Afanyeje kumpima mtoto DNA?

K-Boko

JF-Expert Member
Aug 3, 2013
697
218
Kuna jamaangu kahitaji msaada. Ameniuliza ili ampime DNA mtoto wake mdogo wa miezi kadhaa afanyeje? Yaani process ikoje? Aende na mtoto hospitali? Je ni hospitali ipi Dar yenye huduma hiyo? Je gharama zake ni vipi?

Mimi nimekwama. Lakini nikamwahidi nitajaribu kuuliza kwa wadau. Tafadhali tiririkeni!
 
Nenda Government Chemist Laboratory Agency (GCLA) ndio wanapopimia, pia utapewa maelekezo hitajika yote.
 
Kuna jamaangu kahitaji msaada. Ameniuliza ili ampime DNA mtoto wake mdogo wa miezi kadhaa afanyeje? Yaani process ikoje? Aende na mtoto hospitali? Je ni hospitali ipi Dar yenye huduma hiyo? Je gharama zake ni vipi? Mimi nimekwama. Lakini nikamwahidi nitajaribu kuuliza kwa wadau. Tafadhali tiririkeni!
Aisee we kama umetokwa umetokwa tu DNA ya nini hasa..utakuja leta madhara baadaye kama mtoto si wako...
 
Sina hakika why anauliza. Ila ni mtu na hekima na busara zake na nina hakika hataleta madhara. Sitaki kujua mengi, zaidi ya kumjibu tu coz ni mtu wa karibu yangu kwa kweli.
 
Nenda Government Chemist Laboratory Agency (GCLA) ndio wanapopimia, pia utapewa maelekezo hitajika yote.

Hawa jamaa wazinguaji tu.
Wanasema mashine yao ni kwa ajili ya research na si kuvunja ndoa. Wanaweza kukupa majibu feki. Hebu jaribu kumpeleka na mtoto asiye wako kisha uwapime.
 
GCLA ipo mbele ya Ocean Road Hospital,njia ya nyuma ya kwenda Ikulu/Ferry...ulizia kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.
 
Hawa jamaa wazinguaji tu.
Wanasema mashine yao ni kwa ajili ya research na si kuvunja ndoa. Wanaweza kukupa majibu feki. Hebu jaribu kumpeleka na mtoto asiye wako kisha uwapime.

Duh! Kwa hiyo huko hakuna uhakika, au vipi?
 
Nilishawahi kuulizia Muhimbili mwaka 2009 wakaniambia wanaohusika na DNA ni ofisi ya mkemia mkuu ambayo iko Ocean Road Hosp. Na gharama wakasema ni laki moja kwa kila sample yaani Baba, mtoto na mama(kimsingi hamna mama anayesingiziwa mtoto). Lkn pia lazma upate kiapo kutoka mahakaman cha wazazi (wote) kukubali kupima.

Huwezi kumchukua mtoto kinyemela bila ruhusa ya mama yake mahakamani kwa kutia saini hati ya kiapo!!
 
Nilishawahi kuulizia Muhimbili mwaka 2009 wakaniambia wanaohusika na DNA ni ofisi ya mkemia mkuu ambayo iko Ocean Road Hosp. Na gharama wakasema ni laki moja kwa kila sample yaani Baba, mtoto na mama(kimsingi hamna mama anayesingiziwa mtoto). Lkn pia lazma upate kiapo kutoka mahakaman cha wazazi (wote) kukubali kupima.. Huwezi kumchukua mtoto kinyemela bila ruhusa ya mama yake mahakamani kwa kutia saini hati ya kiapo!!

Shukran sana, Joe!
 
"Isale" ndio nini Bujibuji?

UKIONDOA vitabu vitakatifu vya Biblia na Koran mmea unaojulikana kwa jina la Sale au Isale unashikilia nafasi kubwa pia kwa kuthaminiwa na watu wengi wa kabila la Wachaga kutokana na umuhimu wake katika kudumisha amani, upendo na mshikamano miongoni mwa jamii hiyo.

Kitaalamu mmea wa Isale unajulikana kama Dracaena afromontana na unasifika kwa kilimo cha mseto kwa kuwa una uwezo mkubwa wa kuhimili ukame, haupati magonjwa kwa urahisi, hauambukizi mimea mingine magonjwa, hauweki kivuli kikubwa wala mizizi yake haiathiri mimea mingine.Mmea huo wenye pingili mithili ya miwa na majani marefu membamba una uwezo wa kutunza maji.

Unaelezwa kuwa na faida nyingi hivyo wataalamu wa kilimo huwashauri wakulima wa kilimo cha mseto kuutumia kwa ajili ya malisho ya mifugo, kurutubisha shamba ama kuotesha kwenye mipaka ya mashamba kwa ajili ya kuzuia moto.

Huenda faida na umuhimu wa mmea huo zimesababisha jamii ya Wachaga ambao hulima kahawa na migomba kuendelea kuuthamini na kuuenzi hata baada ya dini za Kikristo na ya Kiislamu kusambaa katika Mkoa wa Kilimanjaro na kusambaratisha ibada za kimila.

Ingawa asilimia kubwa ya Wachaga ni waamini wa dini ya Kikristo ambao hawaamini sanamu wala miungu, mmea wa Isale una nafasi kubwa katika maisha yao ya kiroho hasa imani kwamba unadumisha upendo, amani na mshikamano. Mmea huo pia hutumika kama mlinzi madhubuti wa familia.

Ingawa wataalamu wanasema kuwa mti huo huoteshwa kwenye mipaka kwa ajili ya kuzuia moto kusambaa kwa urahisi kwa kuwa una maji mengi na majani ya kijani kibichi yasioungua kwa urahisi, Eliamini Massawe anasema asilimia 90 ya Wachaga huotesha mmea huo kwenye mipaka ya mashamba ya kahawa na migomba kwa imani kwamba una uwezo wa kulinda mtu mwenye nia mbaya asisogeze mpaka au kuvuka kwa lengo la kwenda kuiba mali.

"Sisi Wachaga tunaamini kwamba Isale lina nguvu sana… Kama mtu akijaribu kuling'oa na kusogeza mpaka ili aibe ardhi ya mwenzake anapatwa na balaa ambayo itaendelea kurithiwa na kizazi chake," anasema Massawe. Anaendelea kusema: "Pia mtu akivuka mpaka na kwenda kuiba ndizi au kahawa anapatwa na balaa. Ndio maana huwezi kukuta migogoro mingi ya mashamba ya kahawa na migomba mkoani Kilimanjaro."

Majani ya mti wa Isale hutumiwa na asilimia kubwa ya Wachaga kwa ajili ya upatanisho na kutoa baraka. Pia kuna baadhi ya Wachaga ambao hutumia jani hilo kuapa, kuthibitisha jambo, kulaani, kutoa mikosi, kufunga laana, kukaribisha mtu kwenye ukoo hasa mwanamke baada ya kuolewa au mtoto aliyezaliwa.
Ikiwa mtu ametenda kosa kubwa hata kama ameua huchukua jani la Isale kwa ajili ya kuomba msamaha na hapo kesi inaisha bila kupewa adhabu. Inasemekana miaka ya nyuma mtu akifanya kosa huchukua jani hilo na kwenda kwa mhusika kisha husema, "ndugu yangu, nimekuja na jani hili la Sale kuomba msamaha kwani nilikuwa nakata mti na kwa bahati mbaya umeangukia shambani kwako na kuua mtoto wako. Naomba unisamehe tafadhali."

Hata kama mtu aliyetendewa kosa atakasirika atalazimika kumsamehe mhusika na kuendelea kushirikiana naye bila kinyongo wala kulipiza kisasi. Inaaminika kwamba nguvu za jani la mti wa Isale zinaweza kusababisha mikosi au maafa zaidi kwa aliyekosewa endapo hatatoa msamaha kwa moyo mkunjufu.
Ikiwa kijana wa ukoo fulani amehusika kwenye uhalifu kama vile kuiba, kubaka au kumuachisha msichana shule kisha wazazi wake wakawahi kuomba msamaha kwa kutumia Isale kesi hiyo haitafikishwa mahakamani. Kesi itasikilizwa na wazee wa pande zote mbili kisha wazazi au koo wa mkosaji utalipa faini na fidia kwa mujibu wa matakwa ya aliyekosewa.

Ikiwa ni kesi ya wizi au ubakaji mhusika huitwa mbele ya shauri na kuonywa kisha kuapishwa kwa kutumia jani la Isale ili asirudie vitendo viovu na akirudia hufikwa na balaa. Ikiwa ni kesi ya msichana kupewa mimba wazazi wa kijana husika hulazimika kutoa posa kwa masharti ya kumuendeleza msichana huyo kielimu baada ya kujifungua.

Endapo msichana atakataa kuolewa basi wazazi wa kijana watagharimia matunzo ya mtoto atakayezaliwa na baadhi ya familia hukubaliana kutoa matunzo pamoja na kumsomesha msichana huyo baada ya kujifungua na ahadi hiyo ni lazima itimizwe vinginevyo ukoo ulioahidi utapata balaa.

Jani la Isale hutumika wakati wa kuposa kama njia ya kuunganisha undugu kati ya ukoo wa msichana na kijana aliyeoa. Kama sherehe ya harusi inafanyika vijijini wanachinja ng'ombe na mbuzi kisha vifurushi vya nyama hufungwa kwa majani ya migomba na kuwekewa Isale kuashiria kuwa chakula ni salama na kimetolewa kwa shughuli maalumu.

Pia Isale hutumika kama ishara ya kutakiana upendo na baraka kwa koo zilizounganisha undugu. Kama ilivyo kwa makabila mengine, miaka ya nyuma wasichana walipaswa kujitunza ili wasipoteze ubikira. Ikiwa mwali aliyeolewa atakutwa bikira akinamama huchukua pombe kwenye madebe yaliofungiwa majani ya Isale na vikapu maalumu vyenye zawadi na kupeleka kwa wazazi wa msichana.

Ikiwa itabainika kuwa msichana huyo hakuwa bikira basi wazazi wa msichana watalazimika kurudisha pombe iliolala kama ishara ya kumshusha msichana huyo thamani kwa kosa la kupoteza bikira kabla ya ndoa. Inaaminika kuwa wazazi wa msichana wakipokea madebe hayo wakati msichana huyo sio bikira basi msichana huyo hatapata mtoto au watoto wote watakufa.

Hata hivyo Wachaga wameacha utamaduni huo kutokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha. Kwa miaka ya nyuma, simulizi zinaonesha kwamba Isale liliweza kutumika kuhalalisha vitendo vya ubakaji ambapo wavulana walikuwa wanamvizia msichana na kumteka kisha kumpeleka nyumbani kwa kijana anayehitaji mke.

Kwa vile ni marufuku msichana kulala nyumbani kwa mwanamume au kukutwa na mvulana katika mazingira yanayoashiria kuwa wanauhusiano wa mapenzi, basi msichana akilala nyumbani kwa mwanamume ilihesabika kwamba ameolewa hivyo hata kama alikwenda kwa kutekwa ama kulazimishwa.
Baada ya hilo kutokea, wazazi wa kijana aliyelala na msichana bila kufuata taratibu wakipata habari, huchukua Isale na kumtuma mtu kwenda kuomba radhi katika familia ya msichana huyo.

Aliyetumwa akifika, baada ya kukaribishwa husema: "Mimi ni mpita njia kutokea ukoo fulani. Nimekuja kuwaarifu kwamba yule binti yenu mnayemtafuta hajapotea bali kijana wetu amemchukua… Naomba mpokee jani hili kama alama ya upatanisho na ishara ya kuthibitisha kwamba siku za karibuni tutakuja kuposa."

Mtoto wa Kichaga huanza ‘kufaidika' na mmea wa Isale siku chake baada ya kuzaliwa kwani jivu laini la mmea huo hupakwa kwenye kitovu cha mtoto mchanga kama dawa. Kadhalika baadhi ya familia hupenda huweka jani la Isale chini ya nguo anazolalia mtoto kama kinga dhidi ya mahasidi au kwa lengo la kumlinda mtoto asifikiwe na upepo mbaya au mizimu.

Mtoto anayezaliwa katika kipindi cha misukosuko ndani ya familia kama vile ugomvi baina ya baba na babu au mama na bibi huchinjiwa mbuzi na kabla mbuzi huyo hajachinjwa Sale hutumika kuomba amani na upendo. Baada ya mbuzi kuchinjwa damu kidogo huchukuliwa kwa jani la Sale na kupakwa kwenye paji la uso wa mtoto kama njia ya kuzuia asikumbwe na hali ya mikosi hasa ugomvi ambao ulikuwepo kwenye familia wakati wakizaliwa.

Tofauti na maendeleo ya sasa ya teknolojia katika kutumia vinasaba kutambua baba au familia ya mtoto, Wachaga walitegemea sana jani la Sale kusuluhisha ugomvi kuhusu nani baba halali wa mtoto. Kama msichana akipata mimba na kudai baba wa mtoto ni kijana wa Kichaga, msichana huyo huchukuliwa na kutunzwa na wazazi au ndugu za kijana husika hadi atakapojifungua.

Baada ya kujifungua, wazee humpatia msichana huyo jani la Isale na kumtaka akubali mtoto wake apokee baraka na ulinzi wa familia kama kweli mtoto huyo ni wa kijana wa ukoo wao. Hata hivyo humtahadharisha juu ya balaa linaloweza kumpata mtoto ikiwa sio damu ya ukoo husika.

Wanawake waliojaribu kudanganya juu ya baba wa mtoto walilazimika kusema ukweli wanapopewa jani la Isale ili kuokoa maisha ya mtoto pia kujiepusha na balaa. Baadhi ya Wachaga wana utamaduni wa kuwaenzi watoto hasa mzaliwa wa kwanza kwa kuchinja mbuzi baada ya mtoto anapotimiza miezi mitatu kisha mtoto huyo hupakwa damu kwenye paji la uso kwa kutumia Isale.

Inaaminika kuwa kitendo hicho hufanyika kwa lengo la kuondoa mashaka juu ya baba wa mtoto na wengine hufanya hivyo ili kuonesha tofauti ya mtoto wa kwanza na watoto wengine kwani mtoto wa kwanza kupewa heshima na wakati mwingine anakuwa na nguvu ya kufanya maamuzi kuliko watoto wengine.

Kitendo cha kuchinja mbuzi hufanyika kwa lengo la kumkaribisha mtoto kwenye familia husika, kumlinda na mabaya pia kumtakia maisha mema na kumuombea baraka kutoka kwa mababu wa ukoo.
Wachaga wanaamini kwamba ikiwa mtoto aliyepakwa damu sio wa ukoo husika anapatwa na mikosi na misukosuko itakayoashiria si damu ya ukoo husika na kama mama wa mtoto akichelea kutubu mtoto anakufa au kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Miaka ya nyuma baadhi ya Wachaga walitumia jani la Isale kuapisha na kulaani ikiwa mkosaji atakataa kuomba msamaha huku akijua ametenda kosa kubwa.
 
Wachaga wanaamini kwamba ikiwa mtoto aliyepakwa damu sio wa ukoo husika anapatwa na mikosi na misukosuko itakayoashiria si damu ya ukoo husika na kama mama wa mtoto akichelea kutubu mtoto anakufa au kupotea katika mazingira ya kutatanisha
. Miaka ya nyuma baadhi ya Wachaga walitumia jani la Isale kuapisha na kulaani ikiwa mkosaji atakataa kuomba msamaha huku akijua ametenda kosa kubwa.
Bujibuji wewe mkali
 
Last edited by a moderator:

Aise Bujibuji huu mti na majani yake yanaweza kuwa yalisaidia wakati huo tu hata huko uchagani, sidhani kama wachaga wa sasa wanajali tena habari ya isale! Thanks kwa juhudi lakini article ndefu na sijui umeiibua kutoka wapi--thanks man!
 
Wanaendelea ku keep culture yao
Na huu ni mwezi wa hayo makitu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom