Afisa Madini wa mkoa wa Tabora, aagizwa kutoa leseni za uchimbaji wa madini ya dhahabu

rose mzalendo

Member
Mar 5, 2019
71
114
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amemuagiza Afisa Madini wa mkoa wa Tabora kutoa leseni za uchimbaji wa madini ya dhahabu katika mgodi wa zamani wa Resolute ulioko wilayani Nzega mkoani Tabora ambalo kwa sasa ni chuo cha madini.

Ameyasema hayo katika kitongoji cha Mkwajuni kata ya Lusu wilayani Nzega alipokutana na baadhi ya wachimbaji wa dogo ambao wamemueleza shauku yao ya kupatiwa leseni ili waweze kuendesha shuguli ya uchimbaji kihalali.

Nyongo amesema kupatiwa leseni kwa wachimbaji hao itawezesha wananchi kupata kipato na serikali kwa ujumla kuliko kuendelea kuachia uchimbaji haramu unao endelea kufanyika eneo hilo.

"Ofisi ya Afisa madini inatakiwa itangaze tenda ya kuuza mabaki ya mchanga wa Dhahabu yaliyoko katika eneo hili, ili libaki salama kwasababu vibaka wamekuwa wakivamia eneo hili hivyo ni vyema kutoa leseni" amesema Nyongo

Said Mgalula ambaye ni mmoja wa wachimbaji wadogo wanaotoka katika kata hiyo amesema endapo leseni hizo zitatolewa itawasaidia kuchimba pasipo buguza yeyote.

" Uchimbaji haramu bado unaendelea katika eneo hili na dhahabu zimekuwa zikichimbwa na kutoroshwa na watu wanao ruhusiwa kuchimba eneo hili ndio wanaowapatia walinzi fedha"
 
Mkuu Naomba kujuzwa ni vigezo gani na Taratibu vyatakiwa ili kupata hiyo Leseni,pia gharama zake ni kiasi gn?.Nina sehemu tumeshafanyia utafiti kidogo tumeweza kupata ghahabu ipo ya kutosha sasa kabla ya wajanja hawaja stuka nataka nipahodhi nianze kupafanyia kazi
 
Majibu yalikuwa magumu jamaa kaukimbia uzi
 
Back
Top Bottom