Afikishwa mahakamani kwa kumpiga mama mjamzito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afikishwa mahakamani kwa kumpiga mama mjamzito

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Aug 23, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  MWANAUME mmoja Azizi Athumani (32) mkazi wa Kigogo Mkwajuni jijini Dar es Salaam amefikishwa kizimbani katika mahakama ya Mwanzo Magomeni kwa kosa la kumpiga mama mjamzito ambaye ni mpangaji wake. Ilidaiwa kuwa Azizi alimpiga vibao vya usoni mama huyo na kuongezea na mateke kwenye paji la uso hadi kupoteza fahamu akidai kakataa kufagia uwanja wa nyumba hiyo.

  Mwendesha Mashitaka wa kesi hiyo Hilda Balele alidai mbele ya hakimu Rukia Katembo wa mahakama hiyo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo huko eneo la Kigogo Kinondoni kwa kumpiga mpangaji wake kwa kosa la kukataa kufagia uwanja wa nyumba hiyo.

  Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Agosti 5 mwaka huu katika majira ya saa 4.00 asubuhi, eneo la Kigogo Mkwajuni na kwamba kwa makusudi kabisa alimpiga Anna Athumani usoni hadi kupoteza fahamu.

  Ilidaiwa na Balele kuwa kutokana na kipigo hiko mama huyo alianguka chini na kuzirai kutokana na hali liyokuwa nayo.

  Mahakama ilielezwa pia kuwa kutokana na kipigo hicho mama huyo alipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili na kulazwa kwa matibabu zaidi.

  Mshitakiwa alikuwa nje kwa dhamana na kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba 9, mwaka huu, itakapotajwa tena kwa mara nyingine.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2876578&&Cat=1
   
Loading...