Afisa NHC Mahakamani kwa kutaka rushwa ya Tsh. Milioni 4 ili mpangaji asihamishwe

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Afisa Miliki, Fadhil Kasegese amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka mawili ambayo ni kuomba rushwa ya Sh4 milioni na kupokea rushwa ya Sh3 milioni.

Kasegese anadaiwa kujipatia fedha hiyo kutoka kwa Vishal Dharsi ili asimtoe kwenye ' Apartment ' aliyokuwa amepanga iliyopo Mtaa wa Msimbazi Kariakoo, inayomilikiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka leo, na wakili wa Serikali Mwandamizi Mwanakombo Rajabu akisaidiana na Henry Mahengo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Ramadhani Rugemarila.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 3, 2023 na Aprili 6, 2023 katika ofisi za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Ilala jijini hapa.

Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili amekana kutenda na yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom