Afadhali mara 100 ametekwa ROMA, ukweli utajidhihirisha

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Kwanza niseme serikali hata ingejiosha kwa brush ya chuma hakuna anayeweza kuwaamini. Kwa hiyo waache kupoteza muda kukanusha au kufanya propaganda.

Serikali ni suspect namba 1 na kama hawakumteka wao basi ndiyo wawajibikaji namba 1 wa usalama wake na wenzake. We want Romaa live!

Lakini mi nasema afadhali ametekwa ROMA maana kelele nilizosikia na nazotarajia kusikia si za mchezo. Tv zote za burudani jana zilikuwa na vipindi maalumu, wasanii waliungana kutoa tamko na mawaziri kadhaa tumeona maoni yao

Redio nimeambiwa mpaka za vijijini zinacheza miziki yake na kushinikiza apatikane. Magazeti yote, mitandao ya kijamii na kwa kuwa kesho ni Jumapili natarajia kauli kali toka kwa viongozi wa dini.

ROMA kama amekufa au yuko hai, alichofanya ameunganisha nguvu ya watanzania ktk kudai haki ya kiusalama na kukemea vitendo ambavyo havijazoeleka kwenye nchi yetu TAKATIFU.

[HASHTAG]#WAKINAROMAWAKOWAPI[/HASHTAG]
 
Mkuu leo sio jumapili, rekebisha brain kalenda. Ingawa tusubiri madereva amesema Roma atarudi kabla ya jpili atakua anajua alikompeleka.!
###bringback Roma###
 
Kwanza niseme serikali hata ingejiosha kwa brush ya chuma hakuna anayeweza kuwaamini. Kwa hiyo waache kupoteza muda kukanusha au kufanya propaganda.

Serikali ni suspect namba 1 na kama hawakumteka wao basi ndiyo wawajibikaji namba 1 wa usalama wake na wenzake. We want Romaa live!

Lakini mi nasema afadhali ametekwa ROMA maana kelele nilizosikia na nazotarajia kusikia si za mchezo. Tv zote za burudani jana zilikuwa na vipindi maalumu

Redio nimeambiwa mpaka za vijijini zinacheza miziki yake na kushinikiza apatikane. Magazeti yote, mitandao ya kijamii na kwa kuwa leo ni Jumapili natarajia kauli kali toka kwa viongozi wa dini.

ROMA kama amekufa au yuko hai, alichofanya ameunganisha nguvu ya watanzania ktk kudai haki ya kiusalama na kukemea vitendo ambavyo havijazoeleka kwenye nchi yetu TAKATIFU.

[HASHTAG]#WAKINAROMAWAKOWAPI[/HASHTAG]
Mkuu Leo siyo jumapili Leo ni jumamosi.Kwa habari ya Roma ninaomba hawa watumishi wa mungu waache kujipendekeza kwa serikali ni bora waiambie kweli. Wanapotea raia wao wapo kimya.
 
Mkuu leo sio jumapili, rekebisha brain kalenda. Ingawa tusubiri madereva amesema Roma atarudi kabla ya jpili atakua anajua alikompeleka.!
###bringback Roma###
Thanks kwa marekebisho
 
cjui ulikuwa unaandika huku unakimbizwa...
Alafu tuseme kapatikana Jumapili....hivi unategemea atasema nn...zaidi yakumshukuru Mungu kaokoa uhai wake..
Au unauchukulia huu utekaji kama Bongo Movie...??
 
cjui ulikuwa unaandika huku unakimbizwa...
Alafu tuseme kapatikana Jumapili....hivi unategemea atasema nn...zaidi yakumshukuru Mungu kaokoa uhai wake..
Au unauchukulia huu utekaji kama Bongo Movie...??
Vyovyote itakavyokuwa, nachosema mimi ni solidarity iliyoonyeshwa na watanzania na nadhani ni mwanzo mzuri wa kukutaa vitendo hivi haramu
 
Mi sielewi. Huyu ana lipi la maana mpaka atekwe na Serikali?
Amefanya nini cha kutishia USALAMA WA TAIFA LETU?
Acheni hizi kiki za aina hii
 
Mkuu leo sio jumapili, rekebisha brain kalenda. Ingawa tusubiri madereva amesema Roma atarudi kabla ya jpili atakua anajua alikompeleka.!
###bringback Roma###
umewahi kumjibu mkuu, ungemuuliza yupo wapi, jf kokote ulipo inakufikia, huenda jamaa yupo LINE ISLANDS
 
Mi sielewi. Huyu ana lipi la maana mpaka atekwe na Serikali?
Amefanya nini cha kutishia USALAMA WA TAIFA LETU?
Acheni hizi kiki za aina hii
Mkuu subiri yakukute kwenye family yako halafu upost kama ulichopost watu wanauchungu na damu yao Mungu akusamehe yawezekana ulijui ulitendalo au akili yako bado ni changa.
 
Mi sielewi. Huyu ana lipi la maana mpaka atekwe na Serikali?
Amefanya nini cha kutishia USALAMA WA TAIFA LETU?
Acheni hizi kiki za aina hii
Ney alikuwa na lipi mpaka akatekwa na polisi na kumsafirisha Moro to Dar?
 
Nimesikia tukio hili wahanga ni watu wanne, kwa nini tunalia na ROMA tu wengine hawa sio muhimu wapatikane? Kama mbaya wa Serikali ni ROMA kwa nini iwachukue na hawa wengine?
 
kwa mtu kama roma mwenye kuweza kumchukua ni polisi leo polisi wanasema hawana taarifa inatisha sana
 
Vyovyote itakavyokuwa, nachosema mimi ni solidarity iliyoonyeshwa na watanzania na nadhani ni mwanzo mzuri wa kukutaa vitendo hivi haramu
Kipi bora kati ya Solidarity ya kinafiki na Solidarity ya kweli toka moyoni...????
Uzalendo na umoja wa taifa aliefanikiwa kuujenga kwa kiwango cha juu ni Mwl tuu..
Labda awamu hii Kitila Mkumbo atasaidia kuujenga tena
 
Back
Top Bottom