Afisa uhamiaji Mwanza anusurika kuuawa kwa risasi na polisi

Ukiwa na pesa tu zaidi ya Police kwao ni jambazi, maana wao ndio wanajua matumizi yake
 
pole sana rafiki Albert.Ushauri omba Mungu sana ndiye aliyemsaada wako.Mahakamani na polisi huwezi kupata haki yako bila kumshirikisha Mungu
 
huyu RPC wa mwanza ana kitu ngoja tutakiona ana lake jambo na anaonekana mpenda ubwanyenye sana km mwanasiasa ivi..
kweli polisi njaa tu tulionao
 
ninge kuwa ni mimi ni afisa uhamiaji,ni bora kuanza upya maana sio ujinga kuliko kupoteza uhai kwa nyumba ama mali ambazo naweza kuzipata muda wowote ule.
ningemwachia tu mali huyo mama,maana anakoelekea sasa ni mauaji ambayo ni kuacha majonzi kwa ndugu na jamaa.
polisi mtatumaliza kwa hizo intelijensia zenu za kuchonga
 
"Hili ni tukio la bahati mbaya, jeshi laetu lilipata taarifa za Kiinterejensia juu ya kuwapo kwa majambazi na kuamua kuweka mtego, sasa afisa huyu alifika muda na wakati ambao askari wetu walikuwa eneo hilo na kuingia katika mtego wetu, alikuja na gari ambalo ni sawa na lile ambalo tulielezwa kuwa lingetumika, lakini bahati nzuri mauaji hayakutokea," alifafanua kamanda huyo.

Kamanda Barlow amedai kwamba kutokana na tukio hilo amepanga kukutana na afisa huyo wa uhamiaji na kuzungumza naye akiwa na askari wake kutafuta suluhu ya jambo hilo ambalo aliekeza kwamba yeye anaamini limetokana na bahati mbaya.

red panahusika sana:
1.hivi ina maana ata kama ni jambazi mmemkamata mnaaza na kumchapa risasi wamuue ata kama hakuwa na silaha wala kuleta purkushani zozote????ivi ndo polisi hawa wanavyofanya kazi?
2.jamabzi hana haki mbele ya sheria yeye ni kuhukumiwa kifo tu kila polisi wanapomkuta?
3.ningekua mimi ningebanana nao kituo cha haki za binaadamu na kesi mahakamani
 
Aise mkuu wa uhamiaji peleka swala lako haki za binadamu ungeshuka wangekumaliza kama walivyommaliza Kombe!!

Bado najiuliza Mkuu,hivi wangemuua story ingekuwaje?
Ingefanana na ya Kombe kabisa!!!
Eti bahati mbaya!!!!!!Waache utani na roho za binadamu
 
PAMBAF intelijensia!! Intelijensia!! intelijensia ya kuua raia wema tu!! Plain stupidity!! mburuze huyu mpuuzi kwa pilato!! haya majambazi yanayoitwa polisi yatatumaliza. Intelijensia imeua Arusha, imeua Mwanza, imeua Iringa!!
kuanzia sasa,wananchi hatutaki intelijensia tena,maana inamaliza hata wasiohusika,eti intelijensia ilisema jambazi atatumia gari linalofanana na afisa uhamiaji,hahahahahahaha,ili mhalalishe kifo cha afisa uhamiaji,duuuuuu
napiga BAN intelijensia kwa miaka 3,hadi hapo tutakapo tafuta kihalalishi kingine cha kuhalalisha kutoa roho
 
Uzembe wa namna hii haukubaliki na hasa kufanywa na watu tunaoamini ni walinzi wetu! Hakuna cha suluhu hapo bali hatua za kinidhamu lazima zichukuliwe!

Mkuu, naomba nitofautiane nawe hususan hapo kwenye wekundu.
Nionavyo mimi, ule haukuwa uzembe, ni mauaji yaliyokuwa yamepangwa kwa lengo maalum na kisha kisingizio kiwe intlijensia yao iliwaaminisha kwamba waliyemuua ni jambazi, au alikuwa akijihusisha na ujambazi bila watu kujua.

Kwa nchi zinazofuata sheria, huyo askari alitakiwa afunguliwe mashitaka ya kosa la kutaka kuua, na mahakama imsafishe kama alichokisema kikionekana kina ukweli.

Pole sana mkuu aliyekoswa koswa, Mungu bado anakupenda.
 
....alizidi kufafanua.

Buchafwe alisema amepatwa na mashaka na tukio hilo kutokana na asakri huyo aliyehusika kuwa na mahusiano ya karibu na mkewe ambaye wamekuwa na ugomvi naye pamoja na kesi ya kutalikiana mahakamani na kusema kwamba huenda ahalikuwa la bahati mbaya.

"Nina kesi na mke wangu mahakamani, na afisia huyu wa polisi amekuwa na mahusiano ya karibu na mke wangu huyu ambaye tunashitakiana mahakamani, inanishangaza kwamba mtu ambaye ananifahamu licha ya kujitambulisha bado alikuwa akishilikilia msimamo wa kunitaka kushuka, nadhani hapa kuna jambo zaidi ya hali ilivyo," alieleza.


Aidha akizungumzia tukio hilo ........

someni hapo ktk red
 
mbona wamezoea?
Wakitaka kukupora mali yako wanakuua na kudai ni jambazi.....
Sasa haya wakitaka kukupora mke watakuua wadai ni jambazi.....

Kiufupi polisi ni jeshi la mauaji, rushwa na kila aina ya dhuluma
 
Basi watatuua wengi.Ina maana kama gari langu limefafana na lamajambazi basi wao ni kuua tu halafu uhakika mbele ya safari du. Hii kali.
 
Usishangae hapa kuna bifu la rushwa. Maana hao watu wa uhamiaji kwa rushwa hamna mfano duniani. Malizaneni sisi tunaangalia tu. Maana mshatugeuza shamba la bibi. Mnatuua sisi sasa mkiuana nyinyi kwetu ni vita ya panzi ati.
 
Dah yani mke wachukue, mali wachukue bado na kukuua tena??

Tanzania tunakoelekea sio kabisa na hizi "Police extrajudicial killings" tutachapana risasi sana huko mbeleni pale kila mtu akiamua kujilinda na chamoto chake
 
hahahaha inteligensia yetu hata FBI NA CIA wanasubiri...yaani ni wa pili kwa upelelezi duniani..hihihihi
 
Kauli hii, "Aidha akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza alikiri kuwapo kwake na kudai kwamba anayo hakika kwamba tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya kwani jeshi lake lilipata taarifa za Kiinterejensia za kuwapo kwa majambazi wakidaiwa kutumia gari sawa na ambalo afisa huyo wa uhamiaji alikuwa nalo," mbona inanikumbusha sababu za mauaji ya Marehemu Amran Kombe!?
 
Huyu Kamanda Liberatus Barlow lyimo ingawaje yeye hapendi kutambulishwa kama "Lyimo" ametoa sababu za hovyo kabisa Intelejensia,hili neno limekuwa ni chaka la kuficha vitendo viovu vya Polisi
 
hahahaha inteligensia yetu hata FBI NA CIA wanasubiri...yaani ni wa pili kwa upelelezi duniani..hihihihi

"Intelijensia"

Intelijensia ya polisi ina uwalakini.
Intelijensia yangu nisiye mtaalamu wa mambo ya ulinzi na usalama imeniambia hivi.Bwana Albert ameripoti ofisi za usalama leo asubuhi tukio hilo.Ambapo usalama walimjulisha RPC kwamba bwana Albert angekwenda kufungua Jalada la Uchunguzi wa tukio hilo.Lengo la Bwana Albert Kureport Usalama kwanza kabla ya Polisi, ni hofu ya watu wake wa karibu kwama ,pengine baada ya kufika Polisi wangemuweka ndani kwa madai kwamba walikua wakimtafuta kutokana na tukio hilo la kijambazi.

Intelijensia yangu inazidi kusema kwamba baada ya bw albert kureport Usalama na Usalama kuongea na RPC,RPC alipanga appointment ya saa nane, ambapo Bw.Albert alikwenda pamoja na afisa Usalama, kwa ajili ya kufungua Jalada hilo.Jalada limefunguliwa ila nimeshindwa kupata namba yake kwani Bw. Albert analikumbatia kwelikweli. Na pia kuna baadhi ya Maofisa waliokua na Bwana Albert pale "Mkunguni' usiku kabla hawajaagana, nao pia walikua wakihojiwa.

Intelijensia inazidi,Kwa mujibu wa redio Mbao,Bwana Albert alikua na mke wake wa kwanza , ambaye anawatoto nae wakubwa kuliko wa huyu ambaye alipofika ugenini,akaanguka katika dhambi na kumtosa wa zamani ambaye inaonekana hata kwao walikua na uwezo mzuri kifedha.

Mke huyu aliye naye sasa inaonekana anadai talaka kwa Udi na Uvumba,hii inaonyesha kwamba anataka wagawane mali,kitu ambacho bw albert hakuwa tayari.Hivyo basi Habari za Kiintelijensia zinaonyesha kwamba Mke huyu waliyetengana yuko nyuma ya Pazia ya kile kilichotaka kutendeka, ambacho ni mauaji ili arithui malim za marehemu.

Kutokana na Intelijensia yangu na habari niliyoweka hapa juu, Ni ushauri wangu kwa Bw. Albert kurudi nyumbani na kuomba radhi kwa yaliyotokea ili aweze kundelea kuishia kwa amani.Huyu Mke wa sasa alikua kimaslahi zaidi
 
Jeshi la polisi ni nyenzo muhimu sana kwa serikali ya CCM yenye viongozi waliodhamiria kuishi juu ya sheria wanazowawekea wananchi wengine: laws are for wimps! Linawasaidia kudhibiti wapinzani wa ndani (ya chama) na nje na kulinda ulaji wao wa moja kwa moja au kupitia "wawekezaji". Kama malipo, wameliachia mianya ya kutumia nguvu kwa maslahi binafsi. Ndio maana hakuna anayejali au kusimamia haki za raia wanaponyanyaswa na jeshi hilo. Hata askari kutesa na/au kuua mtu asiye na silaha sasa ni jambo linalokubalika na kulindwa! Anyway, what goes around comes around.
 
Back
Top Bottom