Aeleza walivyokubaliana na mume wake kutafuta watoto nje ya ndoa

Dar es Salaam. Mkazi wa Tabata Liwiti, Magreth Silaeli (37) ameieleza Mahakama ya Mwanzo Buguruni kuwa walikubaliana na mume wake, Raymond Kulaya (44), waachane kwa muda ili kila mtu akatafute watoto “anapopajua” baada ya kuishi miaka mitano bila kupata mtoto.

Magreth sasa anaiomba mahakama itoe hati ya talaka, ili aweze kuolewa na mwanaume anayeishi naye, baada ya kutengana kwa muda na Kulaya.

Alidai mbele ya hakimu Matrona Luanda kuwa yeye na Kulaya walitengana tangu mwaka 2011.

Alidai alifunga ndoa ya Kikristo na Kulaya mwaka 2006 mkoani Kilimanjaro na waliishi pamoja kwa miaka mitano bila kupata watoto.

Magreth alidai wakati anaolewa na Kulaya alimkuta tayari na watoto wawili, lakini katika kipindi chote walichoishi pamoja hawakubahatika kupata watoto.

Alidai mwaka 2011 mume wake alimueleza kuwa wamekaa kwa muda mrefu bila ya kuwa na watoto na kumwomba watengane ili kila mtu aende akatafute watoto.Alidai katika kipindi walichoishi pamoja, familia ya ndugu wa mwanaume ilikuwa inawasumbua kuhusiana na watoto na kuwasababishia

“Mimi nilikuwa naumia sana kwa kuwa nilikuwa sijapata mtoto, angalau mwenzangu nilimkuta na watoto wawili, mwishowe mume wangu aliniambia tutengane kwa muda ili kila mtu aende akatafute watoto anakojua,”alidai Magreth

Aliiambia mahakama kuwa kutokana na kutopata mtoto, Kulaya alimweleza kuwa ni bora kila mtu aende upande mwingine kwani atakapoleta mwanamke mwingine ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi pamoja hataweza kumuelewa.

“Mimi nilienda kuishi na mwanamume niliyenaye leo na tumebarikiwa kupata watoto wanne,” alisema.

Magreth alidai yeye na Kulaya walitengana kwa makubaliano hawakuwahi kuwa na ugomvi na sababu kubwa ya kutengana ilikuwa kukaa muda wa miaka mitano bila ya kupata mtoto.

“Kwa kuwa mwanaume ninayeishi naye alinikubali na aliniliwaza wakati nikiwa katika hali ya unyonge na nimezaa naye watoto wanne, naiomba mahakama hii itoe talaka ili mimi niweze kufunga ndoa na mwanaume niliyezaa naye,”alidai Magreth.

Kwa upande wake, Kulaya ameieleza mahakama kuwa aliishi na mke wake Magreth kwa miaka mitano na hawakujaliwa kupata watoto.

Alidai mwaka 2011 yeye na Magreth walijadiliana na kukubaliana watengane kwa muda ndipo mke wake alipata mwanaume ambaye alizaa naye watoto wanne huku yeye akizaa na mwanamke mwingine watoto watatu.

“Yaani mimi nipo tayari hata leo hii mke wangu nirudiane naye na sina chuki naye na ninawakubali watoto wake nitawapokea, hivyo naiomba mahakama hii itakapotoa maamuzi yake itumie busara kwa hili,”alidai Kulaya. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 17, 2021 kwa ajili ya hukumu.
Wataalamu wa betting hii tuiitaje.

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Haya yote ni yanatokea kutokana na sheria mbovu za ndoa, miaka mitano wametengana, bado usumbufu wa kwenda mahakamani, bado watarudi kuulizwa mlipata nini wakati mnaishi ndani ya hizo ndoa tatu. haya yangeishia kwa Mwanasheria wa Serikali basi, mambo kama haya yanawafanya watu Wengi masikini.
 
Kumbuk
Kumbuka walikubaliana kufanya hivyo. Kwa maoni yangu naona hakimu awaamuru wakakae tena kujadili matokeo ya makubaliano yao ya mwaka 2011. Wapitishe maamuzi mapya kwa pamoja then mahakama ije kuyabariki
Mkuu kumbuka wameongezeka - watoto saba na wazazi wawili- hilo ni bunge tena lenye upinzani mkali
 
Back
Top Bottom