Afghanistan: Zaidi ya watu 600 wamefanikiwa kupanda ndege ya Jeshi la Marekani

Nani ataendesha ilo dude......
2884812_JamiiForums220813921_540x675.jpg

Dude linaendeshwa na Marubani wa nje. Ndege zinakuja na kuondoka kama kituo cha daladala vile.
 
Baada ya kushuhudia Waafghanistan wakijaribu kudandia ndege ya Jeshi la Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khamid Karzai mjini Kabul jana, Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetoa picha inayoonesha watu 640 wakiwa ndani ya ndege yake ya kijeshi.

Idadi hiyo ya watu inatajwa kuwa zaidi ya mara tano ya uwezo wa ndege hiyo kubeba abiria na moja ya idadi kubwa zaidi kuwahi kubebwa katika ndege hiyo aina ya Boeing C-17 Globemaster III. Waliofanikiwa kuingia ndani ya ndege hiyo walitumia mlango ambao haukufungwa vizuri wakati ndege hiyo ikiwa katika uwanja wa ndege mjini Kabul.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imeripoti kuwa haikuwa na mpango wa kuwabeba watu hao, lakini ililazimika kutokana na vurugu zilizotokea katika uwanja wa ndege jana. Inaripotiwa kuwa watu wawili wamefariki baada ya kuanguka kutoka kwenye ndege hiyo.

Kujaa kwa watu katika Uwanja huo wa Ndege kulitokana na taarifa za uzushi kusambaa awali Mjini Kabul kuwa Jeshi la Marekani linatoa usafiri wa bure kuwapeleka wananchi wa Afghanistan kwenda Marekani na Kanada, ndipo mamia ya watu walipovamia uwanja huo wakijaribu kupata usafiri huo wa bure na kuyaokoa maisha yao kutoka kwa Wataliban.

Waliofanikiwa kupanda ndege hiyo - wakiwamo wanawake na watoto wachanga - wamefanikiwa kutua salama nchini Qatar.

Wapiganaji wa Taliban wamefanikiwa kuchukua udhibiti wa Mji Mkuu na mipaka ya nchi. Uwanja huo wa ndege ndio sehemu pekee iliyo chini ya udhibiti wa Jeshi la Marekani.

Chanzo: Guardian US

View attachment 1895144
Fake, photoShop,
 
Female journalists returned to work on the second day of the Taliban rule. So far, women are seen conducting live broadcasts from the streets of Kabul. Traffic is back to normal and Taliban is patrolling the streets. People are going back at work. https://t.co/EoEdUNykBM
Hii ni kwa muda tu ili kutuliza hali ya mambo. Wakianza kuweka zile sharia zao hutaona hao female Journalist kitaani. Ni mwendo wa kukaa ndani tu na ukitoka lazima uvae nguo zenye chekecheke.

9790EB6B-C9AF-43F9-A5FA-5D4A49E62F7B.jpeg
 
Hiyo haikwenda kuchukua wanajeshi ilienda beba diplomat people ila walichokutana nacho sasa
Hiyo ilipeleka wanajeshi elfu 5 ambao walienda kusaidia usalama wa wanadiplomasia wanaoondoka Afghanistan. Sasa wakati inondoka ndio hao raia wakaomba lift
 
MARA TANO ZAIDI NA PIPA LIKANYANYUKA BILA SHIDA!!! SIPATI PICHA!!
Ni ndege ya jeshi mkuu!..
. Na ukumbuke ni jeshi la marekani ambapo nwanajeshi anadhaminiwa sana kwa hiyo hata vyombo vyao vya usafiri ni vya uhakika!

Fikiria hilo dude linabeba wanajeshi zaidi ya 300 kwa hiyo Marekani hawezi kusafirshia wanajeshi wake wengi namna hiyo kwenye chombo kisicho salama.

Hapo hilo dude utakuta lina hadi vifaa vya ku detect mabomu
 
Hiyo ndege imekuwa ya mwendokasi sasa, maana limebeba uzito x5 ya kawaida yake

Na rubani akakubali na ikapaa du

Kuna movie zingine hazihitaji popcorns kabisa
Mkuu hii ni C 17 Globemaster. Ina uwezo wa kubeba mzigo mpaka tani 77 sasa sijui hao raia 600 kama wanafikia hata nusu ya huo uzito
 
Back
Top Bottom