Afikishwa Mahakamani Kwa Kuangalia Ngono Kanisani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afikishwa Mahakamani Kwa Kuangalia Ngono Kanisani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Sunday, March 14, 2010 7:44 PM
  Mwanaume mwenye umri wa miaka 55 wa nchini Marekani amefikishwa mahakamani baada ya kuzamia kanisani usiku na kuangalia video za ngono kwa kutumia televisheni ya kanisa. Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 55, alizamia kanisani usiku kwa nia ya kuiba na ndipo alipoamua kuangalia video za ngono alizokuwa nazo kwa kutumia televisheni ya kanisa.

  Tukio hilo lilitokea usiku wa siku ya alhamisi kwenye kanisa moja lililopo kwenye kitongoji cha Ames mjini Iowa.

  Mwanaume huyo alizamia kanisani usiku na kuanza kukusanya mali mbali mbali za kanisa kabla ya kuamua kupumzika kwa kuangalia video za ngono alizokuja nazo kwa kutumia televisheni ya kanisa.

  Mwanaume huyo aliangalia video hizo mpaka asubuhi ya siku ya ijumaa alipogunduliwa na waumini wa kanisa hilo waliofika kwenye kanisa hilo asubuhi na kukuta mali kadhaa za kanisa zikiwa hazionekani.

  Waumini hao walishangazwa na sauti za ngono zilizokuwa zikisikika kwenye chumba kimoja cha kanisa hilo na ndipo walipoamua kuwaita polisi.

  Mwanaume huyo alikamatwa na polisi wakati akijaribu kukimbia akiwa amebeba mfuko wa rambo uliojaa vitu mbali mbali kuanzia vyakula, vyombo vya jikoni na vifaa kadhaa vya umeme.

  "Baada ya kukusanya vitu alijiona kama vile yuko nyumbani kwake na kuanza kuangalia video za ngono", alisema kamanda wa polisi wa kitongoji cha Ames alipokuwa akiongea na gazeti la Ames Tribune.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4224250&&Cat=2
   
Loading...