Afisa Elimu msingi Tandahimba amewahamisha walimu bila kuwalipa stahiki zao

Shimoyo

Member
Feb 10, 2021
11
7
Ni mwanamama asiyezingatia wala kuheshimu sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi. Wiki iliyopita amewapatia barua za uhamisho walimu zaidi ya 30 wakihamishwa toka vituo vyao vya zamani kwenda vituo vipya vya kazi. Kati yao hakuna aliyelipwa stahiki zake zikiwemo posho ya usumbufu au ile ya kujikimu.

Walimu hawa wanaletewa lori la polisi na kulazimishwa kupakia mizigo yao bila kupewa maelezo ya kina kuhusu stahiki zao zinazotokana na uhamisho huo. Wanaopeleka barua za madai ofisini kwake huwaambia kwamba pesa hazipo na huwataka wakasajili madai yao kwenye mfumo wa MADENImis ambao unahusu madeni ya watumishi wizara ya TAMISEMI.

Nakumbuka Mara nyingi Rais Magufuli amenukuliwa akiwasisitiza waliokasimishwa mamlaka ya uajiri katika wizara na idara za serikali kuhakikisha kwamba hawamhamishi mtumishi yeyote pasi kumlipa stahiki zake. Huyu mama ameamua kupuuza maagizo ya mheshimiwa Rais kwa kuhamisha walimu bila kuwapatia posho zao.

Mwaka jana Afisa Elimu huyu amewadhulumu walimu wakuu na walimu wa takwimu pesa ambazo hutolewa na program ya EP4R kama motisha kwa ajili ya zoezi la uchakataji wa takwimu mbalimbali za kielimu kwa shule za msingi. Mwanzoni aliwaahidi walimu hao kwamba kama watajituma kuchakata takwimu sahihi na kwa wakati wangepatiwa pesa hizo ambazo hutolewa na TAMISEMI kama motisha ya wote wanaohusika kuandaa takwimu na kuzituma wizarani.

Walimu walijituma na zoezi lilifanikiwa kwa zaidi ya 95% lakini pesa zilipoletwa toka wizarani si mwalimu mkuu wala mtakwimu aliambulia japo senti tano. Fedha zote alizitumia kwa matumizi yake binafsi. Wakati walimu wa msingi wakiambulia patupu, wale wa sekondari angalau walipata kifuta jasho kwa wakuu wa shule na ma-Afisa Elimu kata kulipwa shilingi 30000 kila mmoja na walimu wa takwimu walilipwa 60000 kila mmoja.

Mheshimiwa Jafo tafadhali tuma maafisa toka wizarani kwako wamchunguze huyu mama. Anaihujumu serikali ya Rais Magufuli bila ya wasiwasi wowote. Hata maendeleo ya taaluma hapa wilayani si ya kuridhisha kwa miaka kadhaa kwani walimu wamekosa morari ya kufanya kazi kutokana na matendo wanayotendewa na Afisa Elimu wao.
 
Tamisema imekosa usimamizi mzuri, huko Tandahimba hata mkurugenzi ( DED) analalamikiwa Sana lakini sijawahi kuona hatua zikichukuliwa. Madudu mwanzo mwisho. Kutwa kuchangishana mamichango yasiyokuwa na maana.
 
Back
Top Bottom