Afisa msaidizi wa Forodha TRA, Jennifer Mushi afikishwa Mahakamani kwa kumiliki magari 19 na kuishi maisha ya kifahari

Ukiwa public servant unasaini ile form ya madili unaandika Mali zako na kipato..Na jinsi ulivyozipata
Labda walichunguza form wakaona haziendani.
Halafu sheria sio siasa kwamba kosa LA mwingine linahalalisha lako!!.
Ndo maana utaona wakili wa huyo mtuhumiwa hatatumia hiyo hoja ya Huyo unayemwita Bashite katika utetezi wake
 
Yani hayo magari yote hakuna lenye thamani ya 20m, awamu hii inavyoelekea hata ukiwa unapiga sana pamba itakua ni kosa!
 
Mtajuaje vyanzo vyake vingine vya mapato, sikuizi watu wanabeti mpira, wanacheza biko, tatu mzuka, vilevile yeye kama mwanamke anaweza kupewa na bwanaake. Mbona tunaona dagaa wanasumbuliwa lakini papa wametulia tu?
[HASHTAG]#justice[/HASHTAG]
 
SIONI CHA KUNIUMIZA KICHWA HAPA,TULIAMBIWA KUWA WALIO NACHO WANATAKIWA KUISHI KAMA MASHETANI.HAYO NDIO MAENDELEO TULIO PIGIA KURA.
 
Afisa Msaidizi wa Forodha wa TRA Jennifer Mushi kafikishwa Mahakamani, anadaiwa kumiliki mali, kuishi kifahari kinyume na mshahara wake

-----
AFISA MSAIDIZI WA FORODHA ALIYEISHI KIFAHARI, KAFIKISHWA MAHAKAMANI.

Afisa msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kumiliki mali ambayo ni magari 19 na kuishi maisha ya kifahari kinyume na mshahara wake.

Mshtakiwa alisomewa makosa yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi na Wakili wa Serikali, Vitalis Peter ambaye alidai mshtakiwa ana makosa mawili.

Alidai kuwa kati ya March 21, 2016 na June 30, 2016 katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam, akiwa mwajiriwa wa TRA, kama Afisa Msaidizi wa Forodha alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake, kinyume na sheria.

Inadaiwa alikutwa akimiliki magari 19 ambayo ni Toyota RAV4, Toyota Dyna Truck, Toyota Vitz, Suzuki Carry,Toyota Ipsum, Toyota Wish,Toyota Mark ll, Toyota Regiusage, Toyota Estima, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota Crown, Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Lasso, Suzuki Carry, ambayo yana thamani ya Tsh. Milioni 197.6.

Kosa la pili, anadaiwa kuwa kati ya March 21, 2012 na March 30, 2016 jijini Dar es Salaam akiwa mwajiri wa TRA aliishi maisha ya kipato cha juu tofauti na kipato chake yenye thamani ya Tsh. 333,255,556.24 tofauti na kipato chake.

Wakili Peter amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, hivyo anaomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali (PH).

Hata hivyo, upande wa utetezi kupitia Wakili Elisalia Mosha aliiomba Mahakama hiyo kumpa dhamana mteja wake kwa sababu mashtaka aliyonayo yanadhanika kisheria.

Hakimu Shaidi alimtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Tsh. Milioni 20 ambapo alikidhi masharti na kuachiwa kwa dhamana.

Kesi imeahirishwa hadi November 7, 2017.

Kuwa masikini ni sifa na Heshima kwa Tanzania???
Kuishi Maisha mazuri ni kosa

Wenye mali zisizolingana na kipato ni wengi ajabu. Sijui ni kigezo gani kimetumika kuanza na huyu.
 
Itafika wakati nyie wenye vitambi mkigundulika itakuwa ni kosa kubwa!

Ova
 
Kama wengi tunavojua kesi inayo mkabili afisa forodha wa TRA.Mimi binafsi naona hii kesi ni ya kipuuzi.Eti mali zake haziendani na kipato chake.Mbona Bashite anamiliki X6,Lexus, na Ford Ranger ya $60000 alafu haguswi.Hizi double standards serikalini zitaisha lini jamani.Nakulilia Tanzania
Sidhani kama ni kosa kama una chanzo kngne cha kuingiza kipato tofauti na mshahara
 
Huu ni ujinga unaofanywa na TRA, yaani inaonekana serikali haitaki watu wawe matajiri, inahimiza umasikini
TRA wanaona ni bora hella ulioipata ununulie chakula kuliko kujenga
Tatizo wajinga wengi wamejazana mule

Na serikali isipoangalia hilli kutakuwa na vifo vya biashara nyingi badara ya kusaidia na kuimiza maendeleo
Wanafikiria mwezi huu mapato yaongezeke lkn hawafikirii miaka ijayo
 
huyo dada ana umri gani?? kama yupo tra zaidi ya miaka 10 hizo mali ni halali kwake hata kwa savings tu na vibiashara vidogo vidogo.
 
Nadhani anatakiwa athibitishe tu kuwa ana vyanzo vingine vya mapato tofauti na mshahara wa serikali,full stop
 
Ukiwa public servant unasaini ile form ya madili unaandika Mali zako na kipato..Na jinsi ulivyozipata
Labda walichunguza form wakaona haziendani.
Halafu sheria sio siasa kwamba kosa LA mwingine linahalalisha lako!!.
Ndo maana utaona wakili wa huyo mtuhumiwa hatatumia hiyo hoja ya Huyo unayemwita Bashite katika utetezi wake
Siyo puplic servant wote wanasaini fomu ya kuonyesha mali zao. Ni viongozi tu yaani kuanzia mameneja na wakurugenzi nakuendelea. Ila TRA wao wamejitungia tu sheria yao ambayo inamtaka kila mtumishi kuonyesha mali yake bila kujali cheo au nafasi yake.
Kesi hamna hapo kwani sheria mama(katiba) haimwekei kikomo raia kumiliki mali cha msingi asikutwe na ushahidi wa uhujumu uchumi au ufisadi.
 
Hii ni moja ya kesi ambayo binafsi naiona serikali ikishindwa asubuhi na mapema. ngoja tuone mwisho wake.
 
Back
Top Bottom