Afisa wa TRA aliyetuhumiwa kumiliki magari 19 kusomewa maelezo ya awali Desemba 6

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Dar es Salaam. Ofisa Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi, Desemba 6,2017 atasomewa maelezo ya awali.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kumiliki magari 19, mali inayodaiwa hailingani na kipato chake halali.

Jennifer ameshtakiwa chini ya kifungu cha 27, (1) (a) na (b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Maelezo hayo yalipaswa kusomwa leo Jumanne Novemba 7,2017 lakini Wakili wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter amesema bado hawajamaliza kuyaandaa.

Ameiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine. Upande wa utetezi uliowakilishwa na wakili Elisaria Mosha haukuwa na pingamizi.

Hakimu Huruma Shaidi ameahirisha kesi hadi Desemba 6,2017, mshtakiwa atakaposomewa maelezo hayo.

Jennifer anadaiwa kati ya Machi 21,2016 na Juni 30,2016 jijini Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa TRA kwa cheo cha Ofisa Forodha Msaidizi alikutwa akimiliki magari 19.

Magari hayo ni Toyota RAV4 mbili, Toyota Dyna Truck, Toyota Vitz, Suzuki Carry, Toyota Ipsum, Toyota Wish mbili, Toyota Mark II, Toyota Mark X, Toyota Regiusage, Toyota Estimated, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota Crown, Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Passo na Suzuki Carry.

Katika hati ya mashtaka imeelezwa magari hayo yana thamani ya Sh197.601 milioni mali ambayo inadaiwa hailingani na kipato chake halali.

Anadaiwa kati ya Machi 21,2012 na Machi 30,2016 jijini Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa TRA mwenye cheo cha Ofisa Forodha Msaidizi alikutwa akiishi maisha ya kifahari ya thamani ya Sh333.255 milioni fedha ambayo inadaiwa hailingani na kipato chake halali.

Mshtakiwa aliyekana mashtaka hayo baada ya kusomewa yupo nje kwa dhamana.

Chanzo: Mwananchi

Soma kisa chake chote hapa=> Afisa msaidizi wa Forodha TRA, Jennifer Mushi afikishwa Mahakamani kwa kumiliki magari 19 na kuishi maisha ya kifahari

Mytake: Serikali itashinda kesi au ndo mwanzo wa watuhumiwa kuachiliwa kama akina Masamaki au kesi inafika mahali mara jamuhuri inaiondoa kesi mahakamani.

Nadhani kama tumeamua kufanya kazi tuhakikishe tunaweka siasa pembeni na kutumia weledi siyo mihemko.
 
Eti magari kumi na tisa ndio hadi kesi ??utajuaje kama mshahara wake alikuwa anaufanyia biashara ??Ccm wivu
 
Wonder shall never end, et tatzo ni magari 19 yenye thaman ya mil 198, kwaio angemiliki toyota landcruiser mpya new model kama wanazomiliki wao ya mil 400 sio tatzo?
 
Nitampa zawadi ya gari 2 aina ya Toyota land cruiser maana nimegundua ni mteja wetu mzri sana kwa kampun ya Toyota. Anamiliki Toyota 16 kati ya magri 19 ni jambo LA kushkru sana
 
hivi mtumishi kama analima zake huko kibaigwa atazikosa hizo gari?
 
Unapo sema ccm wivu ina maana huyu mama mtuhumiwa ni wa chama kipi ambacho kina bariki wizi/uhujumu?
 
Magari 19 kwanza ushuru tu kuyalipia ni balaa magari yenyewe thamani yake ndogo.
 
Back
Top Bottom