Afadhali changudoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afadhali changudoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ngoshwe, May 16, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Unaanza nae vizuri ukidhani atakufaa hapo mbeleni lakini mh!.
  Siku zinapozidi kwenda mbele unaona kamba inavutika zaidi upande mmoja:
  1. baada ya siku tatu tu za mahusiano yenu alikuomba umnunulie simu. simu aliyokuwa nayo anaifunga kwa "mipira kama ile ya kufungia hela" betrii inachomoka kila wakati, haina network, ya rangi ya siliver lakini imefuba balaa!,. Unaona ni muhimu kumnunulia simu lakini anasema umpe tu hiyo hela ataongezea apate nzuri zaidi, Lakini unapokutana nae kesho yake una unaona aina ya simu aliyonunua haina hadhi ya thamani ya pesa uliyompa.
  2. Pengine anakutumia sms kukuomba umtumie vocha ili mpate pia kuwasiliana
  3. ukiwa una uhakika kabisa kuwa vocha ya dola 10, lakini wewe hakupigii kamwe, ataishia "kukubip". Ukiuliza "why"...anajibu eti iliishia kumpigia mama yake!.
  4. Anafanya kazi, lakini kila mkikutana akitana kuongeza na mtu anataka kutumia simu yako tu ya kwake anasema haina credit.
  5. ukimwitaji aje kwako angalau kwa "tendo" anakuja kwa taxi, unalipa, mtakula, kumnywa, ila ukimgusa tu anakuambia "nipo katika siku zangu au sijisikii vizuri"..
  6. atataka mtoke kwenda kwenye starehe (club), ataomba hela ya kwenda saloon,ataomba ya taxi nk..
  7. Ukiwa club utalipa kiiingilio, vinywaji na kila zaga zaga mpaka siku iishe. Ukisema huna kitu atanuna na kuona unambania tu. Furaha itaishia hapo, mtakorofishana na ataondoka pasipo hata kuaga.
  8. Siku ambayo wewe upo "bize" yeye kwake anaona unamkimbia, ukimpigia simu hapike, au pengine kakuzimia kabisa.... Ukisema uende kwake hayupo, unaambiwa katoka na wenzake.
  9. Siku akikuomba umsindikize sehemu akanunue kitu, atachagua na kuelekeza wewe ndio ulipe....
  10. Ikiwa yakaribia sikukuu, anataka mwende "shopping",ukimchagulia kile ambacho wewe unaona atapendeza, anakumbia yeye hawezi kuvaa hilo "lapu lapu" atachukua ile ambayo kuilipia huwezi kutoka bila maumivu...ukikataa, kesho yake utaona kaivaa hiyo hiyo hujui alinunua saa ngapi!.
  11. Pengine atakuja na simulizi za shida kibao za kwao, utamwonea huruma umsaidie..lakini ukimweleza leo huna kitu kwa kuwa umetuma kiasi kwa mzazi wako unaona sura yake inabadilia, hanakuwa hana furaha kabisa....
  Pengine unaona ni heri ya kutafuta changudoa tu, una malizana nae hata kama ni gharama kubwa inaeleweka yupo kibiashara na utakuwa mwangalifu zaidi kuliko sehemu unayojiamini kuwa kuna penzi na inafika wakati ukajikuta unajeruhiwa wewe tuuu na kuumizwa moyo!.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Swali:We hawa warembo unawapata wapi???:yuck:

  Kama umekutana na zaidi ya mmoja wa aina hii...nakushauri ubadilishe sehemu unazeotembelea (ulipobahatika kukutana nao), coz wanaonekana wako kibiashara zaidi,au wanyonyaji kwa jina jingine.
   
 3. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Ngoswe ina mana na wewe unapigika mizinga kiivyo?! Mwanamke mstaarabu kama anakupenda hawezi kukugeuza ATM kiasi hicho!...Endelea kuangaza utakutana na sampo nyingine tu ila CD hapana..
   
 4. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,025
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Hii nzuri i etulia
   
 5. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,445
  Likes Received: 2,031
  Trophy Points: 280
  kaka utafute changudoa wa nn wakati huyo uliyenae ni changudoa

  Definition ya changudoa kutoka kwenye kamusi ya Kiswaili
  1. Samaki anayejipeleka mwenyewe kwa mvuvi
  2. Mwanamke anayefanya mapenzi kama biashara

  kwa hiyo definition ya pili huyo wa kwako amegeuza wewe ni mtaji wa matatizo yako (wale wale tu)
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Inabidi uwe unafanya 'due diligence' kabla hujaamua kuwa nao karibu hivyo! Kama uko makini mwanamke wa jinsi hiyo unaweza kumjua mapema sana kabla hata hajakuchuna kiasi hicho.
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Lakini pamoja na yote hayo Changudo ni Changudoa tu.
   
 8. R

  Renegade JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,765
  Likes Received: 1,068
  Trophy Points: 280
  Pole kaka tafuta mwanamke aliyetulia uoe.
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Pole sana kama ni kitu cha kweli kimekukuta ndugu.
  Naomba kuuliza swali la kizushi..... watu kama hawa mnakutana nao wapi?
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  malalamiko yako yote ni ya kujitakia ..........na waswahili wanasema jambo la kujitakia haliambiwi pole.
   
 11. ngonzi zomukama

  ngonzi zomukama Senior Member

  #11
  May 17, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh! pole sana! ila nadhani hzo tayari ni sifa za changudoa
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  May 17, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  1. Maofisini tunakotafuta mkate wetu wa kila siku
  2. Kwenye Harusi/Send Off Party ambako ni "biggest outing" of our times
  3. Baa au Club ambako ndiyo sehemu maarufu zaidi kuwapata
  4. Kwenye Nyumba za ibada
  5. Kwa kupigiwa "cross" na rafiki
  6. Kwa kuunganishiwa na rafiki au ndugu
  7. . . .
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  May 17, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Inatisha kweli!
   
 14. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #14
  May 17, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kwa mtaji huu vijana mtajenga kweli?
   
 15. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #15
  May 17, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  wanafunzi ndio wana haka katabia ka mizinga.

  Ila kuema kweli inategemea wewe mwanaume ume muapproach vipi mwanamke ukiingia kwa kujisifia na wengine hukodi hata magari ya kifahari ili tu waonekane wako juu basi hapo unageuzwa mtaji.
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  May 17, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mpwa acha kudate wanafunzi!
   
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  May 17, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,977
  Likes Received: 23,681
  Trophy Points: 280
  Nikiwashauri vijana wajiunge kwenye chama changu cha kustarehe na mabaamedi wala hata hawanielewagi.

  Acha wachunwe, si wanajitakia wenyewe?
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  May 17, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mwanamme wengi wao huwa wanataka tendo tu kwa mwanamke na mwanamke nae anataka mtaji tu kwako...............kama tit for tat flani hivi
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  May 17, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  I like dating cougars! lol
   
 20. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #20
  May 17, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Tafwadhali nitake radhi naiheshimu sana ndoa yangu takatifu na naogopa kuikashifu vile ilitiwa wakfu na askofu.
   
Loading...