Afande Sele na Sheikh Nurdin Kishki nani kakosea?

Shabdullah

Member
Feb 17, 2020
63
125
Habari zenu wana jamii forum.
Pili poleni kwa msiba wa kitaifa.

Nimekuja kwenu kuiongelea ishu ilotokea juzikati kama kichwa cha habari kinavosomeka. Bila ya shaka ishu hii inamuhusu afande sele na mungu na sheikh nurdeen kishki na mungu wake (allah)

Nimefanikiwa kuzisikiliza pande zote mbili, na pia nimesikiliza watoa maoni wa pande zote mbili na nilichogundua ni kuwa watu wanachanganya kati ya uhuru wa kuabudu na kuheshimu dini , na pia baadhi ya watu kukurupuka kutoa maono yao binafsi na kusahau kuwa kila dini ina muongozo wake.

Kwanza nivyema kabla ya kuchangia chochote kwa upande wowote ni lazima ujue afande sele dini yake ni ipi na sheikh dini yake ni ipi?. Yaani usiitolee maoni dini ambayo huijui na huelewi sheria zake., Pili ujue afande sele amemtukana mungu yupi?

Afande sele alimtukana mungu , mungu ambe hajamtaja jina lake haswa ila alongea maneno kama
"mungu",
"god",
"jitu lisilo ona",
na mengineyo.

Pia alitaja sifa za mungu huyo ni:
Haonekani
Hasikii
Hatendi
Anauwa watu tu
Lipo lipo tu.
Muungu wa wazungu

Pia alitaja miungu yake anayoiamini nayo ni:-

Jua
Ng'ombe
Bange

Ila pia alitoa matusi makubwa sana japo kuwa matusi hayo baadhi ya watu hutukanana kawaida na hakuna reaction yyte ile.

Pia afande sele aliomba ushuhuda kuwa anaeamini kama mungu yupo basi apige magoti aombe kuwa yeye (afande sele) afe kama kweli atakufa.

Lakini pia akamalizia kwa kutoa sababu ya kusema aliyoyasema kuwa ni kwasababu ya kifo cha raisi.

Masuala hayo yote ni mazito kwa wale wanaoamini uwepo wa mungu, afande sele hakutaja jina la mungu kwahio kila dini inapaswa kutafakari juu ya kauli ile na matusi yale kwa mungu wake.

Seikh kishki aliongea kulingana na dini yake na kwa jina la mungu wake, so kama huamini uwepo wa mungu ni vyema usichangie kwenye hilo pia kama huamini dini ya uislam ni vyema uongee kulingana na dini yako tu na wala sio kumtoa makosa sheikh ambae itikadi yake haiendani na yako.

Ni kweli nurdiin kishki aliongea kwa jazba na yeye mwenyewe aliliongelea hilo na alimuomba mungu kutokana na jazba hizo.

Nurdiin kishki alimuombea afande sele kifo kma alivoomba mwenyewe kuwa "anaeamini kama mungu yupo basi apige magoti aombe kuwa yeye (afande sele) afe kama kweli atakufa"

Pia sheikh nurdeen alimuomba mungu amuuwe kabla ya ramadhani na amuue kifo kibaya sana na amuangamize. Maneno haya ameyaongea akiwa na jazba na ni kutokana na uzito wa maneno aliyoyasikia kutoka kwenye clip ya afande sele kulingana na imani yake.

Pia sheikh huyu akasema kuwa "sisi tumeudhika tumeumia kutokana na matusi ya huyu jamaa" na akasema kuwa "hatuumii hakika {kwasababu} sisi tunakupenda" aliongezea kwa kusema "yaarabbi tuma jeshi lako kumteketeza huyo mja wako" pia akaomba kwa mungu wake kuwa "nasisi atusamehe kama tumekosea kumuombea dua ya kumteketeza na kumlaani vikali huyu mja wako",

Na alisema kuwa raisi magufuli alikua ni kimbe tu kma viumbe wengine na isiwe sababu ya mipasuko katika taifa hili.

Kiukweli sheikh aliomba dua kwa mungu wake , sheikh huyu hakumuhukumu afande sele sheikh huyu aliomba dua kwa mungu wake ili amuhukumu kiumbe huyu kwa jinsi alivyomtukana mungu,

Kufa kila mtu ata kufa na ni dua aliyomuombea na ndo clip ambayo inatawala kwenye social media na watu kumkisia vikali sheikh kwa kusema kuwa sheikh amekosea zaidi kuliko afande sele, wakasahau kuwa afande sele ndo kasema aombewe afe na sio takwa la sheikh, hilo ni ushuhuda wa afande sele ambao anataaka kuona na kuamini kuwa kweli mungu yupo.

Inashangaza kuona watu wakimkosoa vikali sheikh na wakiacha imani zao zinasemaje na wengine kukosoa kulingana na imani zao lakini wakisahau kuwa wapo na imani tofauti na sheikh.

Watanzania tunapenda kupokea clip fupi fupi ambazo zinaleta maana ya lile tunalolitaka sisi tu na hapo tunatoa comment zetu bila kujua mbeleni kunaongelewa nini au nyuma kumeongelewa nini.

Tujue kuwa kuna uhuru wa kuabudu lakini pia kuna haki ya kuabudu
 
KOKO NI RAS

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
526
500
binafsi yangu mimi niliona jambo moja nikweli kwamba afande sele amekose tena sana tu mungu amrehemu na nilichotalajia toka kwa watumishi wa mungu ni kumjibu afande sele kwa kumuonyesha ukubwa wa mungu bila kumdhihaki wala kumuombea mabaya binafsi ningemjibu hivi.

Ndugu yangu seleman kwanza ningependa utambue uwepo wa mwenyezi mungu mungu ambaye unasema humuoni kufanya wala cjui nn hko nikwambie tu mungu ndie aliyeumba kila kitu mbingu ardhi mpaka huyo magufuri yeye ndio kamuumba lakini pia naomba nikwambie kitu kwamba.

Mwenyezi mungu ni mkwasi sana yaani haitajii chochote kutoka kwa viumbe wake nikiwemo mimi na wewe yaan tumpigie magoti tusimpigie tumsujudie tusimsujudie yeye hapungukiwi chochote mantik yangu ni kukuambia kua mungu akitaka kuwafanyia jambo binadamu wake haitajii msaada wa binadamu wake aliyewaumba mwenyewe nikwambie tu kama mwenyezi mungu anataka tanzania ifike mahala fulani hamuitajii magufuri hamuitajii kasim majariwa yaani yeyete yule hata wewe hakuitajii.

labda nikupe mifano miwili kutoka kwenye vitab vya dini coz nimewah kuwa kwenye ukrsto then uislam najua A to Z.

Mwanzon wakati uislam unaanza ilikua mtu akigundulika kua muislam anatafutwa then anateswa mpaka anakufa na watemi wa maka kipindi hicho mungu akajaalia moja kati ya majitu yenye nguvu naweza sema maka nzima kipind hicho hamza akasilim waislam wakapata hauen kwan hakuna aliyeteswa tena lakin ilikuaje katika vita vya badr aliuwawa kikatil sana inamaana mungu alikua hajui umuhimu wa hamza katika uislam na je kwanini alikubali hamza afe na je baada ya hamza kufa uislam nao ulikufa? jibu ni hapana mungu alitaka tujifunze kua yeye ni mkwasi amuitajii kiumbe si mwanadamu wala malaika

Turudi kwenye biblia nakumbuka kuna nabii mmoja wajuz watanikumbusha alijificha katikati ya mti maadui zake wakagundua kua kajificha kwenye ti wakaupasua katikati mti kwa msumeno kwani mwenyez mungu hakujua kama yule ni mtume alitambua lakini tunaludi pale pale mungu hamuitajii mtu au kiumbe chochote kufanikisha kazi yake na mimi sikuombei ufe mi nakuombea umri mlefu uendelee kuona ukuu wa mungu uliojidhihilisha machoni pako
 
kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,317
2,000
Sele ni chawa blanket limepigwa fumigation lzm aungue na jua.Sheikh ni mapokeo yake mungu wa sele sio Mungu Allah
 
911sep11

JF-Expert Member
Jan 7, 2018
2,363
2,000
Unamaanisha Mungu au mungu? Maana yasemwa kuna tofauti kati ya god na God.

Na je Mungu akiamua kuwa samehe wote Nikimaanisha huyo shekhe na Afande see afu asichukue hatua ypyote nani ataonekana mshindi kati yao?

Bila shaka zitaibuka pande mbili zinazovutia kwao. Upande mmoja utasema unaona? Hakuna mungu kwani hajafanya lolote hata dua waliyoniombea haijafua dafu. Upande mwingine utasema
 
Tuttyfruity

JF-Expert Member
Dec 3, 2017
2,420
2,000
Afande sele hatuwezi kumlaumu sana coz inajulikana ni mvuta bangi. Sasa sheikh mzima kiongozi wa dini mwenye ilmu yake kwanini ajibishane na mvuta bangi.

Wazungu wanasema “Never wrestle with pigs. You'll both get dirty and the pigs like it”. Sheikh kishki sio muwakilishi wa waislamu wote.

Yeye kawakilisha maamuma wa msikiti wake wa oilcom pale vetenari. Infact atuombe radhi waislamu katuchafua. Pia let God fight his own battles, he is mighty enough.
 
Mkongwee

JF-Expert Member
Jul 29, 2018
363
1,000
Afande Sele na huyo Sheikh ni pipa na mfunikoo
tofauti yao ni ndogo mnoooo
tena inakuja baada ya Afande kukuri kosa na kuomba msamahaa
 
Haya_Land

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
5,658
2,000
Afande sele + tatizo lake nibange au nini ?
Je shekh kwanini abishane na mabange km huyo Afande sele.
 
EvilSpirit

JF-Expert Member
Jun 15, 2017
6,438
2,000
"Unajua we sele bange sana" alisikika mbasha akimwambia sele, mara nikasikia mtu amedondoka chini puuu! Kana kwamba amepigwa ngwala.
 
mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
32,466
2,000
Afande sele anasema MUNGU hayupo.
Lakini cha ajabu anatumia pumzi ya mungu,mwili wa mungu,na kazaliwa kwa mpango wa Mungu.
Na atakufa kwa mpango wa Mungu.
 
kawombe

JF-Expert Member
Mar 26, 2015
4,987
2,000
We ndio umekosea!! Unaendelea kuwa nyoshea vidole ikiwa kwako pia hata ujui kusafi kuasi gani
 
Mubarridi

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
22,613
2,000
Habari zenu wana jamii forum.
Pili poleni kwa msiba wa kitaifa.

Nimekuja kwenu kuiongelea ishu ilotokea juzikati kama kichwa cha habari kinavosomeka. Bila ya shaka ishu hii inamuhusu afande sele na mungu na sheikh nurdeen kishki na mungu wake (allah)

Nimefanikiwa kuzisikiliza pande zote mbili, na pia nimesikiliza watoa maoni wa pande zote mbili na nilichogundua ni kuwa watu wanachanganya kati ya uhuru wa kuabudu na kuheshimu dini , na pia baadhi ya watu kukurupuka kutoa maono yao binafsi na kusahau kuwa kila dini ina muongozo wake.

Kwanza nivyema kabla ya kuchangia chochote kwa upande wowote ni lazima ujue afande sele dini yake ni ipi na sheikh dini yake ni ipi?. Yaani usiitolee maoni dini ambayo huijui na huelewi sheria zake., Pili ujue afande sele amemtukana mungu yupi?.

Afande sele alimtukana mungu , mungu ambe hajamtaja jina lake haswa ila alongea maneno kama
"mungu",
"god",
"jitu lisilo ona",
na mengineyo.

Pia alitaja sifa za mungu huyo ni:-

Haonekani
Hasikii
Hatendi
Anauwa watu tu
Lipo lipo tu.
Muungu wa wazungu

Pia alitaja miungu yake anayoiamini nayo ni:-

Jua
Ng'ombe
Bange

Ila pia alitoa matusi makubwa sana japo kuwa matusi hayo baadhi ya watu hutukanana kawaida na hakuna reaction yyte ile.

Pia afande sele aliomba ushuhuda kuwa anaeamini kama mungu yupo basi apige magoti aombe kuwa yeye (afande sele) afe kama kweli atakufa.

Lakini pia akamalizia kwa kutoa sababu ya kusema aliyoyasema kuwa ni kwasababu ya kifo cha raisi.

Masuala hayo yote ni mazito kwa wale wanaoamini uwepo wa mungu, afande sele hakutaja jina la mungu kwahio kila dini inapaswa kutafakari juu ya kauli ile na matusi yale kwa mungu wake.

Seikh kishki aliongea kulingana na dini yake na kwa jina la mungu wake, so kama huamini uwepo wa mungu ni vyema usichangie kwenye hilo pia kama huamini dini ya uislam ni vyema uongee kulingana na dini yako tu na wala sio kumtoa makosa sheikh ambae itikadi yake haiendani na yako.

Ni kweli nurdiin kishki aliongea kwa jazba na yeye mwenyewe aliliongelea hilo na alimuomba mungu kutokana na jazba hizo.

Nurdiin kishki alimuombea afande sele kifo kma alivoomba mwenyewe kuwa "anaeamini kama mungu yupo basi apige magoti aombe kuwa yeye (afande sele) afe kama kweli atakufa"

Pia sheikh nurdeen alimuomba mungu amuuwe kabla ya ramadhani na amuue kifo kibaya sana na amuangamize. Maneno haya ameyaongea akiwa na jazba na ni kutokana na uzito wa maneno aliyoyasikia kutoka kwenye clip ya afande sele kulingana na imani yake.

Pia sheikh huyu akasema kuwa "sisi tumeudhika tumeumia kutokana na matusi ya huyu jamaa" na akasema kuwa "hatuumii hakika {kwasababu} sisi tunakupenda" aliongezea kwa kusema "yaarabbi tuma jeshi lako kumteketeza huyo mja wako" pia akaomba kwa mungu wake kuwa "nasisi atusamehe kama tumekosea kumuombea dua ya kumteketeza na kumlaani vikali huyu mja wako",

Na alisema kuwa raisi magufuli alikua ni kimbe tu kma viumbe wengine na isiwe sababu ya mipasuko katika taifa hili.

Kiukweli sheikh aliomba dua kwa mungu wake , sheikh huyu hakumuhukumu afande sele sheikh huyu aliomba dua kwa mungu wake ili amuhukumu kiumbe huyu kwa jinsi alivyomtukana mungu,

Kufa kila mtu ata kufa na ni dua aliyomuombea na ndo clip ambayo inatawala kwenye social media na watu kumkisia vikali sheikh kwa kusema kuwa sheikh amekosea zaidi kuliko afande sele, wakasahau kuwa afande sele ndo kasema aombewe afe na sio takwa la sheikh, hilo ni ushuhuda wa afande sele ambao anataaka kuona na kuamini kuwa kweli mungu yupo.

Inashangaza kuona watu wakimkosoa vikali sheikh na wakiacha imani zao zinasemaje na wengine kukosoa kulingana na imani zao lakini wakisahau kuwa wapo na imani tofauti na sheikh.

Watanzania tunapenda kupokea clip fupi fupi ambazo zinaleta maana ya lile tunalolitaka sisi tu na hapo tunatoa comment zetu bila kujua mbeleni kunaongelewa nini au nyuma kumeongelewa nini.

Tujue kuwa kuna uhuru wa kuabudu lakini pia kuna haki ya kuabudu
Wote wamekosea ila Kishk amekosea zaidi.

Ajabu ilioje Afande Sele akakiri kosa ila Kishki amekaa kimya mpaka muda huu, au na yeye amekiri kosa ?
 
Shabdullah

Member
Feb 17, 2020
63
125
Kishki alimuomba radhi mungu wake kwa alilolifanya kama amekosea kumuombea dua hiyo selemani na kumuombea balaa.

Lakini yeye amemuomba msamaha mungu wake na sio watz

Maneno hayo utayasikia ukiisikiliza clip ya sheikh hadi mwisho
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom