Afande Sele aelezea kwanini akifa anataka mwili wake uchomwe moto - TZA_MillardAyo

youngdonats18

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
685
443
‘Hii ni imani ambayo nimeifikiria muda mrefu na nikajua lazima niifate, kila mtu ana kitu ambacho anakiamini na kwangu naamini moto ndio kila kitu kwenye maisha, kama maandiko yanavyosema Mungu ni moto ulao… naamini moto ndio mfumo ambao hata Mungu anatokana na moto wenyewe‘ – Afande Sele

Kwenye sentensi ya pili Afande amesema ‘wakisema Mungu hajulikani au Mungu hujui ni kitu gani hapo kwangu siwezi kuamini kitu ambacho hakionekani kwa hiyo mimi naamini Mungu ni lile jua linalowaka sababu ndio moto mkuu kuliko mioto yote, sasa kama Mungu ni moto ulao basi mimi napaswa niliwe na moto ule‘

‘Naamini nikichomwa moto nitakua majivu, unaposema Mungu ni moto ulao inamaana mimi moja kwa moja nitakua nimeliwa nimeingia ndani ya Mungu mwenyewe, hata kesho nikifariki nikachomwa moto nikawa majivu, sipendi kufufuliwa kwenye mazingira ya ubinaadamu tena sababu nimegundua ubinaadamu sio kitu kizuri cha kujivunia‘

‘Japo binadamu wanaweza kujivunia sababu ndio wanatengeneza Ndege, Magari na vitu vingine…. binadamu ndio kiume mbaya na muovu, msaliti, mnafiki, batili kuliko kiumbe chochote katika ulimwengu, hata dunia yenyewe itamalizwa na binadamu na sio kiumbe mwingine kwahiyo ili kuukana huu ubinadamu sipaswi kuzikwa kwenye udongo, nikizikwa kwenye udongo manake nitafufuliwa kama binadamu tena kitu ambacho sikitaki‘ – Hayo ni maneno ya Afande Sele msanii wa siku nyingi kwenye muziki wa bongofleva

Kwa kumalizia, Afande amesema ‘Mungu ninaemwamini mimi ni moto na moto mkuu kuliko yote ni jua hata samaki anayeishi chini ya bahari kabisa jua likiwaka asubuhi anatoa mgongo juu inamaana anatoa heshima yake kwa Mungu, hiyo ndio imani yangu na wala simlazimishi mtu mwingine yeyote aamini ninavyoamini mimi, hata familia yangu na watoto wanajua baba akifa anatakiwa kuchomwa moto’

Chanzo: Millardayo
 
Mi mwenyewe nina mawazo kama yake.. Kwanza kwa mazingira point of view ni uharibifu wa mazingira. Thats why wan'gari mathai alichomwa moto
 
afande ana vuta sana bange alihojiwa majuzi tu redioni aka kiri yeye huwa ana puliziamo sana bange huenda ndo zina mfanya mpaka kuongea ivo na kuvua nguo majukwani!?
 
Hana mpya, aendelee Tu kuvaa flana za wanasiasa urasta awaachie wenye imani zao.
 
Hii niimani ambayo mime ifikiria muda mrefu nanika jua lazima nifate,,,kila mtu anakitu anacho kiamini nakwangu mimi naamini moto...ndio kila kitu kwenye maisha, kama maandiko yana sema mungu nimoto ulao....naamini moto ndio mfumo ambao hata mungu ana tokana na moto wenyewe.

-Afande sele.

Naamini niki chomwa moto nitakuwa majivu, unapo sema mungu nimoto ulao...inamaana mimi mojakwamoja nita kuwanime liwa nime ingia ndani ya mungu mwenyewe. Hata kesho nikifariki nika chomwa moto nikawa majivu, sipendi kufufuliwa kwenye mazingira ya ubinadamu tena, sababu nime gundua ubinaadam sio kitu kizuri chaku jivunia.

Japo binadamu wana weza kuji vunia sababu wana tengeneza, ndege, magari, navitu vingine....binadamu ndio kiumbe mbaya na muovu, msaliti,mnfiki,batili, kuliko kiumbe chochote katika ulimwengu hata dunia yenyewe ita malizwa na binadamu nasio kiumbe mwingine kwahiyo ili Kuukana hu Ubinadamu sipaswi kuzikwa, kwenye udongo niki zikwa kwenye udongo, nitafufuliwa kama binadamu tena kitu ambacho sikitaki.

-Hayo nimaneno ya Afande sele.

Kwaku maliza Afande amesema "mungu ninae mwamini mimi ni moto na moto mkubwa kuliko yote ni jua hata samaki anaye ishi chini kabisa ya bahari jua liki waka asubuhi ana toa mgongo juu ina maana anatoa heshima yake kwamungu, hiyo ndiyo imani yangu nawala simlazi mishi mtu yeyote aamini ninavyo amini mimi, hata familia yangu nawatoto wangu wana jua baba akifa ana takiwa achomwe moto.

Mimi nina mpongeza, wewe jee ina maoni gani??.. jewewe ushajiuliza mungu wako yuko wapi au ndio utakae mpinga alafu wewe wakwako huto weza kum dhihirisha??.
 
Muumbaji wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, yeye ndiye anayetoa jua Mashariki hadi Magharibi na wala hana mshirika wake,ana majina yenye sifa tofauti zaidi ya 99.Kwa mujibu wa kitabu chake kitakatifu(Quran)ndivyo nitakavyozikwa.
 
Mi ninachojua na kuamini ni kwamba Afande Sele ni msanii mzuri sana na baadhi ya nyimbo zake kali na zenye madundisho ni hizi hapa....
Mtazamo ft Solo Thang and Prof. J
Darubini kali ft Watu pori
Heshima
Mayowe
Mbele yako ft 20%
Mtu na Pesa
Ndugu zangu
Nafsi ya mtu
Karata dume
Kingdom
Dini tumeletewa ft Belle 9
Miaka kumi ya Rap
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom