mitindo huru
JF-Expert Member
- Apr 26, 2016
- 1,607
- 1,596
Ni kweli mdau, na matokeo ya VAT kwenye transit goods ni kuongezeka kwa gharama za uingizaji wa mizigo hali itakayopelekea wafanyabiashara wa Congo, Zambia, Rwanda, Burundi n.k kutumia bandari za Mombasa, Beira Msumbiji au hata South Africa kwani nao wanafanya marekebisho kwenye sheria zao za transit.This solution is the best.
Kama tatizo ni wafanyabiashara kushusha mizigo njiani, watafute jinsi ya kuzuia hilo tatizo. Kuweka VAT kama suluhu ya tatizo sio sawa.
Wakumbuke hiyo VAT imesababisha mizigo kushuka bandarini, kuna watu wameajiriwa kwenye kusafirisha hiyo mizigo. Hao watu hawana ajira tena.
TRA wanatumia vibaya matamko anayotoa Rais JPM kuhusu kodi hivyo wanataka kufanya mambo kwa nguvu bila kuzingatia hali halisi na sheria za kimataifa kuhusu VAT kwenye transit goods.