Afisa mtendaji kata Lulembela awafikisha mahakamani baadhi ya watumishi kwa kutolipa mchango aliouanzisha

Mtz kwanza

Member
Sep 5, 2021
7
2
Afisa mtendaji kata ya Lulembela wilaya ya Mbogwe mkoani Geita leo tarehe 6 September 2021 amewafikisha mahakamani baadhi ya watumishi (Walimu na wataalamu wa afya) kujibu shauri alilolifungua (KUPINGA MAENDELEO) katika mahakama ya mwanzo Lulembela.

Katika shauri hilo walilosomewa watumishi hao lilidai wanapinga maendeleo ya kata kwa kutokuchangia mchango aliouanzisha mtendaji huyo.

Ikumbukwe kuwa watumishi hukatwa pay as you earn kila mwezi ambayo inachangia katika maendeleo ya nchi na jamii kwa ujumla.

Pamoja na kulitambua hilo afisa mtendaji huyo amekuwa akiwalazimisha watumishi kwa kutumia mamlaka aliyonayo kulipa mchango ambao yeye mwenyewe hajazungumza na watumishi wa kata hiyo kuwaeleza lengo la mchango huo.

Watumishi kata ya Lulembela tunalaani kitendo kilichofanywa na afisa mtendaji huyu kuwafikikisha watumishi mahakamani kwa jambo ambalo angeweza kuwaeleza na kuwaelimisha kwanza kabla ya kuchukua hatua hiyo.

Watumishi kata ya Lulembela tunaviomba vyama vya wafanyakazi ikiwemo CWT na TUGHE kulifuatilia suala hili kwani linadhalilisha walimu na wataalamu wa afya kwenye kata hiyo.

Aidha ifahamike kuwa sisi watumishi tuko tayari kuchangia maendeleo kwa jamii yetu lakini kwa kueleweshwa na kuelimishwa kuhusu mchango husika na si kulazimishwa kama anavyofanya huyu afisa mtendaji.
 
Kuna tatizo mahali, kabla ya kuwa peleka mahakamani ilitakiwa kuwafikisha kwa muajiri wao ambae ni mkurugenzi wa halmashauri.
 
Hii imefeli sana ipo siku mwenyekiti wa mtaa atakuja na mchango wa kushona suti na wasiotekeleza kutiwa ndani
 
Back
Top Bottom