Afisa Masuuli ndiye nani?

Al Zagawi

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
2,461
1,447
wakuu..nimesikia hili neno leo wakati nikiangalia taarifa ya habari ya TBC1...liliwekwa tangazo moja kutoka ofisi ya CAG likiwataka maafisa masuuli kuwasilisha financial statements za taasisi zao tayari kwa ukaguzi.

sijawahi kabla kusikia hili neno na ilivyo TBC na tabia yao ya misamiati ya ajabu..si mnakumbuka ule wa habari zilizovunjika basi ikanibidi nifike hapa kuwauliza mabingwa wa lugha..ni nini maana ya afisa masuuli?
 
Accounting Officers! Yaani Watendaji wakuu. kama Makatibu wakuu wa Wizara, CEOs wa Public bodies nk
 
mh! haijaniingia akilini
pengine yule aliyesema afisa wa majukumu kidogo inafanana
Afisa Masuuli ni afisa mwenye mamlaka ya juu na wajibu wa kusimamia na kutoa taarifa kuhusu matumizi ya fedha zilizotolewa kwa taasisi yake kutoka serikaini. Kwa kiingereza wanaitwa Accounting Officers. Hili jina halimaanishi kuwa ni wahasibu, hapana. Linamaanisha kwamba wao ndiyo wawajibikaji wakuu katika taasisi- accountable.
 
uko sawasawa
 
Haswa.., hawa ndio wanaowajibika na ile taarifa ya kaguzi inayopelekwa kwa CAG. Kwa mfano mawizarani, maofisa masuhuli ni makatibu wakuu na sio mawaziri. Wengi wanafikiri mawaziri ndio mabosi kule mawizarani, kumbe wao ni mabosi kisiasa tuu, the really powers ziko kwa ma KM, ambapo waziri lazima ampigie goti kujipatia fungu la ziada.

Hata katika marejesho ya masurufu na maduhuli, ni afisa masuhuli ndio yuko accountable kwa CAG kuhusu matumizi mabaya ya masurufu na maduhuli.
 
Back
Top Bottom