Evarist Chahali: Kuna kiongozi wa nchi jirani ana "compromising information" kuhusu kiongozi mmoja "Mkubwa"

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Huu ni ujumbe wangu kwako binafsi ewe Afisa Usalama wa Taifa mwenye uchungu wa dhati na nchi yako. Natambua ugumu wa wewe kuafiki haya nitakayoandika lakini naiachia nafsi yako ikutume au ikusute.

Najua umeshaskia mengi kuhusu Chahali. Na pengine kila ulilosikia si zuri. Lakini nina hakika hakuna mtu mmoja atakayeweza kukutajia kwa hakika kosa hasa la Chahali ni lipi.

Na hapa sizungumzii huo mpango wa kidhalimu wa Bashite, Kitwanga, na genge lao la Kanda ya Ziwa chini ya maelekezo ya Bwana Mkubwa kwa kumtumia Musiba kunitaja miongoni mwa “watu hatari.” Uzuri ni kwamba nina akili zaidi yao, nilipikwa nikapikika, nafikiria hatua elfu mbele yao, natambua kila wanalopanga. Hawa wazembe nawamudu. What do you expect katika timu ambayo ndani kuna mlevi mbwa Kitwanga na kichwa empty Bashite?

Hakuna atakayetaka kugusia utendaji kazi wa Chahali tangu alipokuwa "kitengo maalum" (pekee kilichowahi kuchanganya surveillance na field work) mara baada ya kutoka chuoni.

Hakuna atakayegusia utendaji kazi wa Chahali alipokuwa mwanafunzi chuo kikuu, akitumia vema kifuniko chake cha uandishi wa habari, akijulikana kama Ustaadh Bonge huku akiwa field officer wa "Kanda." Hakuna atakayekwambia mchango wake katika kudhibiti "kunji" pale Mlimani.

Pia hakuna atakayekwambia kuhusu utendaji kazi wa Chahali kwenye dawati la CI (Counterintelligence). Naam, alikuwa miongoni mwa maafisa wachache waliokuwa wanapambana na ujasusi.

Na hakuna atakayekwambia kuwa baada ya kufanya vizuri kwenye dawati la kuzuwia ujasusi, alipewa promosheni na kuwa Mkuu wa Kanda C. Hutopewa fursa ya kuongea na maafisa waliokuwa chini ya "bosi Chahali" hata wale ambao "Pajero yake kama Mkuu wa Kanda na dereva wake vilikuwa kama vya kila afisa, kwani alithamini kila mtu."

Na hawatakuruhusu uende majimbo ya Temeke na Kigamboni yaliyokuwa maeneo yake ya Kanda, ili ujue alifanya kazi vipi na sources.

Na hawatokwambia kuwa Chahali ndio mtumishi pekee katika historia ya Idara ya Usalama wa Taifa kuandika kitabu cha Kiswahili kuhusu taaluma hiyo, kitabu ambacho kimesaidia sana kuwafahamisha Watanzania umuhimu wa kazi yenu ninyi maafisa, sambamba na kuondoa dhana potofu dhidi yenu.

Hawatokwambia kuwa wakati flani ninyi maafisa mlishauriwa kusoma kitabu hicho kwa vile kina manufaa mengi. Lakini baadaye Bashite akaanzisha kampeni ya fitna kuwatisha wauzaji wa vitabu akidai kimepigwa marufuku.

Jiulize, kama Chahali ni “mtu mbaya kiasi hicho,” kwanini tulishauriwa kusoma kitabu chake? Na pengine hujakisoma, wasiliana nami kwa baruapepe niliyoweka mwishoni mwa makala hii, nikupatie kopi yako, “unihukumu vizuri.”

Hawatokwambia kwa sababu unaweza kuhisi kwamba Chahali hana kosa isipokuwa ameponzwa na uzalendo wake. Au labda kama afisa, hakupaswa kuwakosoa mafisadi hadharani licha ya kuwa alikuwa akitumia cover yake ya uandishi wa habari.

Lakini la muhimu sio umpende Chahali au umhurumie. Nafahamu kuwa wewe afisa kama binadamu una utu pia. Huenda ukaumia nafsi kufahamu kuwa kuna operesheni iliandaliwa mwaka 2013 kutuma watu huku Uingereza kumdhuru Chahali. Unaweza kunihurumia baada ya kutafakari "walitaka kumuuwa kwa kosa gani hasa?" Lakini pia unaweza kupatwa na hasira baada ya kufahamu kiasi gani kilitumika katika operesheni hiyo ilhali walioipanga hawakujihangaisha kufahamu iwapo taasisi za kishushushu za Uingereza zinafahamu dhamira za kumdhuru Chahali. Na ndio maana operesheni hiyo ilifeli.

Huwezi kuambiwa kuwa Julai 2015 maafisa kadhaa walipewa operesheni ya kumsubiri Chahali airport wakitarajia angekuja kwenye msiba wa baba yake. Hawatokwambia kuwa siku moja kabla ya mazishi ya baba yake, maofisa watatu - wanaume wawili na mwanamke mmoja walienda kwenye msiba na wakaendelea kufuatilia hadi kaburini. Kwa kosa gani alilotenda Chahali?

Na mwaka jana mwezi wa tano hivi Bwana Mkubwa hakupendezwa na makala flani ya Chahali katika gazeti la Raia Mwema, akamtuma poti wake (namba mbili hapo) aandae operesheni dhidi ya Chahali. Huyo poti wa Bwana nae hatosema kuwa nilimtumia barua ya kumuonya kuwa nafahamu anachopanga.

Nimeshasema huna haja ya kumhurumia Chahali na wala hahitaji huruma yako. Hata hivyo, kama mzalendo mwenye uchungu wa dhati kuhusu Tanzania yako basi usiendelee kukaa kimya huku nchi yako inateketea. Usikae kimya huku Bashite, poti wa Bwana Mkubwa, akaigeuza Idara kuwa ofisi yake binafsi. Akaitumia kwa maslahi yake binafsi.

Usikae kimya huku maafisa wa idara ya nchi jirani wanaichezea Idara yetu tukufu kwa vile tu Bwana Mkubwa ni anapelekeshwa na kiongozi wa nchi hiyo, jasusi mzoefu ambaye yeye na kitengo cha nchi hiyo wana "kompromat" (compromising information) kuhusu Bwana Mkubwa na wanaitumia kama leverage (kama picha la Putin na Trump)

Usikae kimya wakati unafahamu kuhusu kinachoitwa "Kikosi Maalum" ambacho kinafanya kila baya dhidi ya watu ambao aidha Bwana Mkubwa hawapendi au mwanae Bashite anataka kuwakomoa. Hicho "Kikosi Maalum" ni sawa na Idara nje ya Idara. Neno la kitaalam ni rogue element, na kamwe usiruhusu kitu hicho.

Kwahiyo kama umeguswa na ujumbe huu ufanyaje? Kwani chuoni hamkufundishwa jinsi ya kutetea maslahi ya nchi pindi utawala uliopo madarakani unapokwenda kinyume na maslahi ya nchi? Wewe na wenzio sio waajiriwa wa chama flani wala waaajiriwa wa Bwana Mkubwa. Wewe na wenzio mmeajiriwa kuwalinda na kuwatetea Watanzania. Hiyo OP na mshahara mkubwa sio sababu ya kuwasaliti Watanzania wenzio.

Jiulize, "kama sio mimi ni nani?" Kwa sababu kama hali ikiachwa iendelee kama ilivyo sasa, itafika mahali haitoweza kubadilishwa. Udini, ukabila, ukanda, upendeleo, ubaguzi, uonevu, nk hatimaye vitaiharibu Tanzania yetu. Lakini wewe na wenzio mna nafasi ya kuzuwia haya, iwapo tu mtaamua kuwa WAZALENDO.

