figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,888
Heshima kwenu wakuu,
Nilikuwa namsikiliza Mbunge wa jimbo la Sumbawanga mjini, Aeshi Hilaly, akiuliza kuhusu Shisha.
Namnukuu
"Napenda kuuliza Waziri wa Fedha yupo hapa na Waziri wa Mambo ya Ndani yupo hapa. Shisha hii ni haramu? Shisha hii ni madawa ya kulevya? Na kama ni madawa ya kulevya, kwanini TRA mnakusanya kodi"? Kwanini ile tumbaku inavyofika bandarini mnakusanya kodi?"
"Na kama ni madawa ya kulevya Waziri Ummy yupo hapa naye atujibu. Kama Shisha inatumika vibaya hata sigara inatumika vibaya. Sigara watu wanaweka bangi mle. Ni kazi ya Polisi kuhakikisha ile shisha haitumiki vibaya."
"Sasa lakini leo tunaipiga marufuku, anatoka tu mtu huko sijui kagombana na mke wake...ooh..Mpenzi wake anakuja kusema shisha marufuku."
"Na hiyo Marufuku ya shisha ipo Dar es Salaam peke yake. Ukienda Arusha wanavuta Shisha, Ukienda Dodoma hapo wanavuta shisha, ukienda sehemu nyingine wanavuta."
"Sasa Mimi nataka nikuombe mheshimiwa Waziri, kama shisha hii ni madawa ya kulevya, tuipige marufuku leo na kwenye kodi tuiondoe. Maana kwenye kodi imo na ukiwauliza hawa TFDA wanasema haina madhara. Ukimuuliza mkemia mkuu anasema haina madhara."
"Ukienda nchi za kiarabu wanavuta, ukienda Uingereza wanavuta. Yaani dunia nzima wanavuta kasoro Dar es Salaam tu. Nasema liangalieni hili, tusiwaumize wananchi, kuna watu wanalipia kodi Dar es Salaam lakini ikitoka inapigwa marufuku. Ameongeza Mbunge huyu."
Mwisho wa Kunukuu
My Take
Nakubaliana na Mawazo ya Mbunge. Watu wanataka Dar es Salaam tuishi kama Mashetani, haikubaliki hii. Kodi tunalipa, kutumia tunakatazwa.
Hongera sana