Mike Msimba
New Member
- May 6, 2017
- 2
- 1
Habari wana jf?
Nina mdogo wangu anayesoma mwaka wa tatu katika chuo hiki ambaye yeye pamoja na wenzake zaidi ya 30 wa mwaka huo walizuiliwa kufanya test kwa sababu ya kupungukiwa ada kwa mitihani iliyopangwa kufanyika tarehe 2/05/2017 mpaka 9/05/2017. Wakati anazuiliwa nilikua nje ya mji na sim yangu haikuweza kupatikana kutokana na mtandao kua chini hivyo ikapelekea kushindwa kulipa pesa hiyo kwa wakati ili kijana afanye mtihani.
Nimesikitika zaidi pale ambapo amri ya kuzuia wanafunzi inatolewa na Afisa wa Mitihani kwa jina la Marco Musimba badala ya Kaimu Mkurugenzi wa chuo. Nilipofuatilia zaidi, ikaelezwa kwamba huyu Afisa Mitihani ana kawaida ya kwenda kumshitakia mkuu wa chuo kwenye vikao vya bodi kwamba chuo kinaruhusu wanafunzi wasiomaliza ada kufanya mitihani na hivyo kusababisha Kaimu Mkurugenzi huyo wa chuo kuwa muoga kuruhusu wale waliokwama kulipa kwa wakati.
Lakini maelezo yalienda mbali zaidi na kudai kwamba Afisa Mitihani huyo anapozuia wanafunzi hupendelea kutoa kauli kwamba wazazi wa wanafunzi hawawajibiki kwa kutojinyima ili kulipa ada na kwamba yeye analipia watoto wake pesa nyingi hivyo wazazi wenye watoto chuoni hapo lazima walipe, akaenda mbali zaidi na kudai kwamba baadhi ya wanafunzi wana vyanzo tofauti vya kupata pesa hivyo anashangaa kwanini hawalipi na sasa dawa yao ni kuwazuia mitihani.
Kwa upande wangu naona hili halijakaa sawa kwa kuzingatia kuwa hakuna anayetaka kusoma bure kama Afisa Mitihani huyo anavyojaribu kumaanisha, hali ni ngumu sana na hivyo yeye ndio angefaa kuwa mshauri juu ya suala hili ambapo Serikali kupitia Bunge la bajeti la mwaka 2013/2014 iliagiza kwamba wanavyuo wasifukuzwe kwenye mitihani isipokua matokeo yao ndio yazuiliwe.
Kitendo cha Afsa mitihani huyu kuwa na nguvu zaidi ya Mkurugenzi wake na pia Mkurugenzi kuzidiwa nguvu na Afisa wake kinaonesha kutokuwa na uelewa wa mipaka ya majukumu kwa wawili hawa, hivyo ingefaa wakapata msaada wa kuelekezwa mipaka ya majukumu yao na wakishindwa basi hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.
Wasalaam