

Elias inadaiwa aliomba rushwa hiyo kutoka kwa mfanyabishara raia wa Uturuki ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Hem Heavy Equipments baada ya kumtuhumu kwamba ametoa taarifa za uongo.

Inadaiwa raia huyo alitoa taarifa za uongo kwa ofisa katika usajili wa mtambo aliouingiza kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukwepa kodi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala, Enock Ngailo, alisema uchunguzi wa TAKUKURU ulibaini kwamba Ofisa huyo aliomba rushwa ya kiasi hicho na baada ya majadiliano alipunguza hadi kufikia Tsh. Milioni 35.

Ngailo alisema masharti ya fedha hizo zilitakiwa kupewa zikiwa katika dola za Marekani 17,000.

"Mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kupokea kiasi cha dola za Marekani 1,000 kama sehemu ya rushwa pia alikutwa akiwa na nyaraka mbalimbali za TRA alizokuwa anampelekea mfanyabishara huyo," alisema.

Alisema uchunguzi dhidi ya tuhuma umekamilika na atafikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma zinazomkabili.

Ngailo alitoa wito kwa watumishi wa umma pamoja na wafanyakazi kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwani madhara yake ni hasara kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

"TAKUKURU inatoa wito kwa wananchi wote kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa wakati huu ambao tunakwenda kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu," alisema.
Maria Sarungi na Fatima K wakatolee dhamani. Wanamonea Sana.... ha ha haaaaa.....
 
dogo wa UVCCM mikocheni
 
Simcheki mshkaji hata mm niliwahi kula rushwa.... sikudakwa enzi hizo..
ninachoshangaa huyu jamaa ameshindwaje kusoma alama za nyakati.... !!
majira ya sasa sio ya kipupwe ni kiangazi usiku mchana January to December...
Watumishi wa umma badilikeni shauri zenu!!?
Yaani sasa hivi huku maofisini tunaogopana. Kila mtu ni mlinzi wa mwenzake. Kuna Rafiki yangu mpaka leo yupo Rumande tokea mwaka jana kisa sasa wale wa chini yake walifanya kosa flani yaani namuonea huruma sana naamini yupo innocent ila kosa lake alipitisha document kumbe kule field hii kazi haikufanyika yeye akapitisha kama imefanyika. Too sad.
 
Elias rafiki yangu ila ndio hivyo ajali kazini.

Nisiongee sana wakaja kutumia maandishi Yangu kama sehemu ya ushahidi.

Ila namkubali sana huyu mshikaji nitaenda kumtembelea gereza lolote atakalowekwa.

Kwanini umuwazie kwenda gerezani?
 
TRA punguzeni rushwa jamaniiiiii
Mnapoteaaaaa kupotezaaa ajira
Mtaani hku vichwa vigumu ndy tunakuwezaaaaaa ohooooo

Ova
 
🤣 🤣

Kuna mambo ni ya ajabu sana...

Unaomba rushwa ya US$ 17,000 alafu unaenda kukamatwa na kutiwa hatiani kwa US$ 1,000 tu... hahahaha...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom