Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale asimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha za ujenzi wa Hospitali

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Bw.Omary Chingwile ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Liwale na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo.

"Hatuwezi kufanya mchezo na fedha ya Serikali, tunahitaji kila mradi uende vizuri, fedha iliyoletwa lazima itumike kama ilivyokusudiwa".

Mhe.Majaliwa amesema Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza matumizi mazuri ya fedha za umma ili zikamilishe miradi ya maendeleo ya wananchi na kwamba Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote anayetumia vibaya fedha za umma.

Waziri Mkuu amemsimamisha kazi mtumishi huyo wakati akizungumza na madiwani, watumishi na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Lindi.

ITV
 
Mbuzi

Mbuzi wakafara huyo,

Hapo mlolongo wa upigaji unaanzia Tamisemi
 
Ambao hatuna uelewa tunapata shda kuelewa afisa mipango anapewa vp fedha za ujenz, wakat mkandarasi analipwa na mhasibu/mweka hazina..wenye uelewa msaada tafadhalin
 
Siasa za majitaka. Afisa mipango huwa anashika hela?
Miradi kama hiyo kuna TAMISEMI, mkurugenzi wa wilaya, mhasibu wa wilaya, DSO, DC, DAS. Afisa mipango hapo kauziwa kesi bure.
 
Kazi za ujenzi ni technical work na Afisa Mipango wala hana uhusika wa moja kwa moja. Hata kuidhinisha Certificate hahusiki. Masimamizi Mkuu wa kazi hiyo ni Mhandisi wa Ujenzi. Ndiye anayethibitisha kama kazi imefanyika kwa kiwango gani na kinastahili malipo ya kiasi gani.
Afisa Mipango mipango wala haanzishi dokezo hau hati ya madai. Afisa Mipango ni mtia saini tu wakati wa malipo.

Hivyo hapo hamna kesi. Sana sana amesumbuliwa tu na anakuja kuhamishwa kituo cha kazi.
 
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Bw.Omary Chingwile ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Liwale na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo.

"Hatuwezi kufanya mchezo na fedha ya Serikali, tunahitaji kila mradi uende vizuri, fedha iliyoletwa lazima itumike kama ilivyokusudiwa".

Mhe.Majaliwa amesema Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza matumizi mazuri ya fedha za umma ili zikamilishe miradi ya maendeleo ya wananchi na kwamba Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote anayetumia vibaya fedha za umma.

Waziri Mkuu amemsimamisha kazi mtumishi huyo wakati akizungumza na madiwani, watumishi na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Lindi.

ITV
Hii inati moyo. Niliwahi kuandika humu kuwa Liwale ni miongoni mwa wilaya zilizosahaulika kutembelewa na viongozi wa juu wa kitaifa.

Sijawahi kufanya kazi H/w ila mawizarani na taasisi za Umma PMU kazi yao ni fund realocation kutokana na ACTION PLAN ya ofisi husika yaani kama OC ikiingia kazi yao ni kugawanya fedha kulingana na mpango mkakati by VOTES.

Akishagawanya kila idara inatumia fedha kulingana na mahitaji wao kama vipaombele vyake vinavyoelekeza. Sijui huyu wa Liwale kahusikaje tuwaachie wachunguzi.
 
Ile serikali ilikuwa na watu waongo sana
Hata sasa ni hihii serikali inayotengeneza matatizo kisha inayatafutia ufumbuzi kwa lengo la kutudanganya wananchi kuwa wapo vizuri ktk utendaji kazi.
Ni waongo wakubwa

Mungu atuondolee hii serikali mbovu
 
Namkumbuka Hawa Ghasia enzi hizo.
Watu wakisema zama zile zimerudi wanaitwa sukuma gang, tuweke ligi basi kati ya sukuma gang na Msoga gang tuone nani zaidi...
 
Back
Top Bottom