NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 8,520
- 17,426
Wanabodi habari za asubuhi,
Leo naleta malalamiko ya baadhi ya wakuu wa shule za sekondari wilaya uyui! kumhusu Jakobo Makala huyu kama Afisa elimu wa Uyui!
Malalamiko makubwa yanatoka kwa Aliekuwa Mkuu wa shule Loya sekondari Ndugu Joseph Nduba! Huyu ndiye alisimamia ujenzi wa sekondari ya loya mwaka 2007 na kuifungua mwaka huo huo. Baada ya kuhudumu kwenye cheo hicho hadi mwaka 2011 Mzee aliwekwa pembeni na kupewa Ndugu Khalifa Khamisi hadi leo.
Huyu mzee amekuwa mwalimu wa kawaida tangu kipindi hicho hadi sasa. Japo aligoma kumkabidhi shule ndugu Khalifa na kusababisha mgogoro wa uongozi ambao unafukuta hadi leo kimya kimya. Ndugu Makala ondoa kero iliopo kwa kuwaondoa wote na kumleta Mkuu mwingine kwa sababu wote hawana sifa za kuwa wakuu wa shule kwa vigezo vya sasa.
Wote wana stashahada na sio shahada au degree kwa mujibu wa viwango vya sasa vya TAMISEMI. Acha kufunika kombe mwanaharamu apite tatua tatizo sio kulifunika. Mbona shule nyingine mmewatoa wakuu wenye diploma hapo loya mnasubiri nini?
Hamuoni mnamdhalilisha huyu mzee kwa kumfanya mwalimu wa kawaida wakati yeye ndio alioifungua shule? Mna maslahi gani hasa binafsi na kubakiza Wakuu wa shule ambao hawana vigezo vya kielimu? Je, ni rushwa maarufu kama fungu la kumi hapo Halmashauri ya Uyui?
Acheni kudhalilisha taaluma za watu! wengine mmewafedhehesha kwa kuwatoa kuwa hawana sifa kielimu halafu wengine wawili mmewakumbatia!
Badilikeni tatueni hili jipu kabla Wakuu wa shule mliowatoa kwa kukosa sifa hawajaenda mahakamani kufungua shauri.
Nimatumaini yangu kuwa sinto fahamu hii mtaitatua.
nikutakie kila heri kwenye majukumu yako ya kila siku.