Basi naomba nisikuchoshe sana. Tafakari sana nilichoandika. Najua wakubwa hawatokipenda. Pengine kitawafanya waandae operesheni ya haraka ya kumdhibiti Chahali. Na hapo jiulize "kwanini wanamhofia sana?" Labda wanafahamu uwezo wake ndani na nje ya kitengo. Lakini hilo sio muhimu kama swali "kwanini hawana uchungu kwa nchi hii hadi wanaipeleka huko inakoelekea?" Chukua hatua. Ukijiskia, wasiliana nami kwa secure email hii evarist@protonmail.ch (usihofu kuwa labda watadukua akaunti zangu na kufahamu mawasiliano yangu nawe. Hawawezi. Lakini pia ukiniandikia, sihitaji kufahamu jina lako). KAZI KWAKO

Mungu Ibariki Tanzania
 
Huyu bwa' mkubwa amechafukwa na kitendo cha Musiba kumjumuisha kwenye kundi la "Watu hatari" kwa Usalama wa nchi.

Hii barua ya leo naona kwa mtazamo wangu imejawa na ukakasi wa hali ya juu kwa mazingira ya nchi yetu au niseme nchi za kiafrika kwa ujumla..

Ninavyoona the guy is slowly turning into another Mange Kimambi. An outsider critic.
 
Sisi Raia wa kawaida tunapata faida na vitabu vyako. Maadamu idara ikijiridhisha na kitabu chako naamini tutafaidika na mengi kama tulivyofaidika na kitabu chako cha mwanzo.

Mbili hongera sana kwa kutumikia taifa lako, una akili lakini sasa una tatizo moja ambalo watu wengi wenye akili na kufanya makubwa huwa nalo. Linaitwa Narcissistic personality disorder
 
Chema chajiuza kibaya chajitembeza.Naona mleta maada anajifagilia sana mtu mzuri mwaka jana au juzi si lazima awe mzuri mwaka huu.Ameongea sana kwa past tense zaidi vipi kwa present tense chahali yule wa past tense ndie yule wa present tense? Mbinu hizo alizotumia enzi za kale za past tense ndiizo zinahitajika sasa kiasi kuwa ajione super hakuna wa kumuweza? La pili mtu ukiondoka ofisi ya serikali hata kwa mwaka mmoja usije jifanya unaijua ofisi uliyotoka vizuri huwa kuna mabadiliko mengi ambayo uliyekuwepo ukaondoka unakuwa outdated
 
Sisi Raia wa kawaida tunapata faida na vitabu vyako. Maadamu idara ikijiridhisha na kitabu chako naamini tutafaidika na mengi kama nilivyofaidika na kitabu chako cha mwanzo.

Mbili hongera sana kwa kutumikia taifa lako, una akili lakini sasa una tatizo moja ambalo watu wengi wenye akili na kufanya makubwa huwa nalo. Linaitwa Narcissistic personality disorder
Mkuu hcho kitabu kinaitwaje na kinauzwa wapi hapa dar
 
Huyu jamaa ukimsoma vizuri utangua kuwa ana matatizo kifikra. Anasumbuliwa na paranoia!

His self-imposed insecurities have reached a level that makes it impossible to relax. He needs to take a closer look at the signs of paranoia that are raising the severity of his social anxiety.

Anahitaji kuonana na Daktari wake.

Huyu kwa saa hana tofauti sana na Dk Shika

Tangia taifa la Tanzania lizaliwe umeishasikia mtu wa usalama wa taifa akijitangaza achilia mbali kujigamba kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye ana akili sana kuzidi wafanyakazi wengine wa usalama wa Taifa.
 
Chema chajiuza kibaya chajitembeza.Naona mleta maada anajifagilia sana mtu mzuri mwaka jana au juzi silazima awe mzuri mwaka huu.Ameongea sana kwa past tense zaidi vipi kwa present tense chahali yule wa past tense ndie yule wa present tense? Mbinu hizo alizotumia enzi za kale za past tense ndiizo zinahitajika sasa kiasi kuwa ajione super hakuna wa kumuweza? La pili mtu ukiondoka ofisi ya serikali hata kwa mwaka mmoja usije jifanya unaijua ofisi uliyotoka vizuri huwa kuna mabadiliko mengi ambayo uliyekuwepo ukaondoka unakuwa outdated
Ndio Mkuu naskia huko kumetokea mabadiliko ya hali ya juu sana.
 
