Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,500
- 9,279
Jeshi la Marekani limesema limemuua mtu anayedaiwa kupanga shambulizi kwenye uwanja wa ndege wa Kabul baada ya kufanya shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani.
Operesheni hiyo ya usiku wa kuamkia Jumamosi ilimlenga mtuhumiwa wa kundi la wanamgambo lenye mafungamano na lile linalojiita Dola la Kiislamu, IS-K kwenye jimbo la mashariki Nangahar. Msemaji wa Kamandi Kuu ya Marekani, Bill Urban amesema dalili za awali zinaonesha kuwa wamemuua mlengwa na hakuna raia wowote waliouawa.
Shambulizi hilo limefanyika baada ya Rais Joe Biden kuapa kupambana na IS baada ya mashambulizi ya Alhamisi yaliyosababisha mauwaji ya wanajeshi 13 wa Marekani na takriban raia 79 wa Afghanistan. IS ilikiri kuhusika na shambulizi, huku kundi la Taliban likikanusha kuhusika kwa namna yoyote ile. Biden pia aliliagiza jeshi kufanya mashambulizi dhidi ya viongozi wa IS, pamoja na mali za kundi hilo.
Ama kwa upande mwingine, Marekani imesema itaendelea kuwaondoa raia wa Afghanistan kutoka uwanja wa ndege wa Kabul hadi dakika ya mwisho, licha ya kuwepo wasiwasi kuhusu mashambulizi zaidi ya kundi la IS.
DW