Afande Sele amchambua Zitto Kabwe

yamindinda

JF-Expert Member
Jul 29, 2011
1,581
1,317
Katika mahojiano haya ambayo kwa kiasi kikubwa yamelenga kuoanisha suala la maendeleo ya "vitu na watu", Afande Sele amekiri kuwa Zitto Kabwe si mjinga na anafahamu akili na uelewa wake mzuri ingawa ameeleza kuwa kwa wakati huu ambao siasa zimekosa ajenda, basi ni wakati sahihi wa kiongozi huyo wa chama cha ACT- Wazalendo kutafuta ajenda mbadala.

Hoja kama hizi ndizo zafaa wajibiwe wakosoaji na wapinzani,hoja ujibiwa kwa hoja na sio hoja kwa bunduki.Sioni mantiki ya kuwauwa au kuwapa kesi wakosoaji hoja zina nguvu kuliko risasi.Ni kuwajibu kwa hoja ndio uungwana
 
Afande sele nimesikia una mashamba, kwaiyo twende sambamba mwanao nadai tunda...
 
Hauwezi ukatenganisha vitu na watu. Selemani Msindi yupo sahihi.
Hamna anayepinga reli kujengwa ila issue ni concentration. Yaani huwezi tumia % zaidi ya nusu ya bajeti kwenye miundombinu wakati watu wapo taabani. Mfano kilimo ambacho ni tegemeo la 70% ya labor force bajeti ya maendeleo iliotolewa ni chini ya 20% ila nguvu inawekwa kwa kununua ndege ambazo 1% ndio wanaweza nufaika je ni logic??

Inaingiaje akilini serikali ambayo tayari ina mradi wa gesi kufua umeme kuanza tena mradi wa umeme kule stieglers gorge ilihali wanafunzi wanakosa mikopo!!

Kwanini isiwekeze pesa kwa human capital mfano hyo mikopo, au kilimo cha umwagiliaji ama Kutoa mikopo kwa vijana waliomaliza vyuo kujiajiri kwenye masuala mbalimbali ya kiuchumi?

Ni kweli miundombinu ina faida hakuna anayepinga ila miundombinu haitokuwa na faida kama raia hawana uwezo wa kiuchumi kuifaidi mfano NHC imejenga majumba which is fine!! Ila zaidi ya 50% ya nyumba zimedoda sababu wananchi hawana hela.

Serikali iwekeze kwa watu sambamba na vitu,maana watu wakiwa na uwezo watajenga miundombinu kupitia kodi watakozakata hao wananchi.
 
Kingine anachopotosha ni miradi inanufaisha watanzania kupitia ajira!! Unless ni vibarua tu ila chuma,consultancy sijui vifaa 90% ya pesa imeenda nje kwahiyo sidhani kama value ya 10% inajustify faida ya mradi kwa short term labda angeeleza kipi ambacho reli ya sasa imefeli ambacho SGR itakuja solve!!

Pia sio kweli kwamba faida ya pesa za ndege na miradi mingine ndio inarudi kusaidia mikoa ya watu masikini. Anachotakiwa kufahamu toka rais magufuli anaingia madarakani bajeti ya maendeleo haijawahi kamilishwa walau 70% ya malengo mapato huwa yanaishia kulipa madeni na mishahara na ndio maana tunakopa ili kutekeleza miradi. Kilimo ambacho watanzania maskini hutegemea kinatekelezwa bajeti kwa chini ya 20% toka awamu hii iingie sasa ni pesa gani hiyo ya mapato inayoenda kwa maskini??

Anasema mvua zimezidi sababu magufuli amedhibiti ukataji miti!! Miaka 4 miti yake ndio imebadili jiografia ya nchi?? Hvi afande sele hafahamu tu hata aina za mvua?? Hajui hta role ya msitu wa Congo kwenye mvua za Tz??

Ana hoja nyingi ila elimu ndio inamuangusha
 
Nakweli zto cyo wakujibiwa na magufuri wala Dr nahata katibu wa ccm kata! Huyo niwakujibiwa na akina afande sete kwwliii. Mi naona hata wewe cyo saizi yko zito niwakujibiwa na mziki wa diamond wa magufuri baba lao.
 
Ma
Kingine anachopotosha ni miradi inanufaisha watanzania kupitia ajira!! Unless ni vibarua tu ila chuma,consultancy sijui vifaa 90% ya pesa imeenda nje kwahiyo sidhani kama value ya 10% inajustify faida ya mradi kwa short term labda angeeleza kipi ambacho reli ya sasa imefeli ambacho SGR itakuja solve!!

Pia sio kweli kwamba faida ya pesa za ndege na miradi mingine ndio inarudi kusaidia mikoa ya watu masikini. Anachotakiwa kufahamu toka rais magufuli anaingia madarakani bajeti ya maendeleo haijawahi kamilishwa walau 70% ya malengo mapato huwa yanaishia kulipa madeni na mishahara na ndio maana tunakopa ili kutekeleza miradi. Kilimo ambacho watanzania maskini hutegemea kinatekelezwa bajeti kwa chini ya 20% toka awamu hii iingie sasa ni pesa gani hiyo ya mapato inayoenda kwa maskini??

Anasema mvua zimezidi sababu magufuli amedhibiti ukataji miti!! Miaka 4 miti yake ndio imebadili jiografia ya nchi?? Hvi afande sele hafahamu tu hata aina za mvua?? Hajui hta role ya msitu wa Congo kwenye mvua za Tz??

Afande yupo xawa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom