Afghanistan Target Tanzania

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
UN Report on Heroin Flow
Afghanistan Target Tanzania



East African countries, particularly Tanzania, have been receiving more Afghan heroin flows, as the continent of Africa at large emerges as a conducive drugs trafficking route to Europe, North America and other parts of the world.

The revelation has been made in a report released recently by the United Nations Office on Drugs and Crime, which says that drug traffickers, faced with tough restrictions to transit through Asia and Middle East, have turned Africa into their preferred station for heroin shipment to Europe and elsewhere.

The report titled “The global Afghan Opium Trade: A threat Assessment” points out that Afghan heroin flows across Tanzania and East Africa are now blamed for generating increased drug abuse in the region and some parts of the continent.

It notes that during the first quarter of 2011, there were two major heroin seizures (each above 100 kg) reported by Kenya and Tanzania, adding: “The most fragile African states are particularly vulnerable, as drug trafficking organisations are able to exploit the low capacity at seaports and airports. Indeed, East Africa’s minimal law enforcement at ports of entry has encouraged drug traffickers to transit heroin from Pakistan or Gulf countries through East Africa

DOWNLOAND “The global Afghan Opium Trade: A threat Assessment” at: unodc.org (right click here and save)


Source: Thefrontierpost
 
Nyie peke yenu ndio msiojua game.....mimi nimezaliwa na kukulia uswazi.Ukisikia mtu kaenda shamba Pakistan...maana yake ameenda kuchukua mzigo(heroin/Opium),kwenye boda ya Pakistan na Afghanistan.Hii tangu zamani sana(I'm talking about eighties).Ila wanadhani haya mambo yameanza leo.
 
Nyie peke yenu ndio msiojua game.....mimi nimezaliwa na kukulia uswazi.Ukisikia mtu kaenda shamba Pakistan...maana yake ameenda kuchukua mzigo(heroin/Opium),kwenye boda ya Pakistan na Afghanistan.Hii tangu zamani sana(I'm talking about eighties).Ila wanadhani haya mambo yameanza leo.

Hakuna asiyoyajuwa hayo ila sasa yamezidi, tumeona mpaka wachungaji wakishikwa kwa kufanya hii biashara haram, tumesikia makanisa na bakwata wakihusika kwa namna moja au nyingine, hiyo pekee inaonesha kuwa hii biashara imeshamiri na inabidi ishikiwe bango ili isambaratishwe hapa kwetu.

Tunaona jinsi vijana, watoto (chini ya miaka 18) na wazee wakiathirika kwa haya maunga. Tushirikiane kwa nguvu zote kupiga vita hii biashara inayoangamiza vizazi.
 
Hakuna asiyoyajuwa hayo ila sasa yamezidi, tumeona mpaka wachungaji wakishikwa kwa kufanya hii biashara haram, tumesikia makanisa na bakwata wakihusika kwa namna moja au nyingine, hiyo pekee inaonesha kuwa hii biashara imeshamiri na inabidi ishikiwe bango ili isambaratishwe hapa kwetu.

Tunaona jinsi vijana, watoto (chini ya miaka 18) na wazee wakiathirika kwa haya maunga. Tushirikiane kwa nguvu zote kupiga vita hii biashara inayoangamiza vizazi.
Agree!....zamani walikuwa wana trffic juu kwa juu,siku hizi wanauza Bongo na Zanzibar.Wameharibu na kuua marafiki zangu wengi sana!!
 
Hakuna asiyoyajuwa hayo ila sasa yamezidi, tumeona mpaka wachungaji wakishikwa kwa kufanya hii biashara haram, tumesikia makanisa na bakwata wakihusika kwa namna moja au nyingine, hiyo pekee inaonesha kuwa hii biashara imeshamiri na inabidi ishikiwe bango ili isambaratishwe hapa kwetu.

Tunaona jinsi vijana, watoto (chini ya miaka 18) na wazee wakiathirika kwa haya maunga. Tushirikiane kwa nguvu zote kupiga vita hii biashara inayoangamiza vizazi.

Madawa ya kulevya yameshamiri zaidi kutokana na uongozi legelege katika taasisi nyingi kubwa hapa nchini tangu Mh. Kikwete aingie madarakani.

Ona haya mambo yameanza kuzungumzwa na orodha za wauza unga kutupwa kapuni na wahusika wenye mdhamana wa kutuondolea adha hii:


Serikali yaficha majina ya vigogo wauza ‘unga'
By Habari Tanzania | Published 01/22/2007


Na Charles Mullinda

MAJINA ya vigogo wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, yaliyowasilishwa na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Amina Chifupa katika Wizara ya Usalama wa Raia na kwa Rais Jakaya Kikwete, yataendelea kuwa siri.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake mwishoni mwa wiki iliyopita, Naibu Waziri wa Usalama wa Raia, Mohammed Aboud, alisema kuwa, wizara yake haina mpango wa kuyatangaza majina yaliyomo katika orodha hiyo.


Aliliambia gazeti hili kuwa, hakuna kiongozi yeyote nje ya wizara hiyo asiyehusika na taasisi za usalama, ambaye ameiona orodha halisi ya majina ya watu waliotajwa katika barua aliyotumiwa Rais Kikwete.

Alisema baada ya kupokea majina hayo, upelelezi ulianza mara moja na wananchi watarajie kuona matokeo ya kazi hiyo, hivi karibuni.

Aboud alisema, baada ya Rais Kikwete kupokea orodha ya majina hayo na kuyawasilisha kwa Waziri wa Usalama wa Raia, Bakari Mwapachu, ambaye pia alikayabidhi kwa viongozi wa juu wa Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufanyiwa kazi, uchunguzi ulianza kufanywa kwa tahadhari kubwa na usiri, ili kutoharibu ushahidi.

Alisema baada ya kuanza kwa uchunguzi huo, ilibainika kuwa, kunahitajia usiri wa hali ya juu, ili kufanikisha kazi hiyo kwa ufanisi, kwa sababu wauzaji dawa za kulevya ni wajanja na wenye uwezo mkubwa kipesa, hivyo ni rahisi kuharibu ushahidi.

"Tunachukua hatua kwa uangalifu sana, vinginevyo tutaharibu, tunawaomba wananchi wawe wastahamilivu, vita inaendelea na sisi tunaelekea kushinda, lakini hatutataja mtu miongoni mwa wote waliotajwa.

"Watuhumiwa waliotajwa katika orodha iliyopelekwa kwa Rais Kikwete ni wengi na aliowataja Amina nao ni wengi, lakini watabaki kuwa siri, si kwa sababu yoyote mbaya ila ni kwa mujibu wa taratibu za kufuatilia kesi za aina hii," alisema Aboud.

Alisema vyombo vya usalama vinafuatilia kila mtu aliyetajwa kwa makini na uangalifu na vikithibitisha kuwa anahusika, anakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aboud alisema, hatua iliyofikiwa ni kubwa na wengi wa waliotajwa wamekwishachunguzwa. Aliahidi kuwa, mpaka mwishoni mwa mwezi wa Februari, wananchi watashuhudia hatua kubwa zitakazokuwa zimechukuliwa dhidi ya wale watakaokuwa wamethibitika kuhusika na biashara hiyo.

....inaendelea....
Habari inatoka hapa: http://www.habaritanzania.com/articles/2667/1/Serikali-yaficha-majina-ya-vigogo-wauza-%91unga%92

Mh. Rais Kikwete amekuwa na orodha ya wauza unga tangu 2006, lakini mpaka hii leo hatujasikia hata mmoja akiwa ametiwa nguvuni. Kwa aina hii ya uongozi inayopenda misifa kwa kutoa matamko makubwa lakini utekelezaji wake ni zero, tatizo litaongezeka au kupungua?? Ona habari hii ya mwaka 2006:

Vigogo dawa za kulevya watajwa


Written by Mwananchi
Monday, 18 September 2006


*Majina yao yapelekwa kwa Rais Kikwete
*Ni orodha ndefu ya majina ya watu 58
*Wamo wafanyabishara, wanasiasa, viongozi wa dini
*Mbinu wanazotumia nazo zaanikwa hadharani

WITO wa Rais Jakaya Kikwete wa kutaka wananchi wajitokeze kutaja majina ya wahalifu nchini, umepata mwitikio mpya, safari hii watu kadhaa wakijitokeza kutaja majina ya vigogo wanaoongoza kwa biashara ya dawa za kulevya nchini.

Majina hayo yako katika barua iliyoandikwa na wananchi 15 kwenda kwa Rais Kikwete, ambamo wanadai kwamba walikuwa wakitumiwa na vigogo hao kufanya biashara hiyo, lakini sasa wameamua kuachana nayo. Barua hiyo iliandikwa Septemba 8, mwaka huu na wahusika wanadai wamekwisha kuiwasilisha Ikulu.

Kwa mujibu wa barua hiyo, majina 58 yameorodheshwa yakiwa katika makundi matatu makubwa, la kwanza likiwa ni waagizaji wakubwa wa dawa hizo; la pili ni wafadhili ambao majina yao hutumika kusafirisha dawa hizo; na la tatu ni wauzaji walioko Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Mbeya na Zanzibar.

Katika orodha ya waandishi wa barua hiyo wanaodai kusukumwa na uzalendo na uchungu kwa nchi yao, yamo majina ya wafanyabiashara maarufu nchini na wanasiasa, wakuu wa taasisi nyeti, baadhi ya viongozi wa dini na maafisa wa juu serikalini.

Kundi la kwanza lina majina 12, miongoni mwao ni wafanyabiashara maarufu katika miji ya Dar es Salaam, Morogoro, Zanzibar, Arusha na Bagamoyo na baadhi ya viongozi wa dini wa madhehebu fulani.

Kundi hili linadaiwa kuwa linaingiza dawa za kulevya kwa njia mbalimbali zikiwamo, kutumia mipira ya kondomu, majokofu, vifaa vya hospitali, meli na marobota ya mitumba.

Katika kundi la pili kuna watu 19, miongoni mwao wamo wanasiasa wakubwa nchini wakiongoza kundi hili, kutoka taasisi ya fedha nchini na wafanyabiashara maarufu wa Dar es Salaam na Zanzibar.

Kundi la tatu lina majina 27, ambao si ya watu wenye majina makubwa, lakini ndio wanaotumika kusambaza mitaani kwa watumiaji wa dawa za kulevya.

Mbali ya kushiriki katika kusambaza dawa za kulevya, kundi hili pia lina baadhi ya majina ya watu waliotajwa kushiriki katika kuingiza silaha nzito zinazotumika kwa ajili ya ujambazi kutoka nchi jirani.

...inaendelea...
Inatoka hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/257-majina-ya-wauza-madawa-ya-kulevya-jk-anayo-4.html
 
Biashara ya madawa ya kulevya Heroin, Chalas, Opium, Khat, muda mrefu sana watu wanafanya hapa Tanzania.
Kuna mtandao mkubwa sana wa hii biashara, vijana wengi wa kitanzania kwa tamaa zao za kimaisha tumewapoteza baada ya kuingia kwenye kazi hiyo wamejaa kwenye magereza sehemu tofauti. HongKong, China, Japan, Thailand, Macao,
Hizi nchi nilizozitaja vijana wanapewa dola 10,000 kila kichwa ukifikisha unga.
Cha hatari zaidi katika nchi hizo ukikamatwa na unga wanakufunga miaka mingi. Mfano China kama una mzigo mwingi wanakunyonga, kuhukumiwa miaka 50 ni kawaida tu.
Ulaya nako ndio usiseme uzuri wa ulaya ukikimatwa unafungwa miaka michache, na ugumu wa Ulaya ni viza tofauti na Asia viza rahisi
 
Inabidi Makanisa na Bakwata wachunguzwe kwa kina.


Serikali legelege ndio inayoleta haya madhara, ikiwa inawajua wauza unga kwanini isiwakamate? Huyu Fisadi Kikwete inawezekana nae anafaidika na haya Maunga. Huwezi kusema eti waache kuuza unga au tutawachukulia hatua. Huyu Fidsadi ameiharibu na bado anaiharibu nchi yetu kila siku anatoa muda kwa wahalifu na kuwaambia waache au kama umeiba pesa za EPA na kupa muda uzirudishe Huu ni ujinga utaisha lini Serikalini wa kutowachukulia hatua wahalifu?

Tahadhari Watanzania wenzangu hii Serikali Legelege ya Huyu Fisadi ishatupeleka pabaya na bado itatusukuma sehemu ambayo hatuwezi kuvumilia tena huu ujinga wake. Tuchukueni hatua
 
Hivi kwa nini FF anaandika Makanisa na Bakwata? Kwa nini isiwe Misikiti na Makanisa au Mapadre/Wachungaji/Maaskofu vs Masheick?

Au kuna kitu mie hapa sielewi? Hii ni kitu ni janga jingine la Taifa na si jambo la kujifanya Mie Muislaam/Msikiti silifanyi. Wanafanya watu wa kila aina na kila Rangi. Zinafanya taasisi tofauti na hata za dini, bila kujali ni dini gani.

Ukisoma alichoweka X-Pastor ni kuwa hii hali inatokea sana kwenye nchi za Africa ambazo serikali yake ipo legelege. Hatimaye Effect za Ulegelege wa Uongozi wa Tanzania zimeshaanza kuonekana waziwazi hadi nje.Ila utaona JITU zima na nywele zimeota kila kona, linajifanya halioni hilo na linashinda kutetea Uozo. I hope kwenye familia yao, atazuka Teja mmoja wa nguvu na yeye atashinda akifurahia Uongozi wa Tanzania.
 
watu wanaoyaingiza hayo madawa wanafahmika tatizo kila siku zinatoka political talk tuu n no action taken
 
Back
Top Bottom