Huu ni ujumbe wangu kwako binafsi ewe Afisa Usalama wa Taifa mwenye uchungu wa dhati na nchi yako. Natambua ugumu wa wewe kuafiki haya nitakayoandika lakini naiachia nafsi yako ikutume au ikusute.

Najua umeshaskia mengi kuhusu Chahali. Na pengine kila ulilosikia si zuri. Lakini nina hakika hakuna mtu mmoja atakayeweza kukutajia kwa hakika kosa hasa la Chahali ni lipi.

Na hapa sizungumzii huo mpango wa kidhalimu wa Bashite, Kitwanga, na genge lao la Kanda ya Ziwa chini ya maelekezo ya Bwana Mkubwa kwa kumtumia Musiba kunitaja miongoni mwa “watu hatari.” Uzuri ni kwamba nina akili zaidi yao, nilipikwa nikapikika, nafikiria hatua elfu mbele yao, natambua kila wanalopanga. Hawa wazembe nawamudu. What do you expect katika timu ambayo ndani kuna mlevi mbwa Kitwanga na kichwa empty Bashite?

Hakuna atakayetaka kugusia utendaji kazi wa Chahali tangu alipokuwa "kitengo maalum" (pekee kilichowahi kuchanganya surveillance na field work) mara baada ya kutoka chuoni.

Hakuna atakayegusia utendaji kazi wa Chahali alipokuwa mwanafunzi chuo kikuu, akitumia vema kifuniko chake cha uandishi wa habari, akijulikana kama Ustaadh Bonge huku akiwa field officer wa "Kanda." Hakuna atakayekwambia mchango wake katika kudhibiti "kunji" pale Mlimani.

Pia hakuna atakayekwambia kuhusu utendaji kazi wa Chahali kwenye dawati la CI (Counterintelligence). Naam, alikuwa miongoni mwa maafisa wachache waliokuwa wanapambana na ujasusi.

Na hakuna atakayekwambia kuwa baada ya kufanya vizuri kwenye dawati la kuzuwia ujasusi, alipewa promosheni na kuwa Mkuu wa Kanda C. Hutopewa fursa ya kuongea na maafisa waliokuwa chini ya "bosi Chahali" hata wale ambao "Pajero yake kama Mkuu wa Kanda na dereva wake vilikuwa kama vya kila afisa, kwani alithamini kila mtu."

Na hawatakuruhusu uende majimbo ya Temeke na Kigamboni yaliyokuwa maeneo yake ya Kanda, ili ujue alifanya kazi vipi na sources.

Na hawatokwambia kuwa Chahali ndio mtumishi pekee katika historia ya Idara ya Usalama wa Taifa kuandika kitabu cha Kiswahili kuhusu taaluma hiyo, kitabu ambacho kimesaidia sana kuwafahamisha Watanzania umuhimu wa kazi yenu ninyi maafisa, sambamba na kuondoa dhana potofu dhidi yenu.

Hawatokwambia kuwa wakati flani ninyi maafisa mlishauriwa kusoma kitabu hicho kwa vile kina manufaa mengi. Lakini baadaye Bashite akaanzisha kampeni ya fitna kuwatisha wauzaji wa vitabu akidai kimepigwa marufuku.

Jiulize, kama Chahali ni “mtu mbaya kiasi hicho,” kwanini tulishauriwa kusoma kitabu chake? Na pengine hujakisoma, wasiliana nami kwa baruapepe niliyoweka mwishoni mwa makala hii, nikupatie kopi yako, “unihukumu vizuri.”

Mambo hayo!!
 
Back
Top Bottom