Afisa elimu msingi wilaya ya Siha ni tatizo la kudumu

Kibogoyio2020

Senior Member
May 4, 2018
154
77
Sisi walimu Wa halmashauri ya wilaya ya siha tumechoshwa na vitendo anavyotufanyia afiselimu msingi Wa wilaya yetu.kila Mara ili ufanye kazi maalum au kuhama kituo lazima utoe kituo kidogo.hii imekuwa ni tabia yake miaka yote.posho tunayopewa ya uogozi lazima kila mwezi umatie kidogo vinginevyo cheo hicho atakuondoa na kukupangia au kukuhamisha kituo. Kila tukilalamika anasema nenda unakojua hatafanyiwa kituo.tunaomba sasa serikali itusaidie ili tuweze kukuza elimu kwenye wilaya yetu na asitukatishe tamaa ya kazi ya ualimu.ili tukuze ufaulu kwani kila kipindi tunakuwa karibia Wa mwisho kiwilaya kwa ngazi ya kimkoa.
Amekuwa akifanya kazi kwa mazoea na hana jipya LA kusadie kukua kwa elimu kwa wilaya yetu.
Anaishi KMs 30 nje ya kituo cha kazi hivyo kutembelea shule zetu aatumia remote management na hakuna ufaulu wala motisha wowote ketu sisi walimu
 
Poleni sana waalimu..
Nyie ndo mnatoa elimu lkn ni kati ya kundi linalodharauliwa na kukandamizwa..kimsingi huyu Anapaswa kutumbuliwa..

pole sana mwalimu.
 
Haya umesikika ila post yako ingeambatana na ushahidi mfano sms za kumtigopesa au conversation za sms anazodemand mkwanja na kadhalika.All in all poleni na changamoto za kiuongozi mnazopitia
 
Sector ya elimu ni nyeti sana na inapaswa iwe na sehemu ya malalamiko hasa kwa walimu husika na malalamiko yanatakiwa kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo kwani sector ya elimu ni sector inayoendeshwa kwa heshima, ueledi na nidhamu,

Sasa kama mtu mmoja asiye na nidhamu wala maadili ya elimu anapokuja na kuweka maslahi yake kwanza tena kwakukosa nidhani na ueledi kwa walimu ambao ndio watendaji wakuu na bado mtu huyo huyo hachukuliwi hatu za kinidhamu kuokoa elimu nchini, na tena kwakujitamba kana kwamba sector ya elimu ni mali yake , hii haifai kabisa

Wahusika mnao deal na mambo haya msikae kimya juu jambo hili kwani taifa litaharibika kwa ajili ya mtu mmoja , hivyo shuhulikieni malalamiko ya walimu wote mapema
 
Mwalimu mkuu acha kulialiaa Piga kazi bhana!Si umependa ma vyeo mwenyewe ndo upambane sasa na hali yako!km hutaki izo shurba usipende kushobokea ma vyeo ni vitu za kupita tu
 
Acheni kusema mambo bila kuwa na ushahidi. Nadhani waliotoa taarifa hizo za upotoshaji wanalengo la kuwakatisha walimu tamaa
 
Naomba muache majungu kazini
Ila mtoa taarifa anazo sababu zake binafsi tena amekata tamaa ya maisha na kiukweli nahisi siyo mwalimu wa Wilaya ya Siha
 
Afisa elimu Siha Usijali hao ni mashetani wachache ambao wamepanga kukukatisha tamaa katika kazi yako.
Tunatoa ushauri kuwa malengo ya maadui hayatatimia kamwe.
NB. Wameona unafanya kz kwa ustadi wanaanza kukuchafua, tutawatafuta hao wanaotaka kupata cheo kwa kuchafua wengine
 
Hapo hakuna Kitu umepost bali ni ukosefu wa majukumu na tamaa ya madaraka tu.
Madaraka hutapata kwa kuchafua wengine.
Nashauri wekeni mambo yatakayoleta maendeleo badala ya majungu
 
poleni sana waalimu wilayani siha....nadhan nae ana mkuu wake au ndio lao moja,,,,fanya tu kufikisha kwa wakubwa zake
 
Hakuna cha pole hapa kilichotokea ni mtu mmoja kujifanya anatoa Shutuma za uongo tena kwa maslahi binafsi.
Tutazidi kufuatilia na tunaomba atoe ushahidi wake Kama anao
 
Afisa elimu Siha Usijali hao ni mashetani wachache ambao wamepanga kukukatisha tamaa katika kazi yako.
Tunatoa ushauri kuwa malengo ya maadui hayatatimia kamwe.
NB. Wameona unafanya kz kwa ustadi wanaanza kukuchafua, tutawatafuta hao wanaotaka kupata cheo kwa kuchafua wengine
Anasifiwa kwa lipi ili kuonyesha jitihada za kuikwamua wilaya siha kielimu? Shida inaanzia pale kiongozi tena Wa elimu anavyonunua madaraka ili aweze kututawala.akiwa wilaya ya hai aliwafanya walimu wakakata tamaa ya kufundisha akiwa mtaaluma Wa wilaya. Kwa kuwakatisha walimu tamaa akapandishwa cheo kuwa afisaelimu wilaya yetu.amewafamya baadhi ya waratibu elimu wetu kubwa frustrated na wameshindwa kusimamia elimu vemashule zingine zina walimu watano na ukifuatilia anakujibu yeye sio Waziri Wa elimu. Likizo walimu hawalipwi stahili zao kwa wakati,kituo cha walimu walimu havijui na hstuoni vina ulekeo gani kusadia elimu. Shule za kusaidia KKK alisahau na hajui ziko wapi na zinafanya nini.kwa ujumla tunashauri ili apate utamu Wa cheo chake aungane na walimu kusaidia kufundisha ili aweze wa mfano badala ya sasa kusubiri matokeo ya darasa LA saba na tunakuwa Wa mwisho.
 
Kama kuna mtu anachuki binafsi hapo Sawa lakini kiutendaji ofisa elimu wetu yupo sawa
Kama Ww ulitaka kupewa cheo hicho bc utakaa sanaaaa
n'a pôle kwa usumbufu
 
Suala la shule kuwa na walimu wachache hilo lipo nje ya uwezo wake n'a halina uhusiano n'a hoja iliyotajwa hapo juu
 
Suala la shule kuwa na walimu wachache hilo lipo nje ya uwezo wake n'a halina uhusiano n'a hoja iliyotajwa hapo juu
Wewe utakuwa chama cha walimu.sisi tulioko shule ndio tunaloliona.wewe tena sio mwalimu unatetea usilolijua tuulize sisi tulihamishiwa kufundisha wilaya ya siha tukitokea wilaya ya hai.habsri ya cheo sio deal kwa sasa.hapa kazi tu.
 
Kupuuza taarifa za upotoshaji:
Ndugu wananchi hapa duniani hata shetani anao malaika pia watu Kama hawa wapo tu kwa ajili y'a malalamiko n'a hawajui kufanya kazi.
Naomba tuwapuuze kwani hawana hata ushahidi wa kueleza umma badala yake wanaleta mambo y'a porojo tu, Naomba Kama kuna mtu anahoja ya maana alete tujadili Hapa hakuna kitu
 
Kwa taarifa tu Ofisi ya mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Siha haijawahi kupata malalamiko y'a mwalimu yeyote Siha kuwa ameonewa kwa jambo lolote bali pongezi n'a sifa kemu kemu zinatolewa kila siku.
Acha chuki binafsi Ww utahangaika kuchafua watu lakini hautapata manufaa yoyote bali utaishia kulalamika tu.
 
Mbona sijaona mwalimu anayekuunga mkono hoja yako ?
Acha chuki binafsi Kama ulihamishwa ni kwa Mujibu wa sheria na taratibu. Usihamishwe Ww nani kwani.
Walimu wote Siha wanakushangaa kwa Shutuma zako ambazo hazina ukweli wowote.
 
Mbona sijaona mwalimu anayekuunga mkono hoja yako ?
Acha chuki binafsi Kama ulihamishwa ni kwa Mujibu wa sheria na taratibu. Usihamishwe Ww nani kwani.
Walimu wote Siha wanakushangaa kwa Shutuma zako ambazo hazina ukweli wowote.
Wewe unamtetea tafuta historia yake ulinganishe na historia yako jibu lake angalia ufaulu Wa wilaya yetu. Mtaaluma wake kila siku anatutukana sisi walimu tena akiwa anaona na hajui atusaidieje. Mimi sitaki cheo Niko kusimamia ukweli
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom