Afande mwema walioiba pesa za polisi na kuelekeza kwenye account zao wako wapi??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afande mwema walioiba pesa za polisi na kuelekeza kwenye account zao wako wapi???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Apr 17, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,194
  Likes Received: 3,125
  Trophy Points: 280
  JESHI la Polisi limetoa ufafanuzi kuhusu taarifa za wizi wa Sh3 bilioni za posho za askari kwa mwezi Februari mwaka huu.
  Ufafanuzi huo, uliotolewa jana na msemaji wa jeshi hilo, Abdallah Mssika, umekuja baada ya gazeti hili kuchapisha habari iliyoegemea kwenye malalamiko ya baadhi ya askari kuwa posho zao zilichelewa kutokana na wizi uliotokea ndani ya jeshi.

  Kwa mujibu wa askari hao ambao hawakutaka majina yao

  yatajwe, posho hizo zilipwa Aprili 9 mwaka huu.

  Hata hivyo, katika habari hiyo ambayo ndani yake ilikuwa na madai kuwa askari watatu walikamatwa na baadaye kuachiwa, Jeshi la Polisi halikuzungumzia madai hayo licha ya gazeti kufanya jitihada za kupata ufafanuzi kutoka kwa Mkuu wa Polisi, Said Mwema, Kamanda Mssika, kamanda wa polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

  Mwema na Kova, waliiambia Mwananchi kuwa Mssika ndiye ambaye angezungumzia suala hilo na msemaji huyo aliahidi kufuatilia suala hilo, lakini hakutoa taarifa yoyote.

  Hata hivyo, jana Mssika alijitokeza na kuzungumzia suala hilo akisema madai hayo si ya kweli na kwamba ucheleweshaji wa posho hizo ulitokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wa Jeshi la Polisi.

  "Taarifa hizo ni za upotoshaji na tunaamini zina lengo la kulipaka matope Jeshi la Polisi ama kuleta uchonganishi na migongano baina ya askari na familia zao dhidi ya viongozi wao," alisema Kamanda Mssika.

  "Fedha za posho ya mwezi Machi 2010 zilitolewa kwa awamu mbili tofauti kutoka Hazina, awamu ya kwanza ya fedha hizo ilitolewa Machi 22, 2010 kwa hundi namba 28/EB/AG/159/09/522, fedha ambazo zililipwa kwa baadhi ya askari nchini kote," alisema Mssika.
  Alisema hundi namba 28/EB/AG/159/09/548 ilitolewa Aprili mosi mwaka huu na kwamba fedha zake zilitumika kulipa askari waliosalia.

  Msemaji huyo wa polisi alisema hilo lilifanyika mara baada ya kukamilika kwa utaratibu wa kibenki, kwa kuzingatia kuwa kipindi hicho kilikuwa cha sikukuu.

  "Lakini hadi kufikia tarehe nane na tisa askari wote nchini walikuwa wameshalipwa stahili zao," alisema Mssika.

  Wiki iliyopita, baadhi askari polisi kwa nyakati tofauti, walielezea mazingira ya wizi huo na kusisitiza kuwa ngazi za juu katika jeshi hilo, zilikuwa zikificha taarifa hizo kwa hofu ya kuchafua sifa ya chombo hicho cha dola.

  Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao gazetini, walisema fedha hizo ziliibwa na maofisa watatu baada ya kubadili maelezo kwenye hati ya malipo na kuielekeza katika akaunti za mmoja wao.

  Walidai kwamba kilichosababisha siri hiyo kufichuka ni baada ya kuchelewa kwa posho hizo na kusababisha baadhi ya askari kuanza kulalamika kwa maofisa wao wa juu.

  Askari hao, ambao baadhi walifika kwenye ofisi za gazeti hili, walisema kwa kawaida posho hizo zinatakiwa kulipwa tarehe 15 ya kila mwezi, lakini mwezi Februari zilichelewa hadi Aprili 9 mwaka huu.

  "Awali IGP alikanusha tuhuma hizo, lakini ni kweli zilipotea kwa sababu askari watatu waliotuhumiwa kuhusika walikamatwa na kupelekwa kizuizini katika vituo vya Msimbazi na Salender Bridge vya jijini Dar es Salaam," mmoja wa askari hao alisema huku akihoji:
  "Sasa askari wanajiuliza kwamba kama IGP alikanusha tuhuma za wizi huo, kwanini askari hao walikamatwa?"
  IGP Mwema alikataa kuzungumzia kukamatwa kwa polisi hao, ingawa Aprili 8, mwaka huu alikiri kupata malalamiko ya askari kuhusu tukio hilo
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,418
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Afande mwema amekuwa MWEMA kwa wahalifu pia
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,194
  Likes Received: 3,125
  Trophy Points: 280
  Huyu mtu ata sijamuelewa nahisi ni wale wale wakina omar mahita
  wanalimbikiza nyumb akila mkoa kwa kila rpc atakaechaguliwa ananunuliwa na gari kabisa matokeo yake wanatua watoto zao kwa kushidnwa kulipa htaa lakimoja ya matumizi
   
 4. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,919
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mie naona haina hata maana kututangazia wizi wa mabilioni wakati wanajua hawawezi kuwafanya kitu waliochota.inatuongezea uchungu zaidi kwani tunajua mtu hawezi kuiba billioni 3 hiv hiv tu kwa kurupuka lazima wanajuana wote vizuri au hio account ni invisible pia? Wanajua wanachokifanya wote.
   
Loading...