Afanyeje baada ya kutochaguliwa Form Five?

Andrew Sosipeter

Senior Member
May 29, 2016
189
33
Ndugu wanaJF,

Kuna dogo langu anahitaji msaada wa mawazo afanyeje baada ya kutochaguliwa?

Amehitimu kidato cha nne mwaka jana ila amekosa sifa za kuchaguliwa kidato cha tano na matokeo yake yapo HIVI DIV III 25 CIV D HIST D KISW C CHEM C ENG C GEO D BIOS D PHYS F B /MATH D na alifanya application NACT, sasa anahofia KUTOCHAGULIWA hata pia na NACTE maana hawaeleweki. Aliaply Afya na Education.

Je, afanyeje? Msaada wa mawazo please.
 
Mimi Simshauri aende Private School Coz Hajui Huko Advance Ataibuka Na Nini Kwani Huenda Akenda Akaboronga! Na vile vile Kutokana Na Hayo Matokeo Ni Wazi Kuwa Ataenda Kusom Art jambo Ambao ni Kujirisk yeye mwenyewe Kwa Hatma Yake Ya Baadae (I mean his/her Future Plan).

Sasa Ni jambo la Busara Kama Ana Vijihela Japo Kidogo Ni Bora Akatafute Chuo/College Akajiunge Akasome Certificate Kwani Anazosifa Za Kusoma Certificate Kwa Fani Ambayo itamuezesha Kuajiriwa au Kujiajiri.

Anaweza Ona Kuwa Kuanza Certificate ni Mizinguo, Lakini Ajuwe Kwamba Ndiyo Njia Peke itakayomsaidia Kufikia Malengo! Si muda mrefu Akitoka Certificate Ataendelea na Diploma, Baada Ya Diploma Ataendelea Na Digree, Wengi Wameanzia Huko Na Sasa Wana Digree za Maana.

Ni Ushauri tu Mkuu, Kama Haukukuridhisha Unaweza Utia Kwenye Dustbin.
 
Kuna second selection ambayo watoto wengi watakwenda /wameshakwenda private na hivyo kutakuwa na uwezekano wa kupata kwa pass zake!
 
Kama hela ipo aende college tuh na sio hizi college uchwara asome za maana wanazofundisha vizuri na vyenye status nzuri asomee kitu cha maana ambacho kitampa msingi mzuri wa kujiri au kuajiriwa aendelee na maisha aeleze anataka kufanya nn hapo baadae kama king ngwaba alivyosema
 
huyo hana haja ya kwenda form 5, tokeo lake linatosha kuanza ngazi ya diploma katika baadhi ya vyuo vya serikali mshauri afuatilie kozi itakayomfaa aanzie hapo!
 
Mimi Simshauri aende Private School Coz Hajui Huko Advance Ataibuka Na Nini Kwani Huenda Akenda Akaboronga! Na vile vile Kutokana Na Hayo Matokeo Ni Wazi Kuwa Ataenda Kusom Art jambo Ambao ni Kujirisk yeye mwenyewe Kwa Hatma Yake Ya Baadae (I mean his/her Future Plan).

Sasa Ni jambo la Busara Kama Ana Vijihela Japo Kidogo Ni Bora Akatafute Chuo/College Akajiunge Akasome Certificate Kwani Anazosifa Za Kusoma Certificate Kwa Fani Ambayo itamuezesha Kuajiriwa au Kujiajiri.

Anaweza Ona Kuwa Kuanza Certificate ni Mizinguo, Lakini Ajuwe Kwamba Ndiyo Njia Peke itakayomsaidia Kufikia Malengo! Si muda mrefu Akitoka Certificate Ataendelea na Diploma, Baada Ya Diploma Ataendelea Na Digree, Wengi Wameanzia Huko Na Sasa Wana Digree za Maana.

Ni Ushauri tu Mkuu, Kama Haukukuridhisha Unaweza Utia Kwenye Dustbin.
Kuboronga au kufanya vizuri form six kutategemea sana na juhudi atakazowekeza katika masomo yake. Naona hoja ya kwamba aliendelea advance sababu hajui huko ataibuka na nini (huenda akaboronga) inawezekana isimsaidie sana.

Ukweli ni kwamba kama atapata shule aende, afanye bidii ya ziada ili "atoboe". Wazo la kwenda chuo kusoma certificate licha kuu nafasi ya pili. Na hata akipata chuo ni lazima asome bidii maana tofauti na hapo ni kazi bure tu.
 
hapo hkl inamuhusu ila kama KE bora asome nurse na kama ME lab techincian na km angekua na pass ya physics angekua na uwanja mana wa kusoma any engineering course au CO kuanzia certificata na kuendelea ingawaje pia kwa hayo matokeo any b'ness course inakuhusu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom