Elections 2010 Afarki akisherehekea ushindi

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Monday, 01 November 2010 11:44

Kwirinus Mapunda, Tunduma MTU mmoja anayesadikiwa kuwa ni Mwanachama wa Chama cha CUF Mussa Bakari (27) amefariki gafla usiku wa kuamkia Novemba 1 mwaka huu, baada ya kunywa pombe aina ya gongo katika harakati ya kushangilia ushindi kwenye uchaguzi mkuu.

Mwanachama huyo ambaye ni mpambe wa mgombea wa ubunge wa CUF jimbo la Tunduru Kaskazini, Rajabu Mazee aligundulika amekufa saa 4:00 asubuhi ya Novemba 1.

Marehemu huyo baada ya kunywa pombe hiyo alirudi nyumbani kwake na alizidiwa na kukutwa asubuhi akiwa ameshakufa, saa 4:00 asubuhi.

Mazee aliliambia gazeti hili kuwa, Musa Bakari ni rafiki yake wa karibu na alimtoa Dare s salaam maeneo ya Mbagala kwa kusudi la kuja kudhibiti wizi wa kura ambao alipata habari kuwa CCM wangeweza kuufanya.

Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda ambaye yupo wilayani Tunduru amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na ameasema kifo hicho hakina uhusiano na uchaguzi.
 
... MTU mmoja anayesadikiwa kuwa ni Mwanachama wa Chama cha CUF Mussa Bakari (27) amefariki gafla usiku wa kuamkia Novemba 1 mwaka huu, baada ya kunywa pombe aina ya gongo katika harakati ya kushangilia ushindi ...
Mimi nilidhani pombe ni haramu!
 
Apumzike kwa amani maana uchaguzi wa mabadiliko kama huu uanaenda watu
 
Back
Top Bottom