Afisa Mtendaji aliyebaka mwanafunzi KIMARA afikishwa kizimbani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afisa Mtendaji aliyebaka mwanafunzi KIMARA afikishwa kizimbani

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pdidy, Apr 18, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,416
  Likes Received: 5,687
  Trophy Points: 280
  JAMANI HAWA AWANAOBAKA WAMSHINDWA HATA NAULI YA KUWAFIKISHA JOLI AMA CORNER BAR


  Afisa Mtendaji aliyebaka mwanafunzi afikishwa kizimbani


  Saturday, April 18, 2009 10:02 AM
  AFISA MTENDAJI aliyedaiwa kubaka mwanafunzi msichana mwenye umri wa miaka 16 wa darasa la saba maeneo ya Kimara amefikishwa katika Mahakama ya Mkazi Kinondoni jana.
  Afisa Mtendaji huyo ni wa Kata ya Kwembe ya jijini Dar es Salaam aliyetambulika kwa jina la Dandas Kijo [28] ambaye ni mkazi wa Kwembe.

  Afisa huyo alifikishwa mapema jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu tuhuma zinazomkabili za kushirikiana kimapenzi na msichana huyo bila ridhaa.

  Alifikishwa katika Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Suzan Makabwa na kusomewa mashitaka yanayomkabili na Mwendesha Mashitaka, Nassoro Sisiwaya.

  Sisiwaya alidai kuwa, Machi 27, mwaka huu, mshitakiwa kwa makusudi kabisa alimbaka msichana huyo ambaye jina lake limehifadhiwa na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri.

  Alipotakiwa kujibu shtaka lake hilo linalomkabili na Hakimu alijibu kuwa si kweli hajafanya kitendo hicho.

  Hakimu alijaribu kumuuliza “unahabari kuwa binti huyo ameshafanyiwa uchunguzi wa kina na imegundulika kuwa amebakwa na alipobanwa alikutaja wewe”.

  Alijibu kuwa si kweli hawezi kufanya kitendo hicho na mwanafunzi wa shule kwa kuwa anaelewa sheria.

  Hakimu alimwambia haina haja ya kutoa maelezo mengi ipo siku ya kutoa maelezo hayo pindi kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.

  Hivyo kesi hiyo iliahirishwa hadi hapo Mei 4, mwaka huu, itakapotajwa tena Mahakamani hapo.

  Kabla ya kufikishwa Mahakamani kwa Afisa huyo ilidaiwa kuwa alitoa rushwa kwa familia ya msichana huyo ili kesi hiyo isiweze kufika mbele.

  Pia mama wa msichana huyo alipohojiwa alikubali kuwa kweli na aliamua kumsamehe Afisa huyo kwa kuwa alikuwa ni jirani yake wa karibu.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni alipotakiwa kujibu tuhuma hizo alidai hazikumfikia lakini aliahidi uchunguzi wa kina utafanyika na endapo itagundulika ni kweli atafikishwa Mahakamani.

  Uchunguzi ulifanyika na kupatikana na hatia na jana alifikishwa kizimbani.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  maskini wanafunzi ..tena ukute baba mzima ana VVU na hata kinga hajatumia!
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Charge nyingine bwana!
  Kuna kubaka kwa kukusudia na kubaka bila kukusudia? How would that be framed in English?
   
Loading...