Afisa Mtendaji wa Kata ya Mkuyuni, Mwanza ashikiliwa kwa kubaka mwanafunzi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Jeshi la Polisi jijini Mwanza wanamshikilia ofisa mtendaji wa Kata ya Mkuyuni, Bwana James Chiragwire kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi wa darasa la 3 mwenye umri wa miaka 12.

Habari zilizopatikana kutoka shule anayosoma mtoto huyo na kuthibitishwa na Ofisa Habari wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Oscar Msuya tukio hilo lilitokea juzi baada ya walimu kubaini matatizo ya kiafya ya mwanafunzi huyo aliyeshindwa kuingia darasani na kulala nje ya uzio wa shule.

-----------------
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mkuyuni Wilayani Nyamagana mkoani Mwanza James Chiragwire (42) anashikiliwa na Polisi kwa kosa la kumbaka mtoto ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Nyabulogoya darasa la tatu mwenye umri wa miaka 11 jina limeifadhiwa

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa awali kabla ya kutokea kwa tukio hilo alikuwa na mazoea ya kumchukua mtoto huyo na kuingia naye ndani kwake na kumpatia fedha na zawadi ndogondogo ndipo siku hiyo alipofika nyumbani kwao na alimkuta mtoto peke yake alimchukua na kumfunga kitambaa usoni kisha akaingia naye ndani kwake na kumfanyia ukatili huo.

Mtoto huyo aliyefanyiwa uchunguzi na daktari na kubainika kweli ameingiliwa kimwili na kwa sasa yupo katika hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure akiendelea kupata matibabu na uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi wa polisi Augustino Senga anetoa wito akiwataka wakazi wa mwanza kuwa makini wakati wote na watoto wadogo, na kusema kuwa wasiachwe peke yao ili kuhepusha vitendo kama hivyo.

Chanzo: EATV
 
Yaani huyo mtendaji apewe adhabu kali sana,mimi nina kinyongo sana na hawa watendaji wa kijiji na watendaji wa kata,wengi wao hawana maadili wamekua wakitongoza wake za watu wanaoripoti kwenye vituo vya kazi na pale wanapowakataa wanajaribu kuwazungushazungusha pale wanapohitaji huduma za ruhusa ya kusafiri na huduma nyinginezo.Wengi wao wanaonekana kama miungu watu.
 
Hizi mambo huwa nazihusisha na Imani za kishirikina, na sio tamaa za kimwli. Haiwezekani mtu na akili zako timamu ubake kitoto cha Cha miaka 12 na wakati wanawake wa kila size wamejaa tele mitaani.

Apigwe mvua huo.
 
Watendaji kata wana kiherehere sana kuishabikia ccm, na hayo ndio maadili yao .
 
Back
Top Bottom