Afande wangu Kova, Vijana walioandamana jana mtawafikisha Polisi/ Mahakamani lini?

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,459
29,153
Habari za Asubuhi Kamanda Kova,

Ni matumaini yangu hua unapitaga pitaga humu kwenye hili Jukwaa, au kama sio wewe basi vijana wako wanapitaga na kukuletea taarifa. Maana hata mara nyingi nakusikiaga ukilitaja hili Jukwaa.

Sasa mimi nina swali dogo tu kwako Afande wangu Kova, ni kuhusu wale vijana waliokamatwa Jana wakiandamana kutokea maeneo mbalimbali kuelekea zilipo ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Demokrasiana Maendeleo (CHADEMA). Wale waliokua wakidai eti wao ni wana-Chadema na eti kua wamehuzunika na kukasirika sana kwa Dkt Slaa kujitoa CHADEMA. NI kwamba tu nlikua naomba kujua kama wameshafikishwa mahakamani au bado maana ukweli hata mimi wale vijana walinisikitisha sana kuamua kuandamana bila kibali.

Swali au ombi langu hili linachagizwa zaidi na wale vijana wa 4U MOVEMENT ambao walikua wamekusanyika (inasemekana bila kibali) kukamatwa na kufikishwa Polisi kisha mahakamani kwa haraka sana. Sasa niliomba tu kujua kama na hawa pia watapitia mkondo uleule wa vijana wale.

Afande wangu Kova naomba nieleweke tu sina nia ya kuingilia utendaji wa Jeshi lako la Polisi, bali ni ile tu sintofahamu niliyokumbana nayo juu ya vijana hawa, kwani kwa uelewa wangu mdogo naona kama hawa wana makosa makubwa zaidi kuliko wale wa kwanza. Wale walikutwa wamekusanyika tu, lakini hawa walikusanyika na wakaanza kutembea/kuandamaba.

Zaidi ya yote nakutakia utendaji mwema wa Jeshi lako la Polisi Kamanda wangu.

Wako,
Shark wa JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

Ingekuwa vyema pia waliotajwa kuratibu zoezi hilo wakaunganishwa
 
Last edited by a moderator:
Wale watakuwa wapo huru tokea jana ile ile maana mpango wote ulivurugika.
Magamba mwaka huu mtahangaika sana.
 
Hawezi kujibu hata kwa dawa!.... Anaogopa kupoteza kitumbua chake!...
 
Majibu ya Kova hapa yatakuwa ya KISOMI mno. Atajibu hivi kwa jinsi tumuelewa askari huyu 'msomi', " kusudio la kutenda kosa ni baya zaidi kuliko kutenda kosa lenyewe, hivyo hawa kwa vile wameshatenda kosa tumeona tuwaachie tuu ili liwe fundisho kwa wale wenye kusudio la kutenda kosa"
 
Lowassa kirusi chadema aise!! nakumbuka "Atakaye muunga mkono lowassa akapimwe akili"
Mkuu,
Mi sijaongelea Lowassa kwenye huu uzi, bali ni Vijana waliojiita wa Chadema ambao bila shaka jana walikusanyika wakaandamana bila kibali. Maana wale wa mwanzo wa 4U walipelekwa polisi kisha mahakamani katika kipindi kifupi sana.
 
Walioratibu hao wanaongea baada ya zoezi
Hii ni aibu na fedheha kwa hao aliowataja Masaburi, akiwepo Rais, Mgombea Urais na wengine. Kwamba wanaweza kuutambua mpango ovu kama huu na kuubariki.
Kama kawasingizia wanatakiwa wamkane vinginevyo kama kunakuja kutokea maafa kwa mambo haya basi watahesabika wanahisika na kama huko mbeleni kutakuwa na makosa ya kijinai ya kushughulikiwa huu ni ushahidi wa kuwaingiza moja kwa moja kwenye tuhuma. Yale yale ya Kenyatta kule Kenya.
 
Hao waliotajwa hawawezi kuingilia Kati sababu na wao ni wafaidika wa huu mpango haramu!!
 
Back
Top Bottom