Afande Mambosasa Umetahadhalisha na upotoshaji wa matumizi ya neno utekaji, kuhusiana na Tito Magoti kuwa hakutekwa; Utekaji ni nini?

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,373
73,975
Abduction:
NOUN

  • The action or an instance of forcibly taking someone away against his will.
    eg ‘they organized the abduction of Mr. Tito Magoti on his way to the LHRC offices’ ; ‘abductions by armed men in plain clothes’.

    Najiuliza, Does the above definition match yesterday's action in relation to Tito's fate?

    Najiuliza : Kama mlikuwa na nia njema, Kwanini hamkumtumia wito wa kufika ofisini kwako?




 
Walimteka walipogundua kwamba tukio hilo limeleta taharuki na kuichafua serikali wakabadili gia angani.
Kumbuka hata Kabendera yule mwandishi walikuja kumteka nyumbani kwake, walipojua tu kwamba kamera za usalama zimewabaini wakajidai ni polisi na wakaja na mashtaka ya kipumbaavu kabisa ambayo yamesababisha wamshikilie mpaka sasa.

Kuna jamaa mmoja anajifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda ni njia ya kumtengeneza kwa jambo fulani in the future. Labda pia ni tukio la kijinga lilotoka kwenye vichwa visivyofikiri kwa kina.
 
Kati ya ambao watatumbuliwa kama utani ni miongoni mwa yeye hajui kama anatafutiwa target
 
Mkitaka mabadiliko ya tabia za watu fanyeni kazi ya ziada kubadilisha elimu yetu. Ni sehemu pekee ambayo watoto watafundishwa kuheshimu binadamu wenzao, sheria na kuchukia rushwa. Huwezi leo kulalamika ukamataji wa watuhumiwa wakati miaka yote polisi wanafanya hivyo mitaani hadi jamii imezoea hapa tunaongelea jamii ambayo haigopi kupiga mwizi hadi kufa ambaye hajahukumiwa kisheria. Kwa maneno mengine nyie mtapiga kelele lakini jamii kwa ujumla inawashangaa mnavyopinga jambo ambalo wao wanaona utaratibu wa kawaida.
 
Walimteka walipogundua kwamba tukio hilo limeleta taharuki na kuichafua serikali wakabadili gia angani.
Kumbuka hata Kabendera yule mwandishi walikuja kumteka nyumbani kwake, walipojua tu kwamba kamera za usalama zimewabaini wakajidai ni polisi na wakaja na mashtaka ya kipumbaavu kabisa ambayo yamesababisha wamshikilie mpaka sasa.

Kuna jamaa mmoja anajifa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna raia kwenye uzi wa kutekwa kwake walitabiri kuwa polisi wakiona mambo yamewafika kooni, watajitokeza kukiri. Hizi mambo zinazidi kuitia dosari serikali yetu chini ya rais wetu mpendwa John Joseph pombe Magufuli. Najiuliza, wakati taarifa zinatolewa kwenye vituo vyao mbona hawakusema kuwa wanamshikilia? Soon ataulizwa yalipo makaburi ya babu ya babu ya babu ya babu yake na vyeti vyao.
 
WILE,
Una hoja nzuri sana, ILA sidhani kama jamii inaona kuwa kinachofanywa na polisi/serikali ni sawa! Ni kuwa we are uncivilised, uncooth! hata kama ni mwizi kuna sheria na taratibu za kumshughulikai. Ni kukosa ustaarabu. Shule sawa lkn mbona dini zimekuwepo from time immemorial na zinafundisha hayo unayoyasema! na watu hawajabadilika!
 
Mbona hajawahi kukemea haya mambo? Juzi alisema yule kalitelekeza Jimbo wakati akijua fika yuko kwenye matibabu, tusemeje ,
Mkuu inabidi tu uelewe hivohivo. Mkumbuke Ngugi wa Thiong'o juu ya bif lake na Kenyatta Sr. Inabidi twende na beat, tofauti na hapo tutaharibu muziki. Anyway usimkosoe masihi wa mungu. Ndiye kiongozi wetu angalau tunakula na kupanda ndege.
 
TITO MAGOTI HAJAKAMATWA, AMETEKWA!

Baada ya shinikizo kubwa kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari la kutaka kuachiwa huru kwa Mwanaharakati na Afisa wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Ndugu Tito Magoti, hatimaye Jeshi la Polisi lilijitokeza jana jioni na kukiri kuwa linamshikilia.

Kauli ya Jeshi hilo iliyotolewa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa imeacha maswali mengi bila ya majibu. Taarifa hiyo imesheheni mapungufu mengi ya kisheria na kimantiki. Kwa mazingira yaliyosemwa na Kamanda Mambosasa, ni dhahiri kuwa Ndugu Tito Magoti ALITEKWA na sio kukamatwa na polisi kama anavyosema Kamanda Mambosasa.

Kukamata watuhumiwa (arrest) kunaendeshwa kwa mujibu wa sheria. Jeshi la Polisi haliwezi kumkamata mtu bila kuzingatia sheria. Kwa kilichofanyika kwa Tito, hakina tofauti na utekaji.

Ili atuaminishe kuwa Tito Magoti alikamatwa na polisi kama anavyodai na sio kutekwa, Kamanda Mambosasa atujibu maswali yafuatayo;

1. Kwa nini kuchukuliwa kwa Tito kulikuwa na taswira ya utekaji? Kwa nini watu waliomchukua walimchukua kimabavu akishuka kwenye bodaboda, kumpiga pingu na kutokomea naye kusikojulikana? Kwa nini hawakufuata utaratibu wa kisheria wa kujitambulisha, kueleza kosa na kuondoka naye kiungwana? Tito alikuwa na tishio gani kustahili kukamatwa kama kuku?

2. Tito Magoti ni mfanyakazi anayefahamika wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu. Kwa nini Jeshi la Polisi halikuwasiliana naye aende polisi kwa mahojiano au kumfuata ofisini kwake?

3. Kwa nini Tito Magoti hakupewa haki ya kuwataarifu ndugu, mwajiri na mwanasheria wake kuhusu kukamatwa kwake?

4. Kwa nini kulikuwa na kupishana kwa taarifa za Jeshi la Polisi? Kwa nini Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Mussa Taibu alikana kushikiliwa kwa Tito alipoulizwa na waandishi wa habari mapema baada ya Tito Magoti kuchukuliwa?

5. Kwa nini Kamanda Mambosasa amejitokeza baadaye kwa kuchelewa baada ya msukumo mkubwa kushinikiza Tito aachiwe?

6. Kwa nini Kamanda Mambosasa hasemi Tito yupo Kituo gani?

7. Kwa nini Tito hajapewa haki yake ya kuonana na mwanasheria wake? Anahojiwaje bila kupewa haki ya mwanasheria wake kuwepo?

6. Kwa nini Kamanda Mambosasa hajasema kosa analotuhumiwa nalo Tito?
7. Kwa nini Tito Magoti hajafikishwa mahakamani licha ya masaa 24 kupita tangu achukuliwe?

RAI YETU

Kutokana na mazingira haya tata yanayoligubika suala la kuchukuliwa kwa Tito Magoti, tunatoa rai ifuatayo;

1. Tito Magoti aachiwe huru mara moja.

2. Kama kuna makosa anatuhumiwa nayo, Tito Magoti afikishwe mahakamani.

3. Jeshi la Polisi limpe Tito Magoti haki ya kuonana na ndugu, mwajiri na mwanasheria wake.

Ado Shaibu,
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano na Umma,
ACT Wazalendo.
21 Desemba 2019.
 
Back
Top Bottom