Afisa wa NIDA na Watanzania Hii ni sawa?

Ruwamangi

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
910
1,596
Ndugu Wanajamiiforums Naomba kujua hili maana huyu afisa wa Vitambulisho Vya Taifa Nida amenihangaisha sana Sijui ni sahihi kutumia lugha hiyo. Lakini sijui kama kuna mwingine anapitia changamoto Kama hii au ndio mfumo wa Nida usiotaka kusikiliza kwangu tu? Nilijiandikisha Nida 2018 kwa majina Matatu sawa na sheria inavyoelekeza

Lakini sasa kulingana na Mambo ya kifamilia nikaona si vyema ni tumie Ubini wa katikati nikataka Kubadilisha Nikaenda Nida Wakanituma majina ninayo yataka niwapelekee kilelezo viwili au vitatu nikawapelekea cheti cha kuzaliwa, cha ubatizo na deed poll ya kukana hayo majina na nikalipia 20k nikasubiri wakatuma makao Makuu Nida. Nimerudi wananiambia bado cha shule sasa kwa bahati mbaya sina hicho chenye majina ninayo yataka elimu ya Msingi nilisoma na majina ambayo hayapo hayapo Nida wala kwenye Deep poll.

Je, nikiwapelekea hicho cheti cha elimu ya Msingi watakubali au danadana zitaendelea tu naombeni msaada wenu kwa wenye uelewa na haya maswala
 
Ungefungua mkono wako toka siku ya kwanza huo mzunguko wote usingekuwepo. Inaelekea umeenda kikuda toka siku ya kwanza kupuuzia ishara ulizopewa na afisa za kumaliza mambo.

Ukataka orodha ya vielelezo. Sasa baada ya karatasi ya shule utaambiwa ukalete cheti cha kuzaliwa cha babu yake babu yako.

Hii Bongo mzee, jiongeze.
 
Peleka cheti Cha darasa la saba
Kina majina tofauti na niliyo jisajili nayo Nida je watakubali maana naohofia nisije anza huo mchakato wa kukitafuta niwaletee aseme tena hiki ni tofauti
 
Daah hao jamaa stawasahau walinihangaisha takribani mwaka na miezi sita, sikutaka kutoa hongo kwa maana nilikuwa najua ni haki yangu kupata ikafika shemu nikachoka nikaamua kujilipua nikamwambia officer mmoja akataka nimpe 50 ndani ya wiki napata, nikampa hela kwa kumtumia kwenye simu kweli baada ya siku kama nne hivi akanambia ID yako tayari. nikaenda kuichukua nilivyomaliza tu kusaini nikamchimba mkwara nikamwambia kumbe mnatuzungusha maksudi ili tuwape hela sio sasa nakwambia hivi hiyo elfu 50 lazima ikugharimu stay prepared. Ebhana eeeh yule dada alihaha balaa akanirudishia hela yangu na samahani za kutosha
 
Daah hao jamaa stawasahau walinihangaisha takribani mwaka na miezi sita, sikutaka kutoa hongo kwa maana nilikuwa najua ni haki yangu kupata ikafika shemu nikachoka nikaamua kujilipua nikamwambia officer mmoja akataka nimpe 50 ndani ya wiki napata, nikampa hela kwa kumtumia kwenye simu kweli baada ya siku kama nne hivi akanambia ID yako tayari. nikaenda kuichukua nilivyomaliza tu kusaini nikamchimba mkwara nikamwambia kumbe mnatuzungusha maksudi ili tuwape hela sio sasa nakwambia hivi hiyo elfu 50 lazima ikugharimu stay prepared. Ebhana eeeh yule dada alihaha balaa akanirudishia hela yangu na samahani za kutosha
Pole sana ilikuwa ni issue ya ku change Jina?
 
Nduga Wanajamiiforums Naomba kujua hili maana huyu afisa wa Vitambulisho Vya Taifa Nida amenihangaisha sana Sijui nisahihi kutumia lugha hiyo. Lakini sijui kama kuna mwingine anapitia changamoto Kama hii au ndio mfumo wa Nida usiotaka kusikiliza kwangu tu?
Nilijiandikisha Nida 2018 kwa majina Matatu sawa na sheria inavyoelekeza

Lakini sasa kulingana na Mambo ya kifamilia nikaona si vyema ni tumie Ubini wa katikati nikataka Kubadilisha Nikaenda Nida Wakanituma majina ninayo yataka niwapelekee kilelezo viwili au vitatu nikawapelekea cheti cha kuzaliwa, cha ubatizo na deed poll ya kukana hayo majina na nikalipia 20k nikasubiri wakatuma makao Makuu Nida. Nimerudi wananiambia bado cha shule sasa kwa bahati mbaya sina hicho chenye majina ninayo yataka elimu ya Msingi nilisoma na majina ambayo hayapo kwenye Deep poll.

Je nikiwapelekea hicho cheti cha elimu ya Msingi watakubali au danadana zitaendelea tu naombeni msaada wenu kwa wenye uelewa na haya maswala
 
Peleka kila ulichoambiwa, mambo si mengi japo naona una haraka sana
ni cheti cha darasa la saba Kina majina tofauti na niliyo jisajili nayo Nida je watakubali maana nahofia nisije anza huo mchakato wa kukitafuta niwaletee aseme tena hiki ni tofauti
 
Haya mambo yanakera sana unaweza ukajikuta unajulikana mpaka na mfagizi maana kila siku uko ofisi za nida
Nilienda Nida hadi nikakata tamaa wanashida gani jamaniii mbona miaka inazidi kuyoyoma why wameazisha jambo hili na hawako tayari kumaliza
 
Ni mwaka sasa umekwisha tangu nifanye huo mchakato na bado sijafanikiwa hawa jamaa ni shida nimetumia 270k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom