Afande Kova ndani ya KUMEKUCHA ITV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afande Kova ndani ya KUMEKUCHA ITV

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanamayu, Oct 28, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Leo asubuhi 28/10/2010 kwenye kipindi cha kumekucha ITV nimemsikia na kumuona Kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi DSM na pia ni Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi, Sule Kova, akisema yafuatayo:

  1. Sheria inasema mtu akisha piga kura aondoke kituoni na kukaa umbali usiopungua mita 200 mbali na kituo cha kupigia kura. Ila anasema heri nusu shari kuliko shari kamili akimaanisha ni vizuri kusubilia matokeo nyumbani,

  2. Vyama vya siasa kupeleka walinzi wao kwenye vituo vya kupigia kura ni kinyume na utaratibu na italeta vurugu, kwani polisi, JKT na mgambo wamejipanga vyema na amesisitiza ulinzi shirikishi yaani wananchi watoe taarifa mara wanapo ona viashiria vya kuvunja sheria - tutatumia na helkopta,

  3. Mawakala wa vyama vya siasa ndio walinzi wa kura,

  4. Kwenye ushindani kuna kushinda au kushindwa, hivyo hayo yote yanaweza kutokea kati ya wagombea,

  5. Polisi watahakikisha uchaguzi ni wa amani, huru na salama

  Huyu kamanda je, ataweza kuwamudu Green Guard? Sheria kweli inasema ukisha piga kura ukae si chini ya mita 200 kutoka kituoni? Au kutamka kwake tayari ni mwongozo? Hivi hajui kama uchaguzi unatakiwa kuwa 'huru, haki, wazi, salama, na amani'? Sasa yeye ameacha 'haki'. Je, ujumbe namba 4. anapelekea na akina Kinana, makamba, JK?

  Kova naye anatambua ulinzi wa kura unafanywa na mawakala wa upigaji kura; hivyo basi ushindi wa wagombea unategemea sana umakini, uadilifu na uaminifu wa mawakala. Langu: mawakala wa vyama vya upinzani ndio watanzania watakaolifanya taifa letu kuwa nchi ya asali na maziwa au jangwa/nyika!
   
Loading...