Uchaguzi 2020 Afande Sele: Wasanii wengi walikimbilia siasa wakitegemea umaarufu wao utawapitisha

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Msanii wa muda mrefu kwenye kiwanda cha muziki Bongo, Selemani Msindi, maarufu kama Afande Sele, amesema kwenye mchakato wa uchaguzi mwaka huu amejifunza kuwa wajumbe hawaangalii sura, pesa au umaarufu wa mtu ili kumpitisha kwenye uongozi.

Afande Sele ametoa mtazamo huo baada ya wasanii wengi kutia nia za kugombea ubunge ila wameishia kukatwa na wajumbe huku wengine wakishindwa kwenye uchaguzi mkuu.

“Kuhusu wajumbe nilijifunza kwamba jamii ya Watanzania hawamchagui mtu kwa sababu ya sura yake, umaarufu wake au pesa zake, huwa wanatazama mtu ambaye kimisingi atakuwa mwenzao kuanzia kushughulika naye na kuzunguka naye kwenye maeneo yote,” amesema Afande Sele.

“Kwa bahati mbaya wasanii waliingia kwenye mchakato huu hasa kwenye chama tawala wakitegemea sana umaarufu wa majina yao na sponsa waliokuwa nao kwamba watapata back up za pesa ya kampeni na wajumbe, lakini wananchi hilo ni jambo la mwisho kwao,” ameongeza.
 
Sio lazima wote wapate, Mwana FA kapita, uoga wako ndio umasikini wako,walioshindwa anyway wamejaribu na huenda wakajifunza wapi walikosea ili next time warekebishe, safari ya kisiasa sio sawa na kuweka chumvi kwenye mboga ikolee muda huo huo.
 
Anajisema yeye mwenyewe, Mwaka 2020 hakukuwepo uchaguzi Tanzania kwa sababu watawala walijiteua wenyewe kwa kutumia tume iliyokua upande mmoja wa uchaguzi, Hakuna mshindi katika huo uchaguzi bali uchafuzi.
 
Back
Top Bottom