Afande Sele: Lazima CHADEMA Itashainda Morogoro

Communist

JF-Expert Member
Jun 1, 2012
5,400
1,181
Selemani Msindi (Afande Sele) Jumamosi hii, akihutubia mamia ya wananchi wa Kata ya Kichangani, jimbo la Morogoro Mjini, aliwahakikishia wanachi, kama watashikamana na kusiliza maneno ya busara yanayotolewa na viongozi wa CHADEMA, basi lazima CHADEMA itachukua madiwani wengi na nafasi ya ubunge, Jimbo la Morogoro Mjini. Alieleza sababu za wanamziki wenye upeo mkubwa kuingia katika siasa, kwamba wanasiasa wameziba masikio na hawataki kusikiliza jumbe zao kupitia muziki. Kabla ya kupanda jukwaani alikanusha kabisa, kushiriki katika kuikosoa kamati kuu ya CHADEMA na maamuzi yake, kwani yeye anaipenda CHADEMA, Muundo wake, Katiba na vikao vyake, na hana muda wa kuzungumza mambo yaliyowekwa katika mitandao, yakimhusisha na kauli zisizo za kweli, eti kwamba analaani uamuzi wa kamati kuu. Alisema hizo ni njama zinazopangwa kumchonisha na chama anachokipenda, na kamwe hazitafanikiwa. Kazi imeanza na sasa hakuna kulala mpaka kieleweke. Angalia picha hapa chini.
 

Attachments

  • SAM_0561.JPG
    SAM_0561.JPG
    778.7 KB · Views: 1,751
  • SAM_0566.JPG
    SAM_0566.JPG
    1,013.8 KB · Views: 1,419
  • SAM_0567.JPG
    SAM_0567.JPG
    672.9 KB · Views: 1,258
  • 20131214_153801.jpg
    20131214_153801.jpg
    418.9 KB · Views: 872
  • SAM_0564.JPG
    SAM_0564.JPG
    914.9 KB · Views: 1,230
afande sele yeye avute ndumu zake tu lakini siasa siyo sehemu yake vinginevyo atatia aibu tu.
 
sele anadhani muziki na ubunge ni vitu ambavyo vinafanana kumbe wala hata havishabihiani kabisa.
 
sele anadhani muziki na ubunge ni vitu ambavyo vinafanana kumbe wala hata havishabihiani kabisa.
Akili yako changa sana, soma historia, kuanzia akina mfalme Daudi, walikuwa wanamziki, unamkumbuka Shaba Robert, Unamkumbuka Bob Marley, Meriam Makeba je. Unajua nguvu zao za kisiasa.

Komba wa CCM Vipi?
 
nimekubali mkuu tupo pamoja , lazima sultani afunge virago hapa Moro. Kama anataka kugombea akagombee uarabuni .
 
Kwa sasa Chadema hata ikisimamisha kichaa itashinda. So CCM mna mengi ya kufanya mfno, ondoen folen Dar etc
 
Nyie endeleeni kunywa gongo tu ila mawazo ya kwamba kuna siku mtakuja kutawala nchi sahauni.
Wewe ni nani kwani, mpaka uwapangie watanzania. Mawazo mgando. Kwani ukitaka kupata Gongo, unaangalia bendera ya chama gani. Najua unajua sehemu zinazouzwa gongo zina bendera gani, au unataka nikutajie?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom