Rugas
JF-Expert Member
- Jan 8, 2009
- 1,048
- 196
Kasisi mmoja akiwa anawahi kutoa 'huduma' mahali pa sherehe ya
heshima alisimamishwa na askari trafiki aliyejifanya serious akimzushia
yule Kasisi kwa kukiuka sheria za barabarani. Kasisi alijua hana kosa la kimsingi
isipokuwa mapungufu yasiyoepukika kama ubora wa gari ya kitanzania; mara
tairi moja ni kipara mara gari inatoa moshi mweusi n.k Kasisi akamwambia
trafiki kuwa 'mimi ni father...sio mhalifu wa sheria...'
'geuza twende kituoni" akasisitiza polisi.
Yule kasisi akageuza gari kuelekea 'kituoni'. Walipokaribia yule father
akisononeshwa na kuchelewesha huduma kwa umati unaomsubiri akatamka
'..my God'
'Umesema wee ni 'fwaza ??' akauliza polisi kwa hofu na ujasiri wa sabuni.
Kabla Kasisi hajajibu... 'polisi akawambia kasisi kama anayo BIBLIA apaki
gari pembeni mwa barabara. Yule kasisi akasimama na kutoa BIBLIA ampe polisi.
Polisi akasita kupokea, akamwambia Kasisi 'fungua na usome Matayo 5:25-26
Mtu wa Mungu akasoma "malizaneni na aliyekukamata kukupeleka mahakamani..
..malizaneni upesi.. yamalize mambo haya mngali bado njiani kabla hajakukabidhi kwa hakimu..
ambaye aweza kukuhukumu na kukukabidhi kwa bwana jela ili akutie gerezani. Amin nakwambia
hautaachiwa hadi umetoa senti ya mwisho... Mtu wa Mungu akampa yaliyo yake kaizari. Polisi akatabasamu na kusema 'msifanye migumu mioyo yenu.. nenda na amani.