Aeshi Hilaly: Kwanini Shisha imepigwa marufuku lakini bado mnatoza Kodi?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,721
2,000
Heshima kwenu wakuu,
Shisha-800x600.jpg

Nilikuwa namsikiliza Mbunge wa jimbo la Sumbawanga mjini, Aeshi Hilaly, akiuliza kuhusu Shisha.

Namnukuu

"Napenda kuuliza Waziri wa Fedha yupo hapa na Waziri wa Mambo ya Ndani yupo hapa. Shisha hii ni haramu? Shisha hii ni madawa ya kulevya? Na kama ni madawa ya kulevya, kwanini TRA mnakusanya kodi"? Kwanini ile tumbaku inavyofika bandarini mnakusanya kodi?"

"Na kama ni madawa ya kulevya Waziri Ummy yupo hapa naye atujibu. Kama Shisha inatumika vibaya hata sigara inatumika vibaya. Sigara watu wanaweka bangi mle. Ni kazi ya Polisi kuhakikisha ile shisha haitumiki vibaya."

"Sasa lakini leo tunaipiga marufuku, anatoka tu mtu huko sijui kagombana na mke wake...ooh..Mpenzi wake anakuja kusema shisha marufuku."

"Na hiyo Marufuku ya shisha ipo Dar es Salaam peke yake. Ukienda Arusha wanavuta Shisha, Ukienda Dodoma hapo wanavuta shisha, ukienda sehemu nyingine wanavuta."

"Sasa Mimi nataka nikuombe mheshimiwa Waziri, kama shisha hii ni madawa ya kulevya, tuipige marufuku leo na kwenye kodi tuiondoe. Maana kwenye kodi imo na ukiwauliza hawa TFDA wanasema haina madhara. Ukimuuliza mkemia mkuu anasema haina madhara."

"Ukienda nchi za kiarabu wanavuta, ukienda Uingereza wanavuta. Yaani dunia nzima wanavuta kasoro Dar es Salaam tu. Nasema liangalieni hili, tusiwaumize wananchi, kuna watu wanalipia kodi Dar es Salaam lakini ikitoka inapigwa marufuku. Ameongeza Mbunge huyu."

Mwisho wa Kunukuu

My Take

Nakubaliana na Mawazo ya Mbunge. Watu wanataka Dar es Salaam tuishi kama Mashetani, haikubaliki hii. Kodi tunalipa, kutumia tunakatazwa.

Hongera sana
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,133
2,000
Watu wenye pesa wengi wao wanaipenda SHISHA.Kama inalipishwa kodi,ihalalishwe.
 

tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,195
2,000
Kumjadili aliyeipiga marufuku Shisha jijini kwake Dar sio kosa? Huyu si mwana mpendwa wa nanii? Nafikiri ni marufuku kumjadili huyu mkuu wa wakuu wa mikoa
 

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
4,121
2,000
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dar es salaam ameshashema marufuku.
 

AirTanzania

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
1,139
2,000
Kuwa kiongozi Tanzania haiitaji uwe na cheti cha darasa la saba hata kama hukwenda shule utaiiongoza. Kuwaongoza Watanzania ni sawa na kuwaongoza kondoo, hawajitambui na wala hawajijui. Weka sheria yoyote wataifuata bila ya kuipinga au kuuliza, Taifa wananchi wake wasiojitambua kila kiongozi anaweka sheria zake na zinafuatwa bila ya kudadisiwa au kupingwa. Hata ukiwa kichaa utaiongoza Tanzania kwani nchi yenyewe wananchi wake hovyo kuliko wendawazimu
 

R Mbuna

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,198
2,000
Kuwa kiongozi Tanzania haiitaji uwe na cheti cha darasa la saba hata kama hukwenda shule utaiiongoza. Kuwaongoza Watanzania ni sawa na kuwaongoza kondoo, hawajitambui na wala hawajijui. Weka sheria yoyote wataifuata bila ya kuipinga au kuuliza, Taifa wananchi wake wasiojitambua kila kiongozi anaweka sheria zake na zinafuatwa bila ya kudadisiwa au kupingwa. Hata ukiwa kichaa utaiongoza Tanzania kwani nchi yenyewe wananchi wake hovyo kuliko wendawazimu
Na ndio tunaoongoza kukipenda chama tawala sisi watu wa hovyo kila anayepata elimu lazima aone haya mapungufu na kutamani mabadiliko.

Ili kupunguza wasomi kwenye hii nchi wakaona walete hiyo elimu bure ili watoto wetu wasielimike zaidi maana kukiwa na taifa la Tanzania lenye wasomi wengi hawa wenye hatimiliki ya nchi watalima kwa meno.
 

Mdakeo

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
556
1,000
Huyu si ndie aliesema anaogopa kwenda Dar kutokana na tishio la mwanamfalme?? Ameanza tena kumchokonoa mwanamfalme?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom