Afisa Elimu mkoa wa Mbeya njia unayotumia kukusanya fedha kwa Wakuu wa haikubaliki na ni uwizi

KBG SCORPION

Member
Feb 25, 2022
23
21
Habari wanajukwaa,

Naomba niingie Moja Kwa moja kwenye mada.Tabia na mazoea ya afisa Elimu tajwa hapo juu haikubaliki ambapo afisa huyo pasi na aibu Wala hofu huagiza kila mkuu Wa shule kupeleka fedha kwake.

Mwezi huu kila mkuu Wa shule ya serikali katika wilaya ya Mbarali kaagizwa kupeleka Tshs.100,000/= .Madai ya fedha hizo Kwa wakuu Wa shule hayana barua isipokuwa anachokifanya ni kuwaagiza wenyeviti Wa wakuu Wa shule ngazi ya wilaya Kwa njia ya magrupu ya "Whatsapp".

Kama fedha au michango hii ya wakuu Wa shule kwenda kwake ni halali Kwa nin Haina barua inayotoa maagizo hayo?

Kwa vile fedha hiyo humfikia Kwa njia isiyo halali,je matumizi yake yatakuwa halali?

Tunaomba wahusika Kwa maana ya wateule wake na vyombo vya dola kuchukua hatua.Wakuu Wa shule hawafanyi majukumu Yao Kwa amani maana nafasi zao za madaraka zipo rehani.

Muwe na Dominika njema!
 
Asante kwa taarifa, nalifanyia kazi muda huu hadi juma tatu hicho kiti kitajua wazi

Amini nikuambiacho
 
Milungula kutoka mashuleni (msingi/sekondari) kwenda ngazi za juu ni utamaruni wa siku nyingi sana Bongo. Vyeo vya wakuu wa shule, walimu wakuu ,maafisa elimu kata na maafisa elimu wilaya vinalindwa kwa njia hii.

Wote wanaoteuiwa katika nafasi hizi hujua kabisa kuwa ni wajibu wao, hata kama ni haramu. Tabia hii ya kuchukua milungula kutoka kwa watu wa chini imefanya nafasi nyingi za uteuzi ktk kada ya elimu kushikwa na watu wasiokuwa na sifa za uongozi bali ambao ni wepesi kutoa mlungula.

Na tabia hii haipo mbeya tu Bali ni nchi nzima.
 
Back
Top Bottom