Afisa elimu ashtakiwa wizi fedha za madawati

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Imeelezwa kuwa fedha hizo zilichangwa kwa ajili ya kununua madawati.

Akizungumza na Nipashe, Mkuu wa Takukuru mkoani hapa, Sosthenes Kibwengo, alisema Ndabazi alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma na alitenda kosa hilo akiwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mpwayungu Wilaya ya Chamwino kinyume cha kifungu 273(b) cha Sheria ya Kanuni za Adhabu sura ya 16 marejeo ya 2002.

Kibwengo alisema ofisa huyo anatuhumiwa kuiba kiasi cha Sh. 24,334,920, Aprili, mwaka 2016, wakati akiwa shuleni hapo."Katika uchunguzi wa Takukuru umeonyesha akiwa mjumbe wa kamati ya madawati, Ndabazi alijipatia kwa njia ya udanganyifu fedha hizo zilizochangwa na wananchi na wahisani kwa ajili ya kununua madawati ya shule za Wilaya ya Chamwino zikiwa ni sehemu ya michango ya zaidi ya Sh. milioni 85," alisema.

Alieleza kuwa kesi hiyo namba 9 ya mwaka 2020 ilisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Pascal Mayumba na mshtakiwa huyo ameachiwa kwa dhamana hadi Februari 21, mwaka huu.

MWINGINE ASIMAMISHWA

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita limemsimamisha kazi Ofisa Elimu Msingi wa halmashauri hiyo, Said Matiku, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma anazotuhumiwa ikiwamo kulalamikiwa kuwa mazingira ya uhamisho na upandishwaji vyeo walimu kudaiwa kugubikwa na utata.

Hatua hiyo ilifikiwa katika kikao cha madiwani baada ya kukaa kama kamati kwa mujibu wa sheria na mamlaka ya Baraza la Madiwani pale linapotaka kumjadili mtumishi, ambapo hulazimika kujigeuza kama kamati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Ali Kidwaka, alithibitisha kutolewa uamuzi huo na kwamba ulifikiwa katika kikao chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Elisha Lupuga, ambaye ndiye anayeweza kulitolea ufafanuzi zaidi suala hilo kwa kina.

Lupuga akithibitisha kuchukuliwa kwa hatua hiyo na kwamba taratibu za kuchukuliwa hatua hiyo zilizingatia kanuni na sheria katika kikao kilichofanyika Januari 6, mwaka huu.

Lupuga amesema baada ya kufikiwa uamuzi huo baraza lilimwagiza Mkurugenzi Kidwaka kumsimamisha kazi Matiku na pia kuunda kamati itakayochunguza tuhuma zinazo mkabili yakiwamo malalamiko yanayotokana na uhamisho na upandishwaji vyeo walimu kudaiwa kugubikwa na utata.

Lupuga aliongeza kuwa baada ya kamati husika kukamilisha kazi yake ya uchunguzi matokeo yake yatapelekwa mbele ya Baraza la Madiwani ambapo litatoa maamuzi kutegemeana na matokeo ya uchunguzi wa kamati hiyo bila kuonea mtu.

Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom