Afande Sele, Urafiki wetu na wewe hauko kwenye sanduku la kura

Yani chadema bana, mtu akihama chama Chao kawa adui na kupewa sifa za ajabu ajabu.
Watu wanahama dini iweje mtu kuhama chama iwe nongwa acheni ushamba wa siasa uchwara, hata prof . Jay akihama mtaanza kusema mlevi yule mvuta bangi hafai bora hivo kahama wakati sasa hivi mpo kmy.
 
Acha ujing wewe,sisi mbeya tumemchagua sugu hatujaangalia alikuwa mwanamziki au mlevi tunachoangalia kazi coz hao wasomi ndo mamburula wa kutosha,nenda arusha jambazi lema kaishika sana,ludewa kichaa lusinde wananchi wanamuelewa na anawapa maendeleo.Acheni kubwabwaja kama wanamoro wanamtaka afande sele atashinda tu wananchi ndo sauti ya mwisho.

Wewe ndiye mjinga Lusinde mbunge wa Ludewa? mburula sana wewe
 
Afande sele hana sifa za kuwa mbunge ameenda kujimaliza huko ACT.
 
Yani chadema bana, mtu akihama chama Chao kawa adui na kupewa sifa za ajabu ajabu.
Watu wanahama dini iweje mtu kuhama chama iwe nongwa acheni ushamba wa siasa uchwara, hata prof . Jay akihama mtaanza kusema mlevi yule mvuta bangi hafai bora hivo kahama wakati sasa hivi mpo kmy.
Jay havui nguo hadharani kama huyu muhuni wenu afande sele
 
Chadema tunashukuru kwa huyo mbwia madawa ya kulevya kuhama na kwenda huko kwa zito.Tulikuwa tunajiuliza hivi aibu hii tutaiweka wapi l
kuanza kumnadi huyu marijuana man.Jimbo muhimu kama la Moro tumpiganie mvuta bangi!.Nenda mwana kwenda tutolee hewa chafu ndani mwetu.

Kwa kweli hata mimi hii aibu ilikuwa inaniumiza sana akili
 
Jamaa usaliti hajaanza leo kumbuka aliwasaliti hata vinega kwenye Ant Virus...huyu anakoelekea Zitto akienda CCM naye Ataenda huko huko.
 
Ile katunj ya bunge iliyowahi chorwa na cartoonist wa kenya ndio nalitazamia sasa kama bunge lijalo.
 
Unajua afande kajipima kwenye mizani kaona hafai ukilinganisha na ushindani uliopo ndani ya chama.
 
Afande sele mzee wa karata dume......karamba

Wengi hawajui kuwa jamaa wanahesabu kali za maslahi. Kupigania haki wameshindwa akina ZZK wameishia kuwa mawakala wa chama tawala ndani ya chama chao kushibsha matumbo sembuse Afande Sele?
 
Tunachoshana tuu. Afande sele amesomea wapi uafande. Morogoro wamesha mkataa kwa kukosa msimamo. Tunahitaji system itakaye tutoa hapa tulipo na kutupeleka kule tunakotaka na siyo mtu. Watu wanakufa bwana nani anajua afande sele au zzk watakufa lini.
 
Uogozi siku hizi umekuwa kama fasheni ya nguo, ndiyo maana kila leo utasikia mara huyu anatanganza nia mara nitagombea ubunge,udiwani mara uraisi. Hii imekuwa kama biashara huria kwa wasaka tonge kujichangulia anapoona pata mfaa kuinusuru njaa yake, lakini kimsingi ukichunguza kiundani hauoni kama wanadhamira ya dhati ya kulete mabadiliko kiuchumi na kijamii bali kinachoonekana ni kutafuta kivuli cha kupumzikia kwa kutumia migongo yetu wananchi.

Mara nyingine najiuliza watu hawa wanapata wapi ujasiri wa kuchagua nafasi za uongozi kama nguo gulioni, kwa nyuma nasikia kuna sauti inaniambia ni kwa sababu ya huruma ya muuzaji(mwananchi) na bei yake ndogo ndio maaana hawa wateja(Viongozi) wetu wanachagua kila nguo waitakayo, kumbe ujasiri huu tunawapa sisi wananchi!!

Hiki ndicho kinachomsukuma na kumpa ujasiri Afande sele wa kuijiona anafaa kuwa Mbunge wa Morogoro, kwa vile anaona tunausikiliza muziki wake, tunakaa nae kijiweni na kugongeana vichungi vya sigara na bangi, Seleman msindi hii haimanishi unasifa ya kuwa kiongozi katika jimbo letu, umefika wakati wa kuulizana umetufanyia nini sisi wana Morogoro , wewe unakidhi utashi wa watu wa morogoro kiburudani lakini siyo mahitaji ya wana morogoro kimaendeleo, urafiki wetu na wewe siyo kwenye sanduku la kura, kwenye maswala ya msingi yanayogusa maisha yetu wana Morogoro hakuna ushabiki kama ule tunaokupazia sauti unapokuwa jukwaani unalewa misifa hadi unavua nguo jukwaani.

Wanamorogoro tumeshaamka na tunakuchora jinsi unavyo hangaika kuhama vyama huku fikira zako umezielekeza tumboni mwako, umechangua nguo ambayo siyo saizi yako, sasa unabadilisha tu vyumba vya kuivalia mara Chadema mara ACT ukidhani itakutosha acha kujidanganya, sisi tunakusubiri tukuvue hiyo nguo tuona ungwana wako ni upi utachutama au utakimbia uchi, utakuja tena masikani tugongeane vipisi vya bangi!!

Kiongozi usie kuwa na msimamo unayefanya siasa kishabiki morogoro ya leo siyo mahala pake tumeshakupima kwenye hili hatukutegemea kuona kilichotokea , usijekusema tumekutuma wana Morogoro au ndio msimamo wetu HAPANA hilo umelifanya kwa utashi na mahaba yako.

Nachukua nafasi hii kuwaasa na wanachi wengine kuchukua tahadhari sana dhidi ya watangaza nia, muwapime na kuwachunguza kwa jicho pevu, tujihadhari na ushabiki kwenye masirahi ya nchi yetu na mustakabali wa maisha yetu ya leo na vizazi vya kesho.

SAUTI YA WANANCHI MOROGORO

Mkuu umetoa maneno ya msingi na yenye busara sana ingawa itaonekana ni machungu kwa Afande Sele aipokee hivyo na hasijidanganye kwa kuangalia matokeo ya Mbilinyi pale mbeya akajiona naye sele anaweza kufanya hivyo hapa moro,
 
CHADEMA bhana!! Kisa Afande Sele Kavua Gwanda na kuwa Mzalendo mnaanza kumshambulia kwa matusi.Mbona alivyovaa Magwanda hayo yote hamkuyaona!!

Siasa sio uadui acheni akili zenu za ufipa. Afande Sele kafuata njia anayoona ni sahihi kwake.

Mbona mapovu yanakutoka kama umelishwa sumu mkuu?mbona cdm ipo kimya juu ya kuondoka kwa msaliti?wewe inakuwasha kitu gani?tulia dawa ikuingie vema na october 2015 ndio mtazimia.
 
Uogozi siku hizi umekuwa kama fasheni ya nguo, ndiyo maana kila leo utasikia mara huyu anatanganza nia mara nitagombea ubunge,udiwani mara uraisi. Hii imekuwa kama biashara huria kwa wasaka tonge kujichangulia anapoona pata mfaa kuinusuru njaa yake, lakini kimsingi ukichunguza kiundani hauoni kama wanadhamira ya dhati ya kulete mabadiliko kiuchumi na kijamii bali kinachoonekana ni kutafuta kivuli cha kupumzikia kwa kutumia migongo yetu wananchi.

Mara nyingine najiuliza watu hawa wanapata wapi ujasiri wa kuchagua nafasi za uongozi kama nguo gulioni, kwa nyuma nasikia kuna sauti inaniambia ni kwa sababu ya huruma ya muuzaji(mwananchi) na bei yake ndogo ndio maaana hawa wateja(Viongozi) wetu wanachagua kila nguo waitakayo, kumbe ujasiri huu tunawapa sisi wananchi!!

Hiki ndicho kinachomsukuma na kumpa ujasiri Afande sele wa kuijiona anafaa kuwa Mbunge wa Morogoro, kwa vile anaona tunausikiliza muziki wake, tunakaa nae kijiweni na kugongeana vichungi vya sigara na bangi, Seleman msindi hii haimanishi unasifa ya kuwa kiongozi katika jimbo letu, umefika wakati wa kuulizana umetufanyia nini sisi wana Morogoro , wewe unakidhi utashi wa watu wa morogoro kiburudani lakini siyo mahitaji ya wana morogoro kimaendeleo, urafiki wetu na wewe siyo kwenye sanduku la kura, kwenye maswala ya msingi yanayogusa maisha yetu wana Morogoro hakuna ushabiki kama ule tunaokupazia sauti unapokuwa jukwaani unalewa misifa hadi unavua nguo jukwaani.

Wanamorogoro tumeshaamka na tunakuchora jinsi unavyo hangaika kuhama vyama huku fikira zako umezielekeza tumboni mwako, umechangua nguo ambayo siyo saizi yako, sasa unabadilisha tu vyumba vya kuivalia mara Chadema mara ACT ukidhani itakutosha acha kujidanganya, sisi tunakusubiri tukuvue hiyo nguo tuona ungwana wako ni upi utachutama au utakimbia uchi, utakuja tena masikani tugongeane vipisi vya bangi!!

Kiongozi usie kuwa na msimamo unayefanya siasa kishabiki morogoro ya leo siyo mahala pake tumeshakupima kwenye hili hatukutegemea kuona kilichotokea , usijekusema tumekutuma wana Morogoro au ndio msimamo wetu HAPANA hilo umelifanya kwa utashi na mahaba yako.

Nachukua nafasi hii kuwaasa na wanachi wengine kuchukua tahadhari sana dhidi ya watangaza nia, muwapime na kuwachunguza kwa jicho pevu, tujihadhari na ushabiki kwenye masirahi ya nchi yetu na mustakabali wa maisha yetu ya leo na vizazi vya kesho.

SAUTI YA WANANCHI MOROGORO

Hapo kwenye RED mkuu tumeelewa kwanini unamsakama huyo Afande Sele!

Siasa bana! Ukiwa upande huu wewe ni mteule na kiongozi mtarajiwa ila ukiamia chama kingine unaonekana mhuni wa kijiweni na mpiga msokoto!